Ni kitu gani...?!

Kwa habari ya uzinzi ndoa yaweza vunjwa..dada vigezo umevipanga vizuri..ili kuepuka yoote haya huyo mwenzi kabla ya ndoa ni vizuri umchunguze ktk; anahofu ya Mungu?,ni ideal kwako?,umri na elimu je?,mahusiano na wazazi wake je? nk..lizzy bila ya vetting kwa watarajiwa..ndo malalamiko haya yasiyoisha ktk ndoa/mahusiano..

May be,

Stringent vetting kwenye ndoa inaweza kuwa imekaa kinadharia zaidi!! Naamini kuna watu wamefanya vetting ya nguvu na kwa gharama kubwa sana lakini wameishia kusambaratika kabla ya first anniversary!!

Hadi sasa sina hakika ni variables gani ambazo kwa kiasi kikubwa (strongly and reliably) zinaweza kutabiri (predict) mstakabali wa ndoa!!

Na umri huu, bado niko tayari kupigwa shule!!

Babu DC!
 
Lizzy,

Hongera sana kwa kuonesha jinsi unavyoyathamini maisha yako..Ila naomba umsome Kloroquine (CQ) aliposema hivi:

"...unaweza kuwa unajadili maisha ya gerezani (a.k.a lupango) ukiwa uraiani"

Na pia akasema hivi (huyu huyu CQ),

"..Usitukane mama ntilie kama huna uwezo wa kula hotelini"

Naamini some la leo limeeleweka ingawa tamati bado kufika!

Babu (naona umetoa ruhusa rasmi) DC hiyo misemo ya Kloro siikatai na inawezekana sana ikawa na kweli ndani yake!

Wa kwanza ntapingana nao kwa kiasi kikubwa kwasababu mara nyingi sio lazima mtu binafsi aexperience kitu fulani kujua kwamba ni kizuri au la!Kitendo cha mimi kua uraiani hakuninyimi mimi uelewa wa nini kinaendelea ndani ya gereza...hakuninyimi mimi imagination na wala hakuninyimi mimi ufahamu wa kutofautisha/kuzifahamu adha za kua gerezani na raha ya kua uraiani!!!Kwa kutumia tu akili/fikra nilizojaliwa naweza kutofautisha jela na uraiani pia faida na hasara za pande zote mbili.Sadly to say...kwangu mimi gerezani hakuna faida yoyote kwangu..na kuwa upande huo wa maisha kutaniondolea furaha yangu kwa kiasi kikubwa sana!!Hivyo basi nitafanya kila niwezalo kuhakikisha siishi jela (japo naweza kuingia kwa bahati mbaya)...kwasababu tayari najua sio sehemu nnayotaka kuwepo.Yani huo ni uchaguzi wangu...na nguvu zangu nazielekeza kwenye kukataa kubadili uchaguzi wangu iwe kwa lazima au hiari!!!

Msemo wa pili umejaa ukweli mwingi!Ila kwangu sijamtukana mama ntilie popote...nilichosema tu ni kwamba SIPENDI kula kwa mama ntilie na uwezo wa kutokula kwa mama ntilie nnao hivyo sitokaa nikubali kula kwa mama ntilie!!

Its all in the mind...kam hutaki hutaki tu!!Kwahiyo ikitokea najua jinsi ya kujiengua... simnyanyasi mtu ili na mimi nisinyanyasike! Pia siamini kwamba naishi ili niwe nalia na kuugulia maumivu kila siku.
 
May be,

Stringent vetting kwenye ndoa inaweza kuwa imekaa kinadharia zaidi!! Naamini kuna watu wamefanya vetting ya nguvu na kwa gharama kubwa sana lakini wameishia kusambaratika kabla ya first anniversary!!

Hadi sasa sina hakika ni variables gani ambazo kwa kiasi kikubwa (strongly and reliably) zinaweza kutabiri (predict) mstakabali wa ndoa!!

Na umri huu, bado niko tayari kupigwa shule!!

Babu DC!
Ndugu yangu DC haijakaa kinadharia..hapa ndipo ulipo ukweli..tabia siyo fedha mtu hawezi ficha na ktk hili wengi wamelia, hivyo jamii inayomzunguka huyo mchumba ina a-z ya tabia yake na wala haihitaji gharama kufuatilia..taabu vijana wa leo hawaulizi /hawashirikishi watu wazima ktk hili..ndo tunasikia aah huyo alikuwaga shoga toka chuo nk.,tabia ndiyo kitu kinachoweza tabiri hatima ya ndoa babu dc..ndipo waswahili hunena tulijua tu au fupa lililomshinda fisi...au gume gume lililomshinda ..... angaliweza? ni misemo ya kiswazi yenye kusaza ukweliii..babu dc kuchunguza hakujapoteza maana bado..unaweza beba shipa(dume-shoga au mke mchawi) ukajuuuta kuzaliwa..
 
Kila mtu anajua nini haswa kilichomvutia/mpendeza hata kutaka/kukubali kuo/kuolewa au hata kua na mpenzi aliye nae.Hata wale ambao hawana wapenzi wana idea ya nini kinachoweza kumvutia kwa mtarajiwa wake!

Swali: je ni kitu gani kinachoweza kukufanya uachane na mke/mme/mpenzi wako?!Ni kitu gani unafikiri akifanya au kikitokea kwenye mahusiano yenu baada ya muda hutoweza kuendelea kuvumilia?!

Binafsi vitu ambavyo vinaweza kuniondolea yale mapenzi nlokua nayo mwanzo ni ....
1. Kunipiga - mwanaume kuniinulia mkono mwanamke mzima ambae kama kuna tatizo angeweza kunijulisha kwa njia nyingine na likatatulika kwa kweli siwezi kuvumilia.Maana ukichekelea leo jiandae na kesho!!

2.Kutoka nje ya mahusiano. - sijui kama itatokea siku nikabadilisha mawazo kuhusu hili ...kwa sasa hivi naamini kama mtu ananipenda na kuniheshimu kweli hawezi kutoka nje ya mahusiano tuliyonayo.Kama kuna kinachokosekana aniambie nirekebishe.

3.Kunidharau/tukana mbele za watu - inaonyesha haniheshimu...na kama haniheshimu siwezi kuona tukiendelea hata kufika mbali zaidi ya kua wapenzi tu maana kuheshimiana ni muhimu.

4. Kuonyesha kutokujali hisia/mawazo yangu - mtu ambae anamwachia mwenzake kazi nzima ya kujenga mahusiano ni sawa na mzigo mzito ambao unabebeka ila baada ya muda unachosha.Kuna watu ambao wao hata kumjulia mwenzake hali hawezi...kusongesha mahusiano mbele hawezi..yani we unakua na kazi ya kumpeleka upande huu na ule bila kujua kama kweli ndo kilichopo moyoni mwake.Kama unamlazimisha vile au anafanya tu kukuridhisha uendelee kuwepo kwa muda ule ambao anaweza kutumia uwepo wako.Ubaya wa watu kama hawa ni kwamba hata siku akiamka akakwambia sikuwahi kukupenda huwezi kumbishia kwasababu hakuwahi kukwambia wala kuonyesha kwa matendo!!

5.Ubinafsi - mtu wa mimi..mimi ..mimi.Kila kitu ni vile anavyotaka yeye au hamna kitu.Wakati mahusiano yanatakiwa yawe makubaliano na michango ya pande zote mbili.

6.Ulalamikaji/kutokua na shukrani - hata ufanye zuri gani huwezi pata asante na mbaya zaidi utaambulia malalamiko.

7.Kutokujiamini kulikopitiliza - maana mara nyingi hii hua inazaa tuhuma.Anakua hana imani kwamba unampenda kweli au ukienda sokoni unaenda kununua nyanya tu na kurudi.Tuhuma zikizidi zinaua hisia zilizokuwepo.
N.k....

Wewe je....?!

Bibi Lizzy, haya yote ni ya kusadikika....! Maana katika kila ndoa lazima baadhi ya hayo yatokee...! Cha msingi ni kufahamu yafuatayo;
  1. Mara zote mwanamke humkubali mwanaume, pamoja na mapungufu kwa matumaini kwamba huyo mwanaume atabadilika....! Lakini wanaume hawabadiliki....!
  2. Mara zote mwanaume humtokea mwanamke bila kumjua vema, na hivyo anakuwa na imani kuwa huyo mwanamke hatobadilika....! But, normally they do change....!
  3. Hakuna kosa kama kumsamehe binadamu kosa mlilokubaliana kwamba ni kosa kabla ya kosa hilo kufanyika....!
  4. Bora kuishi peke yako, kuliko kupenda bila kupendwa....!
 
Bibi Lizzy, haya yote ni ya kusadikika....! Maana katika kila ndoa lazima baadhi ya hayo yatokee...! Cha msingi ni kufahamu yafuatayo;
  1. Mara zote mwanamke humkubali mwanaume, pamoja na mapungufu kwa matumaini kwamba huyo mwanaume atabadilika....! Lakini wanaume hawabadiliki....!
  2. Mara zote mwanaume humtokea mwanamke bila kumjua vema, na hivyo anakuwa na imani kuwa huyo mwanamke hatobadilika....! But, normally they do change....!
  3. Hakuna kosa kama kumsamehe binadamu kosa mlilokubaliana kwamba ni kosa kabla ya kosa hilo kufanyika....!
  4. Bora kuishi peke yako, kuliko kupenda bila kupendwa....!
Kipenzi chao umelongaa..ila tahadhari, ni kukosea/kubahatisha kuamini tabia ya mtu itabadilika mbele ya safari (amemshindwa mamaye, iweje weye?) unless there is spiritual efforts... kusugua magoti saana..na hata wengine huishia kwa witch drs..dawa ni umakini ktk selection, ILA MUNGU NI MBELE YA YOTE.
 
Back
Top Bottom