Ni halali Bastola ya katibu mkuu wa CDM kuonyeshwa hadharani na polisi?

Kibori

Member
Jul 21, 2009
72
10
Ndugu zangu mimi nadhani nchi pasipo usawa kwa wote sio nzuri hata kidogo, imani ni kitu kizuri na sio cha kuchezea hata kidogo na Tanzania tujivunie sana amani ambayo misingi yake imejengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Amani ni kitu cha misingi sana lakini lazima tuelewa mambo yafuatayo.


Mwalimu alijaribu kulinda na kuieenz kwa nguvu zote haki za raia wote bila kuonyesha matabaka ya haki za maskini na tajiri. Alijiitahidi sana lazima niseme. Ndio maana amani ikadumu vya kutosha lakini serikali zingine zilizofuata kwa kweli ni maoni yangu kuwa ndio chazo cha vurugu tunazoziona kila wakati na kila kunakucha. CDM wakati mwingi sana wanaonewa watu wakiandamana kudai haki kwanini dola itumike bila busara kwa njii hii Amani anavuruga nani kama sio serikali, CCM kupitia kwa Jeshi La Polisi. Keshi za kila siku kwa wabunge wa CDM kwanini ? Ni dhambi kuwa Mbunge wa chama pinzani ? Nadhani mpaka mwaka 2015 wabunge wote wa CDM kama hawajafungwa wote na wafuasi wao basi kila Mbunge wa CDM na wafuasi wao watafunguliwa kesi hata 1000 kwa hili ya sasa inavyokwenda.

Mimi binafsi kuonyeshwa kwa Bastola ya Dr. Silaa hadharani na polisi tena kwa kusema tumewakamata watuhumiwa na wamekutwa na Bastola na kuwataja majina kama walivyotaja jina la Dr. Silaa ni dharau na kuvunja haki ya msingi ya kujilinda ya Dr. Silaa. Mtu hununua Bastola kwa kujilinda lakini kama adui wako atajua wewe una Bastola basi maisha ya huyu mtu (Dr. Silaa) yatakuwa hatarini zaidi. Haina tena maana kama kila mtu anajua unabastola kama walivyofanya polisi jana kwa Dr. Silaa. Au ni kujibu mashambulizi ya Aden Rage aliyeonyeshwa na Magazeti akiwa jukwaani akiwa na Bastola ? Hili pia sio zuri lakini hili la Rage ni Uzembe wake hakuna aliyemlazimisha kutoificha bastola yake.

Ushauri wangu kwa Dr. Silaa, amfungulie kesi ya jina na madai yule polisi aliyeonyesha hiyo Bastola kwani baadhi yetu sisi jana tulishutushwa na tangazo lilie kwani kwa masikio ya wengi kama mimi ni either Dr. Silaa haimiliki Bastola kwa halali ( Jambazi) au amedhalilishwa tu. Polisi wana haki gani kisheria kutangaza vifaa wanavyoyakuta mikononi mwa mtuhumiwa kama issue sio ya ujambazi ?? This is double standards ni kwa njia hii Amani sidhani na naogopa sana kama itadumu kwa muda mrefu. Polisi na serikali acheni kutuvurugia Amani yetu.

Ndugu zangu Umma maana yake ni POWER. Serikali, Polisi na mtu yeyote lazima kuheshimu kwa nguvu zote umma, madaraka na kila kitu including kazi za polisi ni UMMA. If police whose roles are primarly to protect the walfare, peace and security and create harmony on behalf of all citizens begins to contradict these roles and responsibilities, peace and security will be gone, they legitimacy and respect for police and goverment when it reaches this stage comes to an end and that is NO peace and security anymore. This is impunity we must stand as PUBLIC to say NO.

I stand to be corrected.

United we stand !

Kibori
 
Kamuulize Aden Rage wa A-lshababaab atakueleza umuhimu wa viongozi wa Tanzania kutembea na Bastola.Sheria mnazitunga wenyewe zinawaumiza wenyewe.Patamu hapo nani amfunge mwenzake kengere.Watanzania mtachinjana sana hata Rwanda walianza kiutani utani hadi ngoma ilipokolea ndiyo wakangundua walipaswa kukaa meza moja.
 
Hata mimi nilishangaa na kuogopa sana pale niliposikia maelezo ya afande kuwa wamekamata Dr Slaa akiwa na bastola, halafu wanaishia hapo. Hawatuambii kama ilitumika ndivyo sivyo au haimikiwi kihalali. Binafsi niliona kuwa lilikuwa ni kosa la kiufundi lililofanywa na polisi yule.
 
Polisi wamechoka kulinda wanataka litibuke ili wajivue lawama kwamba wamezidiwa na nguvu ya umma
 
Ni kweli kumtangaza kuwa alikuwa na bastola, ni kumvunjia privacy yake. lakini pia inaweza kufanywa hivyo kisiasa ionekane siyo mtu mzuri kitu ambacho si kweli. kuna watu wanamiliki bastola na mashort gun kibao, lakini huwa ni siri zao, na huzihifadhi si kila mtu ajue ana siraha.

Aden Rage hakuonesha ustaraabu hata kidogo kupanda jukwaani na bunduki, Slaa anatembea nayo lakini hakuna aliyewahi kuiona.

Kila mwaka, maombi kibao yanapelekwa kwa DCP kanumba, ili atoe vibali vya kumiliki siraha, michakato hii huanzia serikali za mitaa kwa mwenyekiyti wa serikali za mitaaa
 
Hata mimi nilishangazwa sana kwa kumsikia yule "Mbwa" akitambulisha silaha walizokutwa nazo Watuhumiwa ambazo wanazimiliki kihalali.

Kisheria, Ukiwa unamiliki Silaha unatakiwa uwe nayo hata kama unakwenda kuoga. Vinginevyo utakuwa umevunja sheria ya Umiliki wa Silaha.

Kitu kisichotakiwa ni Kuitoa hadharani au Kuitumia kutishia Watu.

Swali nililojiuliza, kama lengo lilikuwa ni kuelezea vitu walivyokutwa navyo/ Walivyovisalimisha Watuhumiwa Polisi, mbona hawakueleza na pesa walizokutwa nazo ambazo tunajua mara nyingi ukishazikabidhi Polisi ni vigumu kurudi kwa Mtuhumiwa kama alivyoziwakilisha!
 
Kamuulize Aden Rage wa A-lshababaab atakueleza umuhimu wa viongozi wa Tanzania kutembea na Bastola.Sheria mnazitunga wenyewe zinawaumiza wenyewe.Patamu hapo nani amfunge mwenzake kengere.Watanzania mtachinjana sana hata Rwanda walianza kiutani utani hadi ngoma ilipokolea ndiyo wakangundua walipaswa kukaa meza moja.

Mzee, sihitaji kwenda kwa Aden Rage kujua umuhimu wa kuwa na Bastola sio kwa viongozi tu, nichopinga ni double standards treament wanazopata wabunge wa CDM na wafuaasi wao sio ndivyo. Wao wakiandamana ambayo ni haki ya kikatiba basi wanawekwa ndani lakini CCM hapana. Hii sio, vyombo vya dola pia vinatumia vibaya wakati mwingine, kwa maoni yangu...sasa nani atalinda haki za raia tena ? UMMA stand up and SAY NO TO IMPUNITY ! This is the message I bringing on-board. !!

"Watanzania mtachinjana sana hata Rwanda walianza kiutani utani hadi ngoma ilipokolea ndiyo wakangundua walipaswa kukaa meza moja"[/QUOTE]

Mwenzetu wewe sio Mtanzania nini ?
 
Marehemu DITO alikutwa na risasi ya AK 47 airport ikithibitisha kuwa anamiliki bunduki aina ya AK 47 baada ya kujitetea kuwa mke wake alisahau kuitoa kwenye suitcase. Itakuwaje mtu ushangae pistol na sio AK 47 bunduki za kivita na mtu baki anamiliki?

Huu ni upofu ndani ya miaka 50 ya uhuru.
 
Tunasikitika kwa kuwa na Jeshi la Polisi linaloendeshwa kijinga pengine kuliko lingine lolote Africa nzima.
 
Jinsi walivyo makameruni na masaburi eti wanajiona washindi tayari. Let them know that cdm kuanzia juu hadi wanachama wa kawaida wako very strategic. Bahati mbaya CCM Arusha inebaki na wazee wawili watatu wa kiswahili hapo mtaa wa binddeni tu .The rest ni CDM .Sasa walichoshinda hiyo Mikameruni ni nini. Halafu wanapamabana na PANYA loh.
 
kwa kweli Slaa anawaumiza vichwa...

kwa kweli si halali kutangaza kuwa fulani anamiliki bastola....kwani unamuweka kwenye mazingira ya hatari zaidi pale anapovamiwa.....

pia, sheria ya umiliki wa bunduki inamtaka mwenye nayo aibebe na awe nayo kila aendapo.... hata kama ameshuka kunywa bar, hatakiwi kuiacha ndani ya gari......

wao walitaka aiache wapi?

polisi wa Arusha ni WAHAINI....wafunguliwe mashtaka....
 
Hawajilipwa mishahara ya miezi miwili, karibu watalipuka tu nyie poeni!
 
Polisi alitaka apandishwe Cheo nini..kasahau kazi yake..Acha tuone Mwema kama ni mwema au gamba pevu
 
Hawa polisi wamezidi kuwa mechanical, hivi hata kama umetumwa wewe nawe si ni proffessional, goma likigeuka ukipelekwa kulima viazi kwenu utamlaumu nani? kama kweli wewe ni mtaalam wa jeshi la polisi kumbuka hawa politicians wanaexist kwa mda mfupi sana, nini cha kukusumbua? au ndo unataka upewe cheo? hujui a time will reach kwa wenye sifa tu ndo wapate vyeo? Ni udhalilishaji wa hali ya juu. WATANZANIA TUAMKE TUUPINGE HUU UONEVU KWA NGUVU ZETU, TUKIKAA KIMYA LEO KESHO TUSILALAMIKE WATU WAKIANZA KUPIGANA MASHOKA. hAIWEZEKANI WAJINGA WACHACHE WATUHARIBIE NCHI YETU MCHANA KWEUPEEE KWA MASLAHI FINYU YA KISIASA. HIVI HAWA VIONGOZI HAWAONI? KINACHOENDELEA ARUSHA NI INDICATOR KWAMBA WATU SASA WAMECHOOOOKA.
 
unatangaza umemkamata mtu na bastola then husemi ka anaimiliki kihalali au la huko ni kufikiri ki masaburi didasi (******)
 
Shame on you Slaa...unatembea na bastola ya kazi gani? huna walinzi?
Kweli avatar za watu zina wafanana yule al shabab wa magamba alikuwa nakisu igunga tena kwenye mkutano wa kampeni??shame on you too!!!
 
Polisi wameshindwa kazi na wanachofanya ni kutafuta afadhali kwa kufanya vitu ambavyo hata mjinga hawezi kuamini
 
Back
Top Bottom