Ni chakula gani hupendi, mimi sipendi ndizi za kupika

Wewe ndizi huzijuwi,ulikula ndizi wanazo tumia. kupika pombe, Siku utapokula ndizi,zikapata mpikani,hutatamani chakula kingine
 
kuna makande yanapikwa kama pilau achana na hayo maharage yaani ukipikiwa na wataalam kama sisi utahamia.
ujue hakuna chakula kibaya sema ni mapishi na ulle mpangilio wa kula .chakula chochote ukila kila siku unakinai .chakula kilekile mapishi yale yale ndo tatizo la waafrica

Na wewe utakua ni mpare tu, maana si kwa kwa kupenda huko makande ,umeyasifiaa,mi nikila sishibi,nasikia njaa mara moja.
 
Mimi sipendi wali,pilau,chips,ugali sembe bali napenda dona,mboga za majani,matunda,viazi vya kuchemsha,majimbi ya kuchemsha, ndizi nyama,asali,juice ya mchanganyiko wa mboga za majani na matunda,maziwa e.t.c
 
Kusema kweli ndizi nazipenda zilizoiva tu nakula kama tunda ila sio ndizi za kupika.

Ndizi za kupika nakula tu kuzuia kifo panapokua hakuna chakula kingine.

Katika chakula nisichokipenda zaidi Duniani ni ndizi za kupika.
Tumefanana
 
Back
Top Bottom