Ni intelijensia ya maelekezo inaendelea ndani ya Polisi? Je polisi wanatoa ruhusa?

AmaniKatoshi

Senior Member
Mar 31, 2009
158
14
Source: Gazeti la Tanzania daima la leo, January,10, 2011 www.freemedia.co.tz

Aidha, wiki moja baada ya machafuko ya kisiasa jijini Arusha, jeshi hilo mkoani Kilimanjaro limefuta mikutano iliyoitishwa na CHADEMA kwa lengo la kuwashukuru wapigakura wao.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Moshi (OCD), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Silvin Lukaga, alisema katika barua yake ya Januari 6 mwaka huu yenye kumbu namba namba MOS/A.7/3/A/VOL.1/31 kwa Katibu wa CHADEMA Manispaa ya Moshi kuwa kwa ujumla hivi sasa hali ya kisiasa si shwari, jeshi hilo haliwezi kutoa ruhusa ya mikutano ya kisiasa kwa sasa.

“Ofisi yangu inapenda kukujulisha rasmi kwamba ombi lako la kupatiwa kibali cha kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumamosi tarehe 8/1/2011 kwenye kiwanja cha Manyema kata ya Bondeni, hakijatolewa.
“Hii ni kutokana na hali halisi ya kisiasa kutokuwa shwari kwa ujumla mpaka ofisi ya OCD itakapopata maelekezo mapya,” ilisomeka barua hiyo ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake.

My take:
1. Ni muendelezo wa maamuzi kufanyika DSM na kutekelezwa na POLICE mikoani bila kwa kuwa ndivyo wanavyopaswa kufwata amri?

2. Je, sio kwamba kazi ya polizi ni kulinda...kwani wanawanatoa vibali tangu lini?

Suggestion : Ndesamburo itisha maandamano maana ni mwiba kwa CCM. Baada ya CCM kugundua wakiitisha maandamano yeyote hayatafanikiwa maana wazee wa TANU na ASP wameshapungua kwa kiasi kikubwa na kwamba hawawezi pata support ya akina "twende na wakati au VIJANA" basi wanataka haki itafutwe mahakamani ili waamulia mahakimu na majaji namna ya kuziendesha na kuzimaliza kesi hizo!
'
Namshauri makamba arejee Morogoro kuendesha "usambaa Lodge yake pale NANE NANE. Ila kwa style ya ujenzi wake (wa kutambaa chini badala ya kujenga kwenda juu) hawezi kuijenga CCM.....

nawakilisha
 
Kuna udhaifu mkubwa wa kufikiri nakutafsiri taratibu na sheria za kazi. Kazi ya jeshi la polisi si kutoa ruhusa kwawatu kukusanyika bali kulinda Usalama wa jamii ikiwa ni pamoja na wale waliokusanyika. Mikutano ni haki ya kikatiba ya raia, taratibu za mikutano ni tofauti na ruhusa. Kama hali ya kisiasa si shwari wapo wahusika kuanzia ngazi ya mkoa, hadi taifa wanaopaswa kutolea maelezo na si Polisi ambao hawapaswi kufungamana na upande wowote wa kisiasa.
Yah: Mkutano wa Chama
Rejea barua namba JF/0/01 ya tarehe 0/0/11 kuhusu mkutano wa Chama JF Valley. Kutokana na hali isiyoridhisha ya kiusalama,Jeshi la PO.. halipo katika nafasi ya kuhakikisha usalama wa kutosha kabla, wakati na baada ya mkutano.Ningeshauri kuwa mkutano huo uahirishwe katika tarehe zilizopangwa ili kutoa nafasi ya kuliangalia suala hili kwa ushirikiano na kutafuta muafaka wa kulifanikisha kwa pamoja na kwa ufanisi.

Ahsante NG3
 
Back
Top Bottom