Ni ipi tofauti ya haya maneno?

Jefe

Member
Apr 15, 2011
7
1
HIVI NIKISEMA TUONANE HALAFU.
NA pia nikisema tuonane BAADAE.
NI IPI TOFAUTI HASA YA HAYA MANENO (HALAFU) NA (BAADAE)
 
Test of the words per above distinctio:
Alinipiga halafu akanichomea nyumba
Alinipiga baadaye akanichomea nyumba

Tofauti yeke ni ipi katika sentensi mbili hizi
 
we dogo jefe niaje... we huoni tofauti hapo..we utasemaje muonanae halafu halafu what?
ukisema tuonane halafu inabid useme baaba ya kuonana kinafuata kitendo gani mfano..tutaonana halafu utaondoka
heheeeeeeeeeee ushansoma jefe
 
Test of the words per above distinctio:
Alinipiga halafu akanichomea nyumba
Alinipiga baadaye akanichomea nyumba

Tofauti yeke ni ipi katika sentensi mbili hizi
Alinipiga alafu akanichomea nyumba....alinipiga alafu kilichofuatia akanichomea nyumba!!!
Alinipiga baadae akanichomea nyumba....alinipig alafu baada ya muda akanichomea nyumba.
Kama alivyosema Boss hapo juu ni kwamba halafu inatumika kuonyesha mfuatano wa matukio na baadae inahusiana zaidi na muda.
 
HIVI NIKISEMA TUONANE HALAFU.
NA pia nikisema tuonane BAADAE.
NI IPI TOFAUTI HASA YA HAYA MANENO (HALAFU) NA (BAADAE)

halafu mwendeleo wa tukio. Kwa mfano alikoroga mchuzi halafu akatia ndimu.
Ukisema tuonane baadae halafu ila ina maana kuna jambo ambalo mnataka kuendeleza labda kuendelea kulizungumza au kulifanya.
Baadae ni muda mfupi ujao.
 
Jefe,
Japo inaeleweka una maana gani kwa neno BAADAE ambalo unahitaji ufafanuzi pamoja na neno HALAFU, inaonekana umesahau herufi moja muhimu katika neno hilo. Ongeza herufi 'y' kabla ya herufi 'e' kila unapolitumia neno hilo ili lisomeke BAADAYE kama alivyoliandika ndugu yetu LIZZY hapo juu.
 
Jefe nafikiri ni kwanini umeona maneno hayo yanakuchanganya, ninafofikiri ni kuwa umefkiria sentensi za kiingereza na kutaka kuzitafsiri moja kwa moja kwa kiswahili, kwa uelewa wangu kwenye lugha ya kiingereza maneno yote haya ( halafu na baadaye) husimamiwa na neno "Then"!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom