Ni halali Bastola ya katibu mkuu wa CDM kuonyeshwa hadharani na polisi?

Marehemu DITO alikutwa na risasi ya AK 47 airport ikithibitisha kuwa anamiliki bunduki aina ya AK 47 baada ya kujitetea kuwa mke wake alisahau kuitoa kwenye suitcase. Itakuwaje mtu ushangae pistol na sio AK 47 bunduki za kivita na mtu baki anamiliki?

Huu ni upofu ndani ya miaka 50 ya uhuru.
Kenge, ni kweli watu wanaruhusiwa kumiliki silaha, bunduki na bastola za aina zozote isipokuwa pistor za Colt .38 ni kwa matumizi ya Tiss tuu na AK 47 haziruhusiwi kutumika kisheria, hutumiwa na comandoo na marcernaries katika covert operations ambazo sio za kisheria bali za kijasusi!.

Kama ni kweli Ditto alikutwa na AK 47 then ni kosa kisheria na alipaswa kushitakiwa no matter ameipataje hata kama ni kihalali matumizi yake ni illegal.
 
nawapeni pole wana chadema wote juu ya suala hili la arusha mimi naomba kwa Mungu wetu atawasaidia ukombozi utapatikana
 
Hata mimi nilishangaa na kuogopa sana pale niliposikia maelezo ya afande kuwa wamekamata Dr Slaa akiwa na bastola, halafu wanaishia hapo. Hawatuambii kama ilitumika ndivyo sivyo au haimikiwi kihalali. Binafsi niliona kuwa lilikuwa ni kosa la kiufundi lililofanywa na polisi yule.

kuna nyakati huwa naona mateja wana akili kuliko hao POLISIjui.
Hawajatengeneza mazingira ya kupendwa na wananchi bali ya kuzidi kuchukiwa.

CHADEMA Arusha hili likitulia itisheni kura ya maoni kuwataja Polisi wanaohusika na ujambazi. Kulinda misafara na kusafirisha milungi na bangi, na kuuza dawa za kulevya.
 
Unajua muda mwingine sifa za kijinga zinadhoofisha utendaji kazi kiweledi,
Hakupaswa kuitangaza hiyo silaha hata, atakuwa amepewa shinikizo au ni kutaka kumharibia mtu hapa

Kuhusu AK 47, hii ni silaha ya kivita ambayo risasi zake ni zile ambazo zinatumika kwenye SMG, ambayo ni ndugu moja
 
Tunavyo elezwa kuwa Tanzania kuna amani. Sasa kwanini watu watembee na bastola viunoni?
 
Hao makamanda wa polisi wanaotumika kisiasa wajue siku si nyingi toka sasa hao askari wa chini wanaowatuma kufikia malengo ya kishetani ya CCM watawageuzia hizo silaha wanazoringia ambazo zimenunuliwa kwa kodi zetu kutulinda na kamwe si kwa ajili ya kudhalilisha viongozi wetu.ILAANIWE CCM, LILAANIWE JESHI LA POLISI,ILAANIWE TISS.
 
Tunavyo elezwa kuwa Tanzania kuna amani. Sasa kwanini watu watembee na bastola viunoni?

Labda huko kwenu Zanzibar ndiyo kuna amani, sisi huku Tanganyika amani hakuna kabisa.Kwani yule gaidi wa kisomali alivyopanda jukwaani na silaha kule Igunga hukumuona ?
 
Marehemu DITO alikutwa na risasi ya AK 47 airport ikithibitisha kuwa anamiliki bunduki aina ya AK 47 baada ya kujitetea kuwa mke wake alisahau kuitoa kwenye suitcase. Itakuwaje mtu ushangae pistol na sio AK 47 bunduki za kivita na mtu baki anamiliki?

Huu ni upofu ndani ya miaka 50 ya uhuru.

fafanua vizuri great thinker ina maana kuna sheria inaruhusu raia wa tanzania kumiliki silaha ya kivita kama ak 47,sub machine gun.hebu nielewesheni kabla wengine hawajajimilikisha mabomu na vifaru.
 
Nakuunga mkono Dr slaa inabidi amfungulie kesi yule askari aliionyesha silaha yake adharani kwani hata kama kulikua na adui anamnyemelea ashamuweka wazi adui ajipange tena
 
Nasikia ile bastola ina rekodi ya kutumika kwenye matukio ya ujambazi!
 
whatever they do, its useless bila kutatua kero za watanzania, haitasaidia sababu umaa wa watanzania unajua kila kitu, walianza na mambo ya kumkejeli kapora mke wa mtu, wakaja na ile yeye ni padri, wananchi bado hawakuwajali chochote, Baadaye wakaingia na gia ya uchagga wa CDM ikakwama, Wakatoka na UDINI kwamba CDM ni ya WAKRISTO - Kuona hivyo wazee waasisi wa CCM wamekemea, Sasa wana single mpya kabisa ya kuhakikisha kila mbunge, kila mwanaharakati wa CDM anafunguliwa kesi lukuki, sasa sijui kama hii singel yako itauzika sokoni, wanasaidiana na police kui- promote.
 
Hivi kwani kutembea na bastola Tanzania ni kosa? Kama ni kosa, nanai wanastahiki, nani hawastahiki kutembea na silaha? Nakumbuka Rage alipanda nayo jukwaani, wala haikuwa nongwa, au kama ni kunya anye bata tu, kuku akinya anaharibu mazingira?
 
Tunavyo elezwa kuwa Tanzania kuna amani. Sasa kwanini watu watembee na bastola viunoni?

Mh. Barubaru amani ya nchi haizuii haki ya kujilinda pia unataka kutuambia hakuna matukio ya ujambazi ama mauaji nchi? Swala la umilikaj wa siraha ni privacy ya mtu ni linapaswa kuheshimiwa sana kwa misingi hiyo ndo maana kila anayetaka kumiliki siraha basi anafuata taratibu za kisheria japo kuna baadhi ya nyadhifa basi ukishakuwa nazo basi unauharari wa kumiliki siraha kwa ulinzi wako japo bado linafanywa kuwa siri ili kuendelea kuwalinda wamilikiji wa vyombo hivyo.
 
Back
Top Bottom