Ni bora CHADEMA ifutwe

Kweli kabisa! Chadema kifutwe na huyu ajiuzulu! Aliwezaje kufanya " PH.D" akiwa na vi-cerificate tuu? "Doctor wa ukweli" !!!!

======================================================================
EDUCATION
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993

TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985

St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981

St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]

Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973

Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969

Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960

======================================================================

 
Baada ya kupoteza dira na mkondo wa siasa za kidemokrasia, na dhamira halisi ya kuwepo upinzani, chadema kimepoteza uhalali wake wa kisiasa hivyo hakuna sababu kuwapo katika daftari la msajlli wa vyama vya siasa Tanzania, hivyo kifutwe!

Nasema hivyo kwa sababu chadema baada ya kukubali mtego wa CCM wa kupenyeza mamluki ndani ya chama chao wakiwamo magwiji wa usalama wa taifa wastaafu (Mabere N. Marando), pamoja na magwiji wa siasa za kipropaganda kutoka CCM (John M. Shibuda), hakina tena ile rangi yake ya siasa za upinzani.

Akina Marando wanafanya kazi yao ndani ya chadema, ya kushawishi vurugu makusudi ili kuharibu muelekeo wa chadema ulionza nao, naye ameshafanikiwa hilo, kama alivyofanya na kufanikiwa akiwa ndani ya NCCR-Mageuzi, yeye na Agustino Mrema.

Maoni yangu, chadema kifutiliwe mbali, tayari kimeshajionyesha au kimeshafanywa kijionyeshe kuwa hakitaki siasa za ushindani bali vurugu na kuleta machafuko nchini.

Mbali na kugeuzwa huko kwa hila za makusudi, chadema kimegeuka na siyo chama cha matumaini kwa wantanzania kama kinavyojidai, au kinavyodanganya wananchi, kwani ndani ya dhamira za baadhi ya viongozi wao ni kukifanya chama kuwa mtaji wa kukuza vitega uchumi vyao na kujipatia fedha tu.

Chama kinachojiita, au kinacholazimisha kuwa ni chama rasmi cha upinzani bungeni hali ya kuwa hakiwakilishi jiografia ya upinzani wa Tanzania, hakiwezi kuwa na uhalali wa kusimama na kujiita chama cha kitaifa, hivyo kifutwe!

Wakati bunge la Tanzania lina vyama vingi na wabunge wa vyama kutoka maeneo tofauti, chadema kama chama rasmi cha upinzani bungeni kinawakilisha majimbo kinayoyaongoza tu, katika serikali yao kivuli, wakati wananchi wa maeneo mengine ambao wamechaguwa upinzani pia hawana uwakilishi wowote ndani ya serikali kivuli ya chadema.

Kwa maana hiyo basi chadema wamepoteza uhalali wa kuwa chama cha kitaifa, hivyo Kifutwe!

keep on dreaming Mr...CHADEMA imewakamata.
 
Kama Cdm ikifutwa,2tajua wapi mambo ya ufisad?maana ccm,nccr,tlp na cuf,ni chama kimoja kwa sasa!TANZANIA YENYE USAWA BILA CHADEMA HAIWEZEKANI
 
Ikiwa Chadema imeshindwa na ustaarabu bora Msajili akifute Chama hiki,chama ambacho kinashindwa kujidhibiti na kuwezaa kufuata mkondo wa kisiasa,kwa nini hawaiangalii CUF wapi imetoka na wapi ipo ,hii leo !!

Mimi nawashauri Chadema wasitishe kuingia kwenye Bunge mara moja,nawahakikishia serikali itabadili muelekeo ,ni lazima itabadili muelekeo na vile vile lile lengo la kutomtambua Kikwete kama Raisi halali au alieshinda kihalali, hapo hapana ubishi ni lazima CCM na serikali yake ikae sawa na ni njia moja ya kidemokrasia kabisa.

Lakini kuwarubuni wananchi wakati mnaingia bungeni na kula na kusaza ,hili halikubaliki kabisa kisha kutaka kuwaburuza wananchi kwenda kuchezea maji ya washawasha ,nyie wabunge mnakuwa tandize na majokofu ya jumba la bunge,huo utakuwa utapeli kushinda wa mafisadi,amueni moja tuwafahamu.


Mbona unayumba saaaaaaaana katika misimamamo yako???!!! Sikuelewi kabisa; wana jf watanisaidia!

 
:decision:Watu wengine huwa ni wakuwasikitikia mno.wajua sisi tuna support upinzani haimaanishi ndani ya CCM hakuna watu wazuri ila wapo na ndani ya CCM sera zao wanawapiga vita wale ambao ni wazuri watendaji kazi tumeyaona hayo.unaposema kifutwe hasa kwa lipi wakati chama ndicho kimeshika hatamu za uongozi Mbagala imelipuliwa hatujakaa sawa hata kusahau yaliyopita Gongo la mboto nayo yajibu watu wamepoteza maisha yao na mali ndani ya hiki unachojiita wewe chama chako kwa nini usijitokeze na kuanza kukinyoshea chama chako na serikali yake kiwe cha kwanza kufutwa unakimbilia Chadema. FIKIRI, ZINDUKA NA USOME ALAMA ZA NYAKATI.
 
Jakaya Kikwete Mlimani BA economics Pass!!!
experience
Member of TANU youth league
Political Lieutenant Canal (cermonial position)
DR(ceremonial position).
 
Cha umuhimu nikupata wanaoweza kuikosoa serikali pale inapokosea, inaposhindwa kujisahihisha. Chadema wmeonyesha wanadhubutu kufanya hilo. Naona chama hiki kisifutwe.
 
Huyu Kada Aliepost Hii Comment Inawezekana Yupo Nyuma Kifikra. Kitu Tunafahamu Mpaka Sasa ni Kwamba Kura JK Alipata 27% na Hii Inaonyesha Chama Gani Kifutwe Katika Demokrasia. Sijui Kipimo Kipi Huyu Kada Anaweza Kutuonyesha Chadema Ifutwe! Chama Kipi Kimewaumiza Watanzania Mpaka Sasa? Jibu Lipo Kwako Makada-green jackets...
Yes buddy the guy just get only about 27% of all eligible voters of Tanzania who were about 19millions according to electoral commission so he will never stand strong on his feet as a union president!!!
 
Bwana mwiba hujui ulisemalo, pole sana, but tutakuombe ili uondokane na hiyo narrow and impovershed thinking.
 
Back
Top Bottom