Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,803
- 59,283
- Thread starter
- #41
Sijui nikuelezeje rafiki yangu,mapenzi ni kitu cha ajabu sana na mwanzo mara nyingi huwa ni mtamu hata uambiwe mwenzako kikojozi,mwizi,mbinafsi nayote uliyorothesha unaweza ukakataa sasa mambo hugeuka siku baada ya siku huwa sielewi ni nini?.......inaweza kuwa kuchokana,kuzoeana sana na kuona hakuna jipya au mapenzi kupungua/kwisha hapo ndo huwa tunaanza kuhesabiana kila kosa tunalofanya siamini ale tunayoona kwa wapenzi wetu leo yameanza sasa mengi ni tabia wlizokuwa nazo toka tunakutana
Nimekuelewa ila kusema kwamba yanayoonekana baadae yanakua tabia ambazo zilikuwepo tangu mwanzo napingana na wewe maana kwa kiasi kikubwa mapenzi yanapoanza kila mmoja hua anafocus kwenye kumfurahisha/kumridhisha mwenzake.Kama anatabia za kufoka foka wala hutojua...kama ni mvivu wala hutogundua...kama ni mgomvi ndo kabisa hatokuonyesha mpaka siku atakapochoka kuficha uhalisia wake ndo unashangaa ghafla ukirudi nyumbani jiko limenuna..kila unachofanya anagomba...akikasirika kidogo mkono hewani na matusi juu.Hamna mtu hata mmoja anaeweza kuanza mahusiano na uhalisia wa aina hiyo...hua yanakuja baadae mtu anapoona kwamba ameshakuweka mkononi/kitanzi cha ndoa na vitu kama hivyo.Ndo maana watu hawaishi kulalamika kuhusu makucha ya wenzi wao yanavyochomoza baada ya kuwekana kwenye himaya!
Pili...jiulize kama mtu alianza kwa kujionyesha kwamba hana hizo tabia ambazo zinachomoza baadae kwanini asiendelee kuzificha kama kweli anakuthamini/penda na hataka kukuumiza au kukukera?!Maana tayari unajua kwamba anaweza sana kuzuia hasira zake pale inapombidi (wakati wa kukuchombeza )....nini kinamfinya aziachie wakati huo kama sio amekuchoka?!Owkey unaweza ukampatia visingizio kibao kmf..alishindwa kujizuia na bla bla kibao...mara moja na mbili kisingizio kinaweza kumaliza tatizo ila inakuwaje pale anapoendelea na kurudia kitu kile kile mara nne tano huko?!