Ni haki halmashauri ya Ilala kuanza kuvunja nyumba mabondeni pasipo kujua wataenda wapi?

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Katika kutekeleza sheria ya kuwaondoa waliojenga mabondeni halmashauri ya ilala kupitia kwa meya wake jelly silaa wametoa tamko la kuvunja nyumba zote mabondeni ndani ya mwezi mmoja. je hili ni suluhisho au kuongeza tatizo? kuvunja nyumba bila ya kujua wakazi wa mabondeni wataenda wapi ni kuwasaidia au kuwaangamiza wananchi masikini?
 
hapo sasa wanataka kufanya kosa la karne! kwa jinsi walivyoacha watu wakajenga kwa wingi huko mabondeni nadhani utazuka mgogoro mkubwa sana.Anyway ni moja ya maamuzi magumu kuchukua ngoja tuone mwisho wake.
 
kuna taarifa kwamba wapo waliopata fidia enzi la mwinyi na makamba sijui ni kweli kwa kiasi gani kama wapo mwenye taarifa zaidi watuambie
 
serikali ya awamu ya nne imekuta wakazi hao wako mabondeni ni uamuzi mgumu lakini ipo siku itabidi ufikiwe
 
Itapendeza kama haki za binadamu zitazingatiwa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
 
Mbunge wao ZUNGU yuko wapi?? Inaelekea amesepa kutokana na matamshi yake bungeni kuhusu kuwaondoa watu wake Jangwani!!
 
Katika kutekeleza sheria ya kuwaondoa waliojenga mabondeni halmashauri ya ilala kupitia kwa meya wake jelly silaa wametoa tamko la kuvunja nyumba zote mabondeni ndani ya mwezi mmoja. je hili ni suluhisho au kuongeza tatizo? kuvunja nyumba bila ya kujua wakazi wa mabondeni wataenda wapi ni kuwasaidia au kuwaangamiza wananchi masikini?

ngoja tuone kama ataweza. Makamba ilimshinda hiyo maneno
 
Katika kutekeleza sheria ya kuwaondoa waliojenga mabondeni halmashauri ya ilala kupitia kwa meya wake jelly silaa wametoa tamko la kuvunja nyumba zote mabondeni ndani ya mwezi mmoja. je hili ni suluhisho au kuongeza tatizo? kuvunja nyumba bila ya kujua wakazi wa mabondeni wataenda wapi ni kuwasaidia au kuwaangamiza wananchi masikini?

Ipi bora warudi wafe au wahamishwe kwa nguvu ?

Ipi bora warudi wafe au wahamishwe kwa nguvu ?

Kuhama wahamishwe tu. Tena amri hii imechelewa sana. Tatizo ni wanakohamishiwa. Hakuna huduma yoyote ya maana kule Mbopo. Hakuna barabara. Hakuna maji. Shule ya msingi ni ndogo sana. WAnapewa viwanja vitupu na wanaohamishwa ni masikini wa kutupa.
 
Ipi bora warudi wafe au wahamishwe kwa nguvu ?

huku si kuamishwa bali ni kufukuzwa kwani kuhamishwa lazima kuwe na sehemu unayoenda lakini serikali imewafukuza hivyo wakalale kwenye mitaro na chini ya madaraja na maporini , nadhani itakuwa ni mbaya zaidi na wanavyofikiri
 
kwanza viwanda vilivyojengwa na kuziba mikondo ya maji vibomolewe i.e Al- hamza area

miundombinu inayokidhi ukuaji wa jiji ijengwe, then watakeleze yao
 
kwani wale waathirika wa mabomu gongo la mboto wameshajengewa nyumba kama walivyo ahidiwa?
 
Nadhani ni wakati sasa wa serikali kuanza kupima maeneo yote yasiyopimwa na kuweka mifumo ya maji taka na barabara za mitaa na kuanza kusimamia sheria za ujenzi katika miji ili mtu asijenge jengo lolote pasipo na kibali cha ujenzi la sivyo baada ya miaka 10 taifa litapoteza dira ya mipango ya miji na kutakuwa na msongamano na pia hakutakuwa na mfumo wowote wa huduma ya jamii kama umeme au mabomba ya maji yanayoweza kupita katika mitaa
 
hapo naipongeza serikali no kosa kubwa sana kuwaruhusu wajenge tena kwenye maeneo hayo
 
Absolutely yes!

Ni raia wangapi wa tanzania wanatafutiwa viwanjwa na sehemu za kuishi,

Think Big!

The rest ni politics.
 
waondolewe nasikia serikali imeshapaga maeneno.. tatizo wengine wanasema ni mbali na wao wanataka wakae mjini ... . najuwa kuna wanasiasa uchwara watalichukulia hili jambo kisiasa na ili kujipandisha chat
 
serikali imesema itatoa viwanja 2000 tu lakini nyumba zilizo mabondeni ni zaidi ya 20,000 unadhani nini kitatokea?
 
Back
Top Bottom