Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..

Nawasilisha..karibuni
Soma Ufunuo wa Yohana kuanzia mwanzo hadi mwisho, utajua hatma ya shetani na watu wote, na chunguza sana biblia unayoisoma kwani wameanza kuzibadilisha, usipende kuuliza mambo ya Mungu mtandaoni kwani waliojaa humo ni ......., kasome "Revelation"
 
Anaejua ni Mwenyezi Mungu mwenyewe hiyo faida anayoipata kwa hiyo ni ngumu kwangu Mimi Kama mwanadamu kujua faida anazopata isipokuwa mi ninachojua ni kutii amri zake!!!!!
Unaweza mtafuta mwenyewe ukamuuliza labda atakuwa na majibu.
Mbona akiulizwa anajibu, tatizo watu hawasali wenyewe, wakidhani kuenda kanisani pekee kutamfanya kujua ukweli, muombe mungu kwani hakuna binadamu atakayekujibu, hats akikujibu hutaelewa, sala tu ndiyo inayofunua watu na chanzo cha hekima.
 
Mungu hayupo! Ni mastory ya watu tu wajanja ! Nakuuliza swali: Kama Mungu aliwaumba Adamu na Eva, walikuwa weupe, sasa weusi , wachina, wazungu walitoka wapi? Aliwaumba siku moja, ilikuwaje wakaa kama walivyo sasa hivi! Kwa nini Mungu aliumba bacteria, virus etc wa kumuumiza mwanadamu? Aliwaumba lini na tunaambiwa aliumba vitu vya kumsaidia mwanadamu! Maswali ni mengi ukiyatafakari unaambiwa UNAKUFURU ili usidaisi
Yani shetani ameteka nafsi yako, kusema hivyo ni kudanganywa na shetani ambaye yeye mwenyewe anajua yupo na anamuogopa kama nn, anachofanya saivi ni kutafuta washirika wake motoni
 
Yani shetani ameteka nafsi yako, kusema hivyo ni kudanganywa na shetani ambaye yeye mwenyewe anajua yupo na anamuogopa kama nn, anachofanya saivi ni kutafuta washirika wake motoni
Jibu swali habari ya unakufuru iache kwanza
 
nafasi ya wanawake bado ipo chini hadi mbinguni wanaenda kutumiwa kama vyombo vya starehe.
Huyo katoa mfano wa dini nyingine, na dini nyingi ni za uongo, navyojua mm dini pekee chimpuko lake ni kwa Abrahamu, nyingine nni uongo, hats usipoamini saivi utaamini baadaye ukiwa katika hali ya majuto, WOTE mtaamini tu.
 
Wazazi na mababu wa huyo abraham walikua dini gani au hakukua na dini?
 
Hivi umu kuna vivuli vya watu binadam au vivuli vyamashetani au mashetani wenyewe? nahisi kuna mashetani wanawacharenji watu humu kwanye uziii huuuu!
 
Mungu hayupo kwa hiyo wewe amekuumba mamako siyo??

........hahahahaahaha! imekosekana (u na k) mwazo dah atari chariiii wangu!
 
Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..

Nawasilisha..karibuni

Una pepo wewe si bure, uponywe.
 
Back
Top Bottom