JK amejiruhusu kuwa rais rojorojo, ambae amezungukwa na watu dhaifu ambao hawamsaidii, hata kuliona hilo na lenyewe ni jambo lakuhitaji ushauri wa Bana.
kweli tutaona mengi mpaka huyu Mkwere atakapoondoka Ikulu.
Rais kikwete si Rais wa kwanza kufanya vikao vya chama Ikulu hata waliomtangulia walifanya hivyo lakini pia Katiba yetu inaruhusu kufanya vikao Ikulu kwa maana ya kisheria kwamba katiba iko kimya kwa jambo hilo au haijasema lolote....si kosa. Hata hivyo, Rais kufanya kikao Ikulu na chama kinachotawala sio jambo geni katika siasa za dunia, hata pale chama kingine kikishika dola ni ruksa kufanya vikao vyake Ikulu na CCM haitakuwa na ruksa hiyo kama hakitakuwa chama tawala. Ni vigumu sana wakati mwingine kutenganisha kofia ya urais na shughuli za chama hii ni kwa sababu serikali iliyoko madarakani inatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama kinachotawala. Tukumbuke kuwa moja ya agenda za mikutano ya chama ni pamoja na kujadili utekelezaji wa shughuli za serikali kama ilivyoagizwa na chama.
Hata hivyo, bado suala hili linazungumzika endapo sheria itaamua vinginevyo. Maoni ya watanzania kuhusu suala hili ni muhimu lakini bila sheria si vema kulaumu.
Na Lowasa ambaye ni visadi papa yumo? maweeeeeeeeeNa hapa ni katika ukumbi wao wenyewe...see the difference