Ni chakula gani hupendi, mimi sipendi ndizi za kupika

kuna makande yanapikwa kama pilau achana na hayo maharage yaani ukipikiwa na wataalam kama sisi utahamia.
ujue hakuna chakula kibaya sema ni mapishi na ulle mpangilio wa kula .chakula chochote ukila kila siku unakinai .chakula kilekile mapishi yale yale ndo tatizo la waafrica
Kenya makande yao yanaitwa Githeri wanaongeza vikorombwezo mfano viazi ulaya,mboga mboga etc iko vizuri sana
 
ahahaa huyo maza house wako hajui kuchanganya misosi huwezi kupika bilinganya peke yake linaboa bilinganya unachanganya kwa maharage yawe na nazi halafu ulie wali mzee au kwenye dagaa au samaki utalipenda mwenyewe.bilinganya lina afya sana mimi nalipika sana
Njaa inauma.. dah
 
Kwa ujumla sivutiwi sana mboga zenye mafuta mengi hasa michuzi michuzi .

Na kama utanikuta nakula basi mpishi alipika kwa ustadi mkubwa hadi kunivutia .

Ila kuna products zisipende sababu zinaniletea kichefuchefu hasa kama nikizitumia zaidi ya Mara moja

Mfano

Blue band

Siaga ya karanga.

Haya madude huniletea kichechefu so kwangu no taboo.

Pia mi in mpenzi mkubwa Wa nyama na samaki hasa kama ni za kubanika

Beside nakula kila msosi ukitoa hiyo niliyoorodhesha.

Ila sio misosi ya kihindi no never kwa kweli
 
Back
Top Bottom