Ni haki housegirl kufua nguo za ndani za mabosi wake yaani mtu na mumewe??

katika hali ambayo me nimeiona ni ngeni machoni pangu nimeshuhudia housegirl akifua chupi za mabosi zake. Tena c mara moja ni zaidi ya miezi sita sasa.<br />
Jamani labda me ni mshamba kushangaa ishu hiyo naombeni mnijuze jamvini ni sahihi suala hilo?
<br />
<br />

hao ni wachafu hasa huyo mama. Lazima hata kitanda anatandikiwa na choo cha master anasafishiwa. Wanataka kumuambukiza binti wa watu maradhi ya fangasi!
 
Sio sawa tena ni unyanyasaji kabisa. Lakini tujiulize swali moja la msingi ktk hili, mwanaume/mwanamke unavaa nguo ya ndani halafu unaitupa chini? kwanini usiende kuoga nayo na hapo ufue kabisa, kama mnaoga pamoja yaani baba na mama pia bebeni mkafue wote, huu mtindo wa kurundika chupi ni uchafu sana, tubadilike jamani, house girl ni mtu kama wengine na ipo siku na yeye atakuwa na maisha yake tena usishangae hata kupita yako!!!
 
Hivi kwa nini hawa wasaidizi wa ndani wanaitwa "beki tatu"?

I think that's pejorative.
 
Sio sahihi hata kidogo huwezi muachia dada wa ndani ukoko wenu aufue wale huwa nawachukulia kama wadogo zangu unaweza mpatia mdogo wako chupi ya mumeo afue achilia mbali ya kwako.
 
kiukweli huo ni unyanyasaji.wanawake wa aina hiyo ni wale ambao hawana huruma na wavivu,kwa kuwa house girl anamlipa wao wanaona sawa tu.jee wao wangeweza kufua chupi za house girl wao?na nyie wanaume,kwa nini mshindwe kufua chupi zenu?mbana ni kazi ya dakika chache tu?ukifuliwa ki mapenzi na mke wako ni poa ila ahhh,jamani msijiendekeze.chupi ina heshima yake sio umpe dada wa kazi akufulie.mimi chupi yangu sipendi mtu yoyote yule aione.labda awe mpenzi wangu
 
Hicho kitendo siwezi kuruhusu kitokee..Nitafua mwenyewe ikishindikana My wifey yupo ndio afue sio Msaidizi wa kazi za ndani.
 
Back
Top Bottom