Ni kosa la jinai kuipinga tume ya katiba

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
kuna kipengele katika muswada wa uundwaji wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kwamba ni kosa la jinai kuhoji au kupinga au kukebehi maoni/maamuzi ya tume. Imekaaje hii?
 
kikwete ameanza kuchakachua huu utaratibu muhimu ambao sisi wananchi ndio wenye mamlaka ya kuamua ni kwa namna gani tunataka tujitawale.
 
Hata mimi hii imenishangaza, ina maana hata wakikosea hakuna kuhoji!!
 
Muswada unapoanza kunyonga uhuru wa kutoa maoni (Freedom of expression) tangu siku ya kwanza tutafika?
 
kuna kipengele katika muswada wa uundwaji wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kwamba ni kosa la jinai kuhoji au kupinga au kukebehi maoni/maamuzi ya tume. Imekaaje hii?

Duh kama ni hivyo tunatakiwa kuanza kupinga hicho kipengele kabla huo muswada haujapitishwa..
 
Nadhani tuanze kwanza kupinga muswada huo kabla hatujaendelea na mchakato wa kupata Katiba mpya. Hapo ndo naona lile swala la mtu kuogopa kivuli chake sasa anatafuta jinsi ya kukificha asikione!!!!!
 
huo ni udikteta. muswada wenyewe werema kakopi toka kwa amos wako wa kenya.:disapointed:
 
Hivi mnategemea nini kumpa mamlaka fisi alinde butcher? Elewa kwamba baada ya kutokuwa na ruhusa ya kupinga matokeo ya kura za urais, sasa linakuja kwamba hakuna kuhoji tume ya katiba. Itakalosema, wadanganyika wote mseme kwa heruf kubwa "AMIN".

Kwa mwanzo huu, tegemeeni katiba inayokuja ndiyo itakuwa imelinda mambo mengi sana ya ovyo!.

MUNGU TUSAIDIE WATANZANIA WENGI TUSIOKUWA NA MTETEZI.
 
Back
Top Bottom