Ni chakula gani hupendi, mimi sipendi ndizi za kupika

Kusema kweli ndizi nazipenda zilizoiva tu nakula kama tunda ila sio ndizi za kupika.

Ndizi za kupika nakula tu kuzuia kifo panapokua hakuna chakula kingine.

Katika chakula nisichokipenda zaidi Duniani ni ndizi za kupika.


Binafsi siupendi Ugali na haijalishi kuna mboga gani, nakula Ugali tu kama sina jinsi lkn siupendi na hata kama ukipigwa marufuku kwangu poa tu na kamwe siwezi kuumiss!
 
kuna makande yanapikwa kama pilau achana na hayo maharage yaani ukipikiwa na wataalam kama sisi utahamia.
ujue hakuna chakula kibaya sema ni mapishi na ulle mpangilio wa kula .chakula chochote ukila kila siku unakinai .chakula kilekile mapishi yale yale ndo tatizo la waafrica

Hapo kwenye bold and blue ndio point haswa ilipo mengine mbwembwe tuuu
 
Sipendi ugali nyama
Sipendi ugali maharage
Sipendi makande
Sipendi yai la kisasa kuku wa kisasa nikila naskia kichefuchefu
 
Ukianzishwa Uzi wa msosi niupendao Nna mengi yakuongea apa ata sijui nn sipendi sababu misosi mingi mibovu tu
 
Mie huwa najaribu kila chakula hata nilivyokuwa siviwezi sasa nakula,ila vitu vilivyonishinda ni soseji na maziwa ya mtindi.
 
Back
Top Bottom