Ni halali ndg Edward Lowassa kuitwa 'Waziri Mkuu mstaafu'?

Hii ilishajadiliwa sana na kufikiwa muafaka. Kama ulikosa ni kuwa Lowasa ni Waziri mkuu aliyejiuzulu. Waandishi wanaoandika mstaafu ni wale walioshindwa kutofautisha hayo mawili. Tuna kumbukumbu za uhakika kuhusu hili. Wewe hata ukimwita Waziri mkuu aliyejiuzulu hakuna hatua zozote za kisheria dhidi yako, infact ukimwita mstaafu unamdhalilisha kwasababu bado anahamu ya kurejea.
 
Ni waziri mkuu aliyefukuzwa. Huyu hakustaafu wala hakujiuzulu. Alifukuzwa kutokana na kashfa ya rushwa. Tusimung'unye maneno hapa.
 
Ni waziri mkuu aliyefukuzwa. Huyu hakustaafu wala hakujiuzulu. Alifukuzwa kutokana na kashfa ya rushwa. Tusimung'unye maneno hapa.

kiswahili fasaha ni waziri mkuu wa zamani period,mambo ya mstaafu ,sijui aliyejiuzuru ni kupoteza nguvu na muda,mbona sokoine haitwi waziri mkuu aliyekufa?
 
Kwani katiba haisemiiiiiii????? Maana mwingine atakaa siku 2 atajiuzulu naye ataitwa mstaaafu kweli?
 
Napendekeza CDM wapeleke hoja bungeni ili EL avuliwe title ya
ya Waziri Mkuu mstaafu.licha ya kuharibu maana ya neno mstaafu kwani yeye
yeye hakustaafu pia ni kumwongezea mapesa juu ya yale aliyopata
Richmond na kupelekea kutimliwa.
Kumwita yeye ni mstaafu,anawekwa kundi moja na our heroes like
Nyerere na Kawawa au waungwana kama Salim,Warioba,Msuya,Sumaye na
Malecela.
Hastahili kujinasibu kuwa na hadhi sawa na watu hawa vipi awe na title sawa na wao?
 
Napendekeza CDM wapeleke hoja bungeni ili EL avuliwe title ya ya Waziri Mkuu mstaafu.licha ya kuharibu maana ya neno mstaafu kwani yeye yeye hakustaafu pia ni kumwongezea mapesa juu ya yale aliyopata Richmond na kupelekea kutimliwa. Kumwita yeye ni mstaafu,anawekwa kundi moja na our heroes like Nyerere na Kawawa au waungwana kama Salim,Warioba,Msuya,Sumaye na Malecela. Hastahili kujinasibu kuwa na hadhi sawa na watu hawa vipi awe na title sawa na wao?
Kwa hicho cheo kapewa na nani
 
Kunradhi wakubwa, kuuliza si ujinga. Hivi hili neno "kustaafu" linapaswa litumike wakati gani? Maana kila mara naona vyombo vya habari vinamripoti Mh.Lowassa kama waziri mkuu msaafu. Sasa hapa ndipo napata kichomi kwamba Mh.Lowassa alistaafu au alijiuzulu?? Sijasikia wakisema Msuya, Warioba, Sumaye, Salim, Malecela na wengine waliopita kwamba ni wastaafu. Mara nyingi husikia wakisema waziri mkuu wa zamani fulani Bin fulani. Na hawa ni wale waliomaliza angalau term moja ya miaka 5. Kwanini basi kwa Lowassa wasiseme tu waziri mkuu aliyejiuzulu? Maana alijiuzulu huyu. Kwa hiyo basi kumbe mtu akijiuzulu kwa hiari au kwa shinikizo, ndiyo anaitwa mstaafu??
Naomba mwongozo wakuu.
 
Mkuu, hata mimi nimesikia vyombo karibu vyote vya habari vikimuita Lowassa "mstaafu". Ukisoma gazeti la Mwananchi leo utaona ujumbe wa Kardinali Pengo kuwa ufisadi unanunua habari ili kuficha ubaya wao. Inaelekea wahariri wote wamenunuliwa AU wametiswa wasimu-address Lowassa kwa cheo chake hasa "Waziri Mkuu aliyefukuzwa kazi" au aliyejiuzulu.
 
Hawa waandishi pamoja na wahariri wao hawajui lugha ya kiswahili, au wamenunuliwa!!
 
Sisi tunajua kuwa tulimfukuza kazi....wacha wawanunue waandishi lakini hawata tununua sisi waajiri wao
 
Hawa waandishi pamoja na wahariri wao hawajui lugha ya kiswahili, au wamenunuliwa!!
Mkuu, miye nilidhani sifa mojawapo ya uandishi wa habari ni kujua lugha kwa kina?? Sasa kama mtu anakurupuka tu na kuandika pasina kuelewa maana ya neno analotumia,,huyu si mwandishi makini. Mimi naamini hata Mh.Lowassa mwenyewe huwa anakereheka anaposikia wakim address waziri mkuu mstaafu,, yaani ni kama wanamchora vile. Na kama kwaeli hajisikii kukerwa na hilo,,, basi LEAVE ME ALONE!
 
I will certainly LEAVE YOU ALONE
 
Wandugu, nimeyashangaa sana yanayoendelea hapa Tanzania. Kwa ufahamu wangu vyeo vya kisiasa havina kustaafu. Hivyo mtu anayeshika madaraka ya kisiasa na kuondoka kwenye nafasi hiyo kwa sababu yeyote haitwi Mstaafu bali Aliyekua...(Direct translations from Retired and Former respectively). Kichekesho ni pale unaposikia Mbunge Mstaafu, waziri mstaafu, Diwani mstaafu n.k. Huu ni upotoshaji wenye lengo la kumfurahisha 'Bwana Mkubwa'. Hivi ni nani anayesimamia utumiaji sahihi wa 'TITLES'? Hali hii ya upotoshaji haikubaliki.
 
Sifa/cheo/wadhifa anayoistahili Lowassa hivi sasa ni WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU KUTOKANA NA KASHFA YA RICHMOND. PERIOD
 
Sifa/cheo/wadhifa anayoistahili Lowassa hivi sasa ni WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU KUTOKANA NA KASHFA YA RICHMOND. PERIOD
Ndiyo,, ni vizuri tuwe makini maana leo tupo kesho hatupo. Vizazi vijavyo vipate historia iliyo sahihi,, ndiyo maana tunasoma History ili kujua yaliyotokea zama za kale. Tusipotoshe mambo hapa. Je, Mzee Mwinyi alipojiuzulu kwa kashfa,, naye alistaafu nafasi hiyo?? Kama ndivyo,, basi Karamagi,Msabaha nao ni mawaaziri wastaafu? Watoto wetu ni vyema wakapata historia ya ukweli, kama alijiuzulu,, isomeke hivyo, na watoto waelezwe alijiuzulu kwa sababu gani kama tunavyosoma kwamba Mwinyi alijiuzulu maana wengine tulikuwa bado. Tusipindishe ukweli na historia
 
Kunradhi wakubwa, kuuliza si ujinga. Hivi hili neno "kustaafu" linapaswa litumike wakati gani? Maana kila mara naona vyombo vya habari vinamripoti Mh.Lowassa kama waziri mkuu msaafu. Sasa hapa ndipo napata kichomi kwamba Mh.Lowassa alistaafu au alijiuzulu?? Sijasikia wakisema Msuya, Warioba, Sumaye, Salim, Malecela na wengine waliopita kwamba ni wastaafu. Mara nyingi husikia wakisema waziri mkuu wa zamani fulani Bin fulani. Na hawa ni wale waliomaliza angalau term moja ya miaka 5. Kwanini basi kwa Lowassa wasiseme tu waziri mkuu aliyejiuzulu? Maana alijiuzulu huyu. Kwa hiyo basi kumbe mtu akijiuzulu kwa hiari au kwa shinikizo, ndiyo anaitwa mstaafu??
Naomba mwongozo wakuu.

Mkuu,
Dr. Salim hakumaliza miaka 5 akiwa ni premier, Msuya alitumikia u-premier kwa nyakati mbili tofauti, Malecela hakumaliza term ya miaka 5 akiwa ni premier. Ni sahihisho tu kidogo ili tubaki vema kwenye mada.
 
Back
Top Bottom