Ni INIESTA...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Andres Iniesta,kiungo mchezechaji wa FC Barcelona,ndiye mchezaji bora wa Ulaya kwa msimu wa 2011/2012. Amejizolea alama 18 huku Lionel Messi na Christiano Ronaldo wakijipatia alama 17 kila mmoja. Nionavyo,Iniesta anastahili. Bado mchezaji bora wa Dunia...
 
Mkuu mimi nimeona hivyo long time! Iniesta ni mchezaji anayenipa sababu za kuangalia mpira kwa sasa.anafanya uone raha ya soka na kwa miaka ya karibuni ni Zidane tu aliyekuwa akinikosha kwa mpira wa utulivu,uhakika na uliojaa kipaji cha pekee!

Iniesta ni mchezaji hatari sana kwa sasa Duniani na amecheza na viungo wote bora duniani akawafunika vibaya akiwemo Pirlo! Kwa iniesta utaona pasi za uhakika na zilizopimwa,chenga zenye mahesabu makali na akimbii hovyo na mpira kama wafukuza upepo! Miguu yake inaweza kufanya lolote na mpira na kukufanya uone raha ya soka!

Yote kwa yote ameshiriki kwa asilimia mia kuiweka hispania na barcelona ilipo leo na kama Hispania na Barcelona ndio bora duniani kwanini Hispania na Barcelona wasitoe mwanasoka bora duniani na atakuwa nani zaidi ya Iniesta?

Viva la Iniestaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kombe la Euro 2012 limemsaidia. Mimi ningekuwa na kura ningempa Hernandez mtu anayeujua mpira na ametulia
 
Kweli uefa imeamia bacelona, mchezaji gani bora hana physic,. Ukimgusa tu kanguka
 
Kweli uefa imeamia bacelona, mchezaji gani bora hana physic,. Ukimgusa tu kanguka

acha ww iniesta ana physic sana by the way physic siyo kigezo 2 cha kumuchagua mchezaji bora,iniesta ni mashine hatar!!!
 
kweli uefa imeamia bacelona, mchezaji gani bora hana physic,. Ukimgusa tu kanguka

kweli ndo mana soka letu la bongo liko nyuma, kama watu wenyewe ndio kama nyinyi, basi mpira hatuna hapa tz, na uwenda wewe ukawa na nafasi ya juu kwenye club kongwe moja hapa nchini, mana ndo akili zenu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom