Ni halali ndg Edward Lowassa kuitwa 'Waziri Mkuu mstaafu'?

Mimi naona tuangalie kwanza historia fupi ya kufukuzwa kwa Edward Lowasa na je yeye mwenyewe analikubali hilo? Kule Bungeni alipewa aina mbili za chaguo ili achague moja, yaani ajiuzuru mwenyewe au asubiri kufukuzwa Bungeni. Alipopima maji akaona akigoma kujiuzuru atafukuzwa kweli, akachagua kujiuzuru. Mara baada ya tukio la kujiuzuru Uwaziri Mkuu, mwamba huyu aliandaa mapokezi makubwa sana jimboni kwake. Kitendo cha kupokelewa kishujaa jimboni kwake kina maana kubwa moja, yaani kilichotokea Bungeni ni USHUJAA. Hivyo hakukubaliana nacho moja kwa moja. Kilichomtoa Lowassa ktk Uwaziri Mkuu ni kashfa ya Richmond, kampuni iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura nchini. Akiwa ktk mahojiano na Tido Mhando ktk TBC (aliyoyaandaa na Tido kwa nia ya kumsafisha), Lowassa alirudia kusema kuwa "hajutii maamuzi aliyoyafanya kuhusu Richmond" na hata kama angekuwa bado ktk nafasi hiyo leo, angeamua kama alivyoamua awali. Katika hotuba yake ya kujiuzuru Bungeni, Lowassa kwa ukali na hasira alisema kuwa ameonewa, na kuwa yeye kama Waziri Mkuu hakupewa nafasi ya kujitetea, na kuwa HAHUSIKI na maamuzi yaliyofanywa ya kuipa Richmond zabuni hiyo nono, hivi Waziri anapodai kuonewa atakuwa anaonewa na nani?, hivi inawezekana ukaonewa na mdogo wako nyumbani?. Huyu ndio Edward Lowassa, leo hii anajiandaa kuliongoza Taifa hili mwaka 2015.

Waandishi wetu wa habari wana mapungufu mengi sana, sitashangaa nikiambiwa kuwa Lowassa kawanunua waandishi wa habari karibu magazei yote, haiingii akilini, mtu aliyejiuzuru akapewa hadhi ya kustaafu, hata hili nalo tunahitaji kwenda darasani jamani? Kama waandishi wa habari hajanunuliwa, basi kuanzia sasa waandike ukweli wa hadhi ya Lowassa kuwa "Waziri Mkuu aliyejiuzuru?.Kwa kufanya hivyo watakuwa wanawatendea haki watanzania, ikiwa ni pamoja na "baba na mama" zao waliowazaa.
 
Nimekukubali mkuu, Huyu EL anapenda sana kutumia fedha zake kununua kila kitu mpaka watu. Hatutamkubali 2015
 
Nimepita tu mkuu.... ngoja nisubiri mwandishi atakayethubutu kumtaja kama unavyopendekeza.

Mimi napendekeza wamwite waziri mkuu wa zamani ....

Nitarudi
 
Kunradhi wakubwa, kuuliza si ujinga. Hivi hili neno "kustaafu" linapaswa litumike wakati gani? Maana kila mara naona vyombo vya habari vinamripoti Mh.Lowassa kama waziri mkuu msaafu. Sasa hapa ndipo napata kichomi kwamba Mh.Lowassa alistaafu au alijiuzulu?? Sijasikia wakisema Msuya, Warioba, Sumaye, Salim, Malecela na wengine waliopita kwamba ni wastaafu. Mara nyingi husikia wakisema waziri mkuu wa zamani fulani Bin fulani. Na hawa ni wale waliomaliza angalau term moja ya miaka 5. Kwanini basi kwa Lowassa wasiseme tu waziri mkuu aliyejiuzulu? Maana alijiuzulu huyu. Kwa hiyo basi kumbe mtu akijiuzulu kwa hiari au kwa shinikizo, ndiyo anaitwa mstaafu??
Naomba mwongozo wakuu.

ukiona chombo chochote cha habari kinamuita waziri mkuu mstaafu ujue walishavuta mkwanja.
 
Mkuu,
Dr. Salim hakumaliza miaka 5 akiwa ni premier, Msuya alitumikia u-premier kwa nyakati mbili tofauti, Malecela hakumaliza term ya miaka 5 akiwa ni premier. Ni sahihisho tu kidogo ili tubaki vema kwenye mada.
Nimekubali mkuu. Kwa hiyo sasa kumbe hakuna cheo ama sifa rasmi za wakuu hawa? Huenda waandishi wetu wa habari wako sahihi basi. Maana kama Msuya katumikia vipindi 2 tofauti aitweje? Malecela naye hakumaliza (je, kwa nini hakumaliza? au naye alijiuzulu?) na anaitwaje sasa? The same applies to Dr. Salim hakumaliza,, na nadhani anaitwa waziri mkuu wa zamani. Ikubalike kuwa na Lowassa aitwe waziri mkuu wa zamani, maana hii "kustaafu inakwaza kidoogo.
Imekaa vibaya.
 
Nimepita tu mkuu.... ngoja nisubiri mwandishi atakayethubutu kumtaja kama unavyopendekeza.

Mimi napendekeza wamwite waziri mkuu wa zamani ....

Nitarudi

Si suala la mjadala anymore kuwa huu ni mkakati wa makusudi wa EL kwa ajili ya 2015. Wanahabari wote ambao wako kwenye payroll yake wataendelea kum-address kama "waziri mkuu mstafu" regardless of what sisi humu jamvini tunachokisema!

Kwa wanahabari ambao wako sober lakini huwa wanatumia "waziri mkuu mstaafu" kimkumbomkumbo tu, kwa nini msim-address kwa cheo chake cha sasa "mbunge wa monduli" badala ya cheo marehemu ambacho kiukweli alinyang'anywa??
 
Au,, wakitaka na hiyo "waziri mkuu" iwepo, basi waseme Mbunge wa Monduli ambaye alipata/aliwahi kuwa waziri mkuu. Labda ingeleta maana zaidi kama angejiuzulu halafu akaachana kabisa na siasa, na kwamba hana cheo chochote. Lakini anacho cheo chake cha Ubunge. Ni Mheshimiwa huyu.
 
ikitokea mtu huyu amechukua urais nadhani wengine kutakuwa kuchungu wakati wote

ha ha ha haka kamtu kanafanya mapambano ya chini kwa chini na inawezekana kanataka kupunguza watu kama mwakyembe katika mchakato wa kuwepo
 
Kunradhi wakubwa, kuuliza si ujinga. Hivi hili neno "kustaafu" linapaswa litumike wakati gani? Maana kila mara naona vyombo vya habari vinamripoti Mh.Lowassa kama waziri mkuu msaafu. Sasa hapa ndipo napata kichomi kwamba Mh.Lowassa alistaafu au alijiuzulu?? Sijasikia wakisema Msuya, Warioba, Sumaye, Salim, Malecela na wengine waliopita kwamba ni wastaafu. Mara nyingi husikia wakisema waziri mkuu wa zamani fulani Bin fulani. Na hawa ni wale waliomaliza angalau term moja ya miaka 5. Kwanini basi kwa Lowassa wasiseme tu waziri mkuu aliyejiuzulu? Maana alijiuzulu huyu. Kwa hiyo basi kumbe mtu akijiuzulu kwa hiari au kwa shinikizo, ndiyo anaitwa mstaafu??
Naomba mwongozo wakuu.

Mimi nawaheshimu sana waandishi wa tz ila juzi al Adawi alivyowaambia wasimpige picha nao wakakubali, ndipo waliponivunja nguvu. nadhani huo ni muendelezo wakuu. kiswahili sanifu ni kuwa
"edward ngoyai lowasa ni waziri mkuu aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya richmond". hiyo ndio tittle yake kwishney.
 
Mbaya zaidi hata serikali yenyewe inamchukulia EL kama waziri mkuu mstaafu na ndio maana hadi leo analipwa asilimia80 ya mshahara wa waziri mkuu kila mwezi, hayo ni malipo ambayo hulipwa waziri mkuu mstaafu.
 
[B said:
Ndibalema;1736094]Mbaya zaidi hata serikali yenyewe inamchukulia EL kama waziri mkuu mstaafu na ndio maana hadi leo analipwa asilimia80 ya mshahara wa waziri mkuu kila mwezi, hayo ni malipo ambayo hulipwa waziri mkuu mstaafu[/B].

Mkuu Ndiba tunaweza kupata uhakika katika hili? Please tusaidie ili tufuatilie kumake sure nonsenses kama hizi zinaachwa mara moja. Hatuweza kutreat kujiuzulu kwa kashfa na kustaafu kama ni same thing. Wote tunajuwa HR policies za mahala pengi tu kwamba ukijiuzulu kuna benefits fulani unazipoteza hili linapaswa kuapply kwenye uwaziri mkuu pia. Maana ya 80% ni shukrani kwa mchango wa kulitumikia Taifa sasa kama mtu kaliingiza Taifa kwenye shida then tunaendelea kumreward kwa lipi? Huu ni uwendawazimu na si vinginevyo.
 
Hilo swala linajulikana na wala sio siri.
Dr.Slaa katika moja ya mikutano yake ya hadhara alishalisema sana hilo la Lowasa kuendelea kulipwa 80% mpaka leo wakati aliacha kazi.
lakini si waziri mkuu wala kiongozi yeyote wa serikali anayelitolea maelezo swala hilo.
 
Hivi Watanzania hatujui Kiswahili? Hatujui kutofautisha maana ya kustaafu na kujiuzulu? Na hawa waandishi wa habari wa Tanzania kwa nini wanatupotosha? Sijui ndio ukanjanja au shuruti za muathirika wa tukio la kujiuzulu yaani Mh. Lowassa kujaribu kurekebisha taswira yake katika jamii.
Kwa mujibu wa 7th Edition Oxford Advanced Learner's Dictionary-International Student's Edition tazama maana ya maneno haya mawili:
*Resign-to officially tell sb that you are leaving your job,an organization etc.
*Retire-to stop doing your job especially because you have reached a particular age or because you are ill/sick;to tell sb they must stop doing their job etc.
Sasa Mh. Lowassa alimuandikia barua Mh. Rais akimuelezea nia yake ya kuacha kazi ya Uwaziri Mkuu baada ya kuombwa apime uzito wa tuhuma wa kuhusika kwake kwenye kashfa ya Richmond kama ilivyodhihirika kwenye ripoti ya Bunge iliyoongozwa na Mwakyembe. Mh. Rais alimkubalia kuondoka mara moja! Haikuwa kwa sababu ya uzee wala kwa muhula kuisha! Pia, sio kwa ugonjwa bali kwa kashfa!
Now, was this a resignation or retirement? Definitely, a resignation! Hata kustaafu kwa hiari kupo i.e voluntary retirement lakini hoja hapo huwa ni umri pia. Lakini kwake si kwa namna hiyo! Sasa kwa nini Mh. Lowassa anaitwa Waziri Mkuu Mstaafu? Ni kwa nini na kwa maslahi ya nani?
Hivyo basi, tujifunze kwamba viongozi wanaotoka madarakani huwa viongozi wa zamani. Mfano, Rais aliyetoka madarakani wa Marekani huitwa former US president na sio retired US president! Utasikia former British PM na sio Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza! Bila shaka aweza kuwa retired kwa maana halisi ya neno hilo lakini haileti maana yoyote kila mara kurejea namna alivyotoka madarakani. Mbona hatuwaiti Rais aliyekufa wa Marekani? Rais aliye hai Congo
DRC n.k. Rais aliyepinduliwa wa Madagascar au Rais aliyeoondolewa kwa maandamano ya umma wa Tunisia n.k. Lazima tutambue bila kujali walitoka kwa staili gani, wapo hai au wamekufa wote watabakia kuwa viongozi wa zamani tu! Tuache mbwembwe za kuwapamba viongozi waliopita nchini bila sababu za msingi.
Matumizi ya majina ya fulani mstaafu si mageni yapo kwenye Utumishi Jeshini,Vyuo Vikuu,Mahakama Kuu na Rufaa na kwa baadhi ya kazi nyingine. Hata hivyo, kwenye Majeshi kama ilivyo kwa taasisi nyingine nilizotaja kuna mipaka. Ni kuanzia senior officers i.e Captain to General. Ndio maana hakuna Leutenant(rtd) Kibakuli au Retired Corporal Chuma n.k. japo kwa Bongo wapo akina Luteni Mstaafu Makamba n.k. Hizi ni mbwembwe tupu hapa kwetu! Watu wanapenda sifa sana! Kuna Captain(rtd) Mkuchika,Gen(rtd) Mboma n.k. Na huko mahakamani kuna majaji wastaafu pia. Kwa mfano judge(rtd) Katiti (RIP) n.k. sio Hakimu Mstaafu wa Mahakama ya Mwanzo Temeke Shabani! Naomba nitaje wachache tu.
Naomba nieleweke kwamba kwenye mazungumzo ya kawaida inawezekana kumuita Mstaafu mtu huyo bila tatizo. Ila kwenye mazungumzo rasmi inakuwa kichekesho!
Je, ni bahati mbaya kwa Mh. Lowassa kuitwa hivi au ndio ubabe na nguvu ya CCM ya kutaka kumsafisha? Make wakitaka kukuita Daktari au Profesa watakubatiza tu na Wananchi watafuata. Kumbuka wakina Dr. Luta Nelson wa Kibaha ambaye alikuwa ni lab technologist! Hata Cisco Mtiro alipewa digrii na CCM bila kumaliza chuo UDSM wakati wa kugombea Ubunge wa jimbo la Temeke 1995! Yote yanawezekana katika nchi yetu!
 
Naomba kupewa maelezo kuhusu swali hilo, maana ninavyojua mimi Lowasa alijiuzuru, hakuwahi kustaafu kama ilivyo kwa Sumaye. Imekuwa kawaida kwa waandishi wa habari kupitia magazeti, redio na television kumtambulisha Lowasa kuwa waziri mkuu mstaafu. Inawezekana mimi sielewi kiswahili vizuri, naomba kueleweshwa tafadhari.
 
Mimi mwenyewe nashangaa wanamwita waziri mkuu mstaafu,nadhani tungejibiwa na wataalamu,kustaafu ni nini na kujiuzuru maana yake nini,nimesikia juzi alipoenda Loliondo walidai waziri mkuu mstaafu, tujibuni jamani
 
Mimi itapendeza sana tukimuita na kumtambulisha hivi: Waziri Mkuu aliyejiuzuru tena atakuwa pake yake, kuliko hivi sasa kuna, Waziri wakuu akina: Warioba, Malecela, Msuya, Sumaye, Sokoine, Nyerere, Kawawa, salim, Mizengo.
 
Back
Top Bottom