Ni bora tu ATC ifutwe.....

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Kuna tetesi kuwa serikali iko mbioni kulifuta kabisa shirika la ndege Tanzania (ATC) kutokana na shirika hilo kutokuwa na tija kwa serikali. Habari zinapasha kuwa licha ya serikali mara kadhaa kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha bado shirika hilo halijaonyesha dalili ya kutoka kwenye usingizi wa pono hali inayopelekea kuonekana ni gunia la misumari lisilobebeka...Hata mimi binafsi naunga mkono wazo hilo huenda tukaja kuwa na kitu kipya chenye matumaini na si ATC ya sasa.

My take:
Ilisemekana kuwa ATC itatafutiwa mbia ambaye huenda ikawa kampuni ya kichina. Nina wasiwasi kama kweli serikali kwa kufanya hivyo itakuwa imetatua tatizo. Huenda tukarudi kwenye mambo ya Net- Group solution na Tanesco. Kwa hiyo tunawashika masikio na msikie kuwa mchinaaaa kimeo!!:mad2:
 
Sasa ni wakati wa kuanza upya ATCL




27th May 2010








KATUNI(193).jpg





Maoni ya katuni



Jana katika ukurasa wa kwanza wa gazeti hili kulikuwa na habari iliyosema ‘ATCL ni bomba linalofuja fedha' ikieleza taarifa zilizotolewa kwenye kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi na ofisa kutoka Hazina jinsi Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limekuwa mzigo.
Ofisa huyo tunayethubutu kusema kuwa ana ujasiri, alisema wazi kwamba ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara kubwa, huku ikitegemea kupewa fedha kutoka Hazina kwa ajili hata ya kulipa mishahra na gharama zake nyingine za kiuendeshaji kama vile ada na malipo mengine ya kisheria.
Kauli hiyo tunaiona kuwa ni ya kuthubutu kwa sababu Ofisa huyo anajua vilivyo kwamba serikali imekuwa na mtazamo tofauti na huo alioutoa juu ya ATCL. Serikali na kama alivyosema Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, imekuwa na msimamo kwamba wanataka kufufua ATCL na kwa sasa wanaitafutia mbia, ingawa inajua fika kwamba kwa kiwango cha madeni ilicho nacho ATCL itakuwa ni kazi ngumu sana kumpata mwekezaji au mbia wa maana hasa ikizingatiwa kwamba mashirika mengi ya ndege duniani kwa sasa yako kwenye msukosuko mkubwa kiuchumi.
Tunajua kwamba ni fahari kwa taifa kuwa na shirika lake la ndege, lakini fahari hiyo ni lazima iwe na maana, kwani kuwa na shirika mzigo kama ATCL ambalo halijiendeshi lenyewe hata kumudu gharama zake muhimu achilia mbali kutoa gawio kwa serikali, haina maana; ni hasara; ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma kwa maana ya kodi za wananchi ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye mambo mengine muhimu zaidi.
Hakuna asiyejua historia ya ATC kabla ya kuwa ATCL; tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini kumekuwa na juhudi kubwa za kuvunja nguvu ndogo ya ATC iliyokuwapo, kwanza ilikuwa ni kuiunganisha na AJAS ambayo ilishindikana, lakini baadaye ikauzwa kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) hadi miaka michache iliyopita ndoa hiyo, ambayo haikuwa na manufaa kwa ATCL, ilipovunjwa.
Kwa maelezo mengine ATC na sasa ATCL imepita katika mabonde na vikwazo vingi kwa muda mrefu; imetengenezewa mikakati ambayo kwa hakika haijikiti kutazama ni wapi tulikosea, ndiyo maana kila hatua inayochukuliwa kwa nia ya kuiokoa badala ya kuwa neema inakuwa ni balaa zaidi ya awali.
Kwa wastani kwa muongo mmoja na nusu sasa tunaweza kusema wazi na bila hofu yoyote kwamba ATCL imeshindwa kubadilika kuwa shirika la umma linalojiendesha kwa ufanisi uliokusudiwa na kwa maana hiyo kweli iwe fahari ya Tanzania kama yalivyo mashirika ya ndege ya mataifa mengine ulimwenguni.
Sisi hatuna kinyongo chochote na ATCL ila tunaumwa na kuona uchungu wakati taifa hili linashindwa kuwa na shirika la ndege linaloweza kutimiza wajibu wa kusafirisha raia wake hata kama ni ndani ya mipaka yake tu achilia mbali safari za kimataifa. Watazania wamekuwa wanajiuliza tena na tena ni kwa nini tunaendelea na utaratibu huu wa kukumbatia kitu ambacho kimekwama? Ni kwa nini basi tusianze upya kwa kuzingatia mazingira mapya, changamoto za sasa na kujielekeza katika utendaji unaowekewa malengo ili tuwe na shirika linalojiendesha kwa ufanisi na kuleta tija?
Kwa maoni yetu msimamo wa serikali kisera wa kutaka bado kuibadili ATCL hii kwa kutafuta wabia, hakika tutapata matatizo tu; hatusemi haya tukiichuria ATCL, ila tunasema hayo kwa kuwa njia pekee ingekuwa ni kukubali yote yaliyotokea, kuivunja ATCL na badala yake kuanza upya.
Tuanze kuliunda upya kwa kuzingatia mambo mengi, kwanza changamoto za sasa na mbinu za sasa za kuendesha mashirika ya ndege, kuwa na damu mpya ya watendaji ambao wanatambua maana na umuhimu wa kujiwekea malengo, wajue kwamba bila kuzalisha faida ya kujiendesha shirika hilo haliwezi kuwa na nafasi katika sekta hiyo.
Utaratibu wa kuendelea kuchota kodi za wananchi na kutoa kwenye mashirika yasiyojiendesha yenyewe ni utaratibu uliopitwa na wakati. Kama vishirika vidogo vya ndege vinajiendesha kwa ufanisi mkubwa tena ndani ya Tanzania ni balaa gani inaifanya ATCL nayo isifanye hivyo pia? Tukatae kuendelea kuidekeza ATCL, imeshindwa na sasa tuanze upya, inawezekana!




CHANZO: NIPASHE
 
ni huzuni kusikia hivyo, ni aibu kwa kweli. hivi tumekosa wataalamuu, pesa au nini hadi kufikia hali kama hii? bila shaka itakuwa ni nchi pekee africa kufikia hatua kama hiyo.
 
Hiyo katuni inanikumbusha kitabu kimoja cha kiswahili nilikisoma kati ya darasa la 4 au 5. Jina la kitabu limeandikwa "Tujifunze Lugha Yetu" kuna hadithi ya yule nyoka anaitwa Nonda mla watu....Wale wenzangu tuliosoma mwaka 47 nadhani mnakumbuka hii.........Hiyo ATCL inapiga hatua 2 mbele na kurudi nyuma hatua 10 safari hatufiki miaka nenda rudi aibu kabisa.:target::target::target:
 
ni huzuni kusikia hivyo, ni aibu kwa kweli. hivi tumekosa wataalamuu, pesa au nini hadi kufikia hali kama hii? bila shaka itakuwa ni nchi pekee africa kufikia hatua kama hiyo.

Inasemekana kuwa Bwana Msella ambaye ni kaimu msajili wa hazina ameshauri kuwa Atcl shirika la ndege Tanzania liwaachishe kazi wafanyakazi wote na lianze upya kama serikali ilivyofanya kwa NIC [ shirika la bima la Taifa]. Ingawa ushauri huu ni mzuri on the surface lakini ukifanya uchambuzi makini sidhani hatua hizo zitatatua matatizo yanayoikumba ATCL. Kwanza kabisa huwezi kulifananisha shirika la Bina na shirika la Ndege kwani mahitaji yao kiutaalamu na kimtaji hayafanani; leo hii ukiwaaachisha kazi marubani wote na engineers wa ndege ambao hivi sasa ni haba sana duniani, haitakuwa rahisi kuwapata wengine kuziba nafasi zao. Pili mtaji unaohitajika kuliendesha shirika lolote lile la ndege kibiashara ni mkubwa ; Utahitaji kununua ndege zaidi ya moja pamoja na vupuri vyake vinavyohitaji kubadilishwa mara kwa mara kukidhi mahitaji ya usalama angani, marubani na wahandisi watahitaji mafunzo ya mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya tekinolojia ya ndege duniani na vyote hivyo vinahitaji pesa. Tofauti na NIC, unapowaachisha kazi marubani na wahandisi wote itakubidi uwalipe fedha nyingi halafu utalazimika kuwaajiri tena hao hao kwani hawa wana utaalamu adimu!! Serikali inajua fika matatizo ya ATCL ;kuwa shirika halikuwa na vitendea kazi vya kutosha yaani NDEGE na pia management ya shirika haina uweo unaotakiwa katika kuendesha shirika hilo!! Hayo ndio mambo ambayo hata wakiachishwa hao wafanyakazi wachache waliobaki [kwani ATCL ilipunguza wafanyakazi wengi hivi karibuni] ni lazima iyashuhulikie!! Ili shirika La ATCL liwe commercially viable suluhisho sio kuwafukuza kazi marubani na wahandisi bali ni kuongeza mtaji kwa kununua ndege nyingine na kuwa na management inayoielewa biashsra ya ndege. Waziri Kawambwa amekuwa akilidanganya bunge kila kukicha kuwa muwekezazi mchina amepatikana kuja kuwekeza na kuleta management yake lakini mpaka leo hii hakuna lolote la maana aliloweza kufanikisha na Ilani ya CCM inasema pamoja na Rais kuahidi mara chungu nzima kuwa wataimalisha ATCL!!. Hawa wasanii kazi yao kubomoa mali zote Nyerere alizowaachia; waliuza mabenki na viwanda sasa wanamalizia shirika la ndege
 
Mi kinachonishangaza ni kwa vipi mashirika mengi yalianzishwa wakati wa utawala wa awmu ya kwanza kwa lengo la kuijenga nchi katika misingi ya kujitegemea eti yanatushinda. Tena katika nyakati hizi tukiwa na wasomi wengi wazalendo kuliko miaka ile wasomi walikuwa wachache. Mi binafsi nampongeza sana Mwl. Nyerere nadhani alikuwa na ndoto za maana. Sasa hivi kila shirika linapukutika mara mengine yabinafisishwe kw kweli inaniuma sana. Yaani kila kukicha ni afadhari ya jana!!:target::target::target:
 
Back
Top Bottom