Ni haki kwa binti kumtia adabu mama wa bf wake?

Kwa hiyo huyo binti ana haki ya kumpiga mama wa bf wake?

Sishabikii kitendo alichofanya huyo binti kwa sababu sio kizuri. Lakini, just fikiria kama ni wewe umeamka asubuhi unahesabu hatua zako moja mbili tatu, busy tu na jazba zako unaenda kumnyeshea mvua ya matusi binti wa watu unategemea nini??
 
Yani kama mimi ndo angenipiga, haki ya Mungu huyo binti asahau ndoa......katu asingeolewa na mwanangu,ningeitisha vikao hadi vya ngazi ya taifa kuhakikisha huyo binti haingii kwenye mji wangu. Hata kama nina madhaifu hapaswi kunipiga......

hapo amekuwa mbuzi wa kafara
 
wengine hufikiria kwa kutumia masaburi .... huyu dada hakuwa anaelewa anachofanya angeelewa kwamba anajifungia milango ya riziki asingekuwa na uthubutu

Thats why I said she is so careless, alijiangalia tu for that time ana uwezo wa kufanya nini ila hakuangalia anafanya kwa nani na kwa effects zipi zitakazompata. Katibu ugonjwa mmoja kwa kuibua maradhi mia moja!
 
Wote wana makosa kwanza huyo mama kuwa na hako katabia kachafu,pia binti kumtembelezea mama huyo kichapo kwani kuna njia nyingine nyingi angetumia tofauti ya kumtembezea kichapo.
 
Thats why I said she is so careless, alijiangalia tu for that time ana uwezo wa kufanya nini ila hakuangalia anafanya kwa nani na kwa effects zipi zitakazompata. Katibu ugonjwa mmoja kwa kuibua maradhi mia moja!

nadhani hata hayo mahusiano yake na huyo kijana hayatadumu au kuchukua muda mrefu kwani hayana baraka
 
Mama mtu mzima kudamka kwake, kitanda na usingizi anaacha kwenda kuangalia nani kalala na mwanae ? Hiyo sio laana?

Japo sishabikii kupigwa lakini acha achapwe ashike adabu, anamuingilia kijana wake mpaka kwenye sita kwa sita zake ?

Na ndoa itakuwepo tu jamaa kama angetaka kumsevu mama angetoka nje,

We mzazi wako wa kike kila siku asubuhi akijua umelala na msichana anakuja kuzua zogo maana yake ni nini kama si ukosefu wa adabu uliopitiliza
 
hivi mamaako akikosa ndo unaruhusa ya kumpiga Kweli?

Huyo mwanaume nimemtoa thamani na girlfriend wake! No wonder hata mama yake kakosewa adabu mbele yake na ndo maana pia hata huyo mamaake anamfanyia huo upuuzi.
 
kama mama yake akikosa anamhukumu hivyo je siku huyo mcharuko wake ukikosa atafanyaje???
 
binti ana laana huyo...kalaanika hata na barabara anayopita juu yake!
 
kama mama yake akikosa anamhukumu hivyo je siku huyo mcharuko wake ukikosa atafanyaje???
Ndo hapo sasa!! Kwa kweli hapo wote watatu wamekutana.

Mama mtu mzima hovyo, kijana mpuuzi na binti ndo mcharuko. Hivi angempuuza tu na kumwita mwanae aje ajibu hayo maswali ingekuwaje?
Kujivika cheo cha kurekebisha tabia za mama wa mwenzio hata bado hujasoma ramani.
 
Huyo msichana na huyo mwanaume watakuwa akili zao haziko sawa. Lazima wanavuta bangi au madawa ya kulevya. Kumpiga mtu mzima si kitu cha kawaida kwa mtu mwenye akili timamu; leave aside mtu mzima huyo ni mama mzaa chema.

Yani afu anategemea kabisa kuwa wife??? Kwa ndoa ya sherehe au kubebana??? Maana I can't imagine siku ya harusi kama mama mkwe anaweza kuhudhuria. Kwa kweli hiyo couple imenitia hasira sana. Kijana asubiri laana tu.
 
Huyo mama hana watoto wengine eeh. Maana am trying to imagine kibinti kimpige hata kibao mama yetu no matter amefanya nini atajua kuwa maharage si mbonga.
 
Mwenye kosa hapo juu ni jamaa kuruhusu mama yake kudhalilishwa.
 
Huyo mama hana watoto wengine eeh. Maana am trying to imagine kibinti kimpige hata kibao mama yetu no matter amefanya nini atajua kuwa maharage si mbonga.

Mama hana watoto wengine huyo ndio mtoto pekee,na ndie aliemruhusu gf wake amsaidie kumrekibisha mama yake,unafikiri acngetoa ruhusa binti angempiga huyo bi mkubwa? na nafac ya bi mkubwa kama mzazi unaichukuliaje?
 
Wote hawafai. Kijana hafai kuwa mume, binti hafai kuwa mke na mama naye hafai kuwa Mama sio mstaarabu. wote ni washenzi.
 
Back
Top Bottom