Ni kitu gani ungependa kiwepo kwenye katiba mpya?

Lyamungo

Member
Aug 17, 2011
91
7
Toa maoni yako kwenye huu uzi kuhusu chochote ambacho ungependa kiwepo au kisiwepo kwenye katiba mpya ili tutakapokutana na Tume tutoe maoni yanayofananafanana.
 
Wazee wote kuanzia miaka 65 wasitaafu na ambao hawakuwa watumishi kwa ujumla watunzwe na serikali kama kundi maalumu

Watumishi waruhusiwe kupewa haki ya kufanya siasa mfano ktk uchaguzi na wawe huru kuendelea na kazi zao za awali endapo hawakupata kuchaguliwa ktk nafasi za kisiasa
 
Rais apunguziwe madaraka ya kuteua vyeo kibao! Viti maalumu viwe maalumu kweli mfano,walemavu,wazee,vijana,albino,wanawake baasi kila chama kitoe viti sawa!! RC,DC,Mawaziri,wakurugenzi wa idara mbalimbali/wilaya/mkoa,Makatibu wa wizara na wote wanaoteuliwa na prezda wote wawe wanaapply position hizo na qualification husika strictly degree/master/phd etc

•mbunge aweze kuadabishwa na wananchi sio lazima afikishe miaka mitano na akiondolewa mshindi wa pili ashike kiti(kuepuka gharama za uchaguzi)

•Mfanyakazi wa umma waziri,mkurugenzi,katibu na vyeo vinavyofanana na hvyo akila rusha au akiliingizia hasara taifa shurti afilisiwe na apate mvua zisizopungua 10

•Serikali isomeshe wanafunzi bureee vyuo vikuu
 
Back
Top Bottom