Ni Bagamoyo au Bwagamoyo?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Wana jf nawaombeni Mnisaidie kunijuulisha kuhusu huu mji unaitwa bagamoyo au bwagamoyo? Nawaombe ni munisaidie lugha imenichanganya asanteni.
 
Wana jf nawaombeni Mnisaidie kunijuulisha kuhusu huu mji unaitwa bagamoyo au bwagamoyo? Nawaombe ni munisaidie lugha imenichanganya asanteni.

Kaka MziziMkavu...hapo mahali panaitwa "Bagamoyo" na sio "Bwagamoyo".

Niliwahi kutembelea Wilaya hiyo mwaka 1989 na kwa bahati nzuri nilifika Kaole na kuonana na Mzee Asante Rabi....Kwa wasiomfahamu Mzee Rabi ni mtunza kumbukumbu za kihistoria katika Eneo la Kaole.

Alinipeleka katika Eneo lililozaa jina Bagamoyo...Hapo mahali ni sehemu yenye gati kuu...ambako watumwa kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika walikuwa wanapandishwa katika Majahazi kuanza safari ya kupelekwa Uajemi...Wazungu walipaita "Point of No return".Mtumwa ukifika sehemu hiyo unaambiwa "Bwagamoyo wako" kwa sababu hutegemei kurudi tena ulikotoka....Wazungu walishindwa kusema Bwagamoyo wakawa wanatamka "Bagamoyo" hiyo ndio asili ya jina Bagamoyo.
 
Ahsante mkuu Mawado,

Kama alivyosema mkuu, jina kamili la kale lilikuwa Bwagamoyo, ila jina lilibadishwa kidogo kidogo hadi likawa Bagamoyo badala ya Bwagamoyo!

Tofauti ni kuwa katika miaka mingi ya nyuma niliwahi kujulishwa Mwalimu wangu mwenyeji wa Bwagamoyo (ni marehemu kwa muda mrefu sasa, na pia namwombea Muumba amlaze mahala pema peopni) kuwa paliitwa Bwagamoyo kwa uzuri, na jinsi ambavyo ukifika hiyo sehemu una relax, na mawazo yote yanakuishi ukipata upepo mwanana wa mwambao, na kujishtukia tu moyo wako, shida zako na mawazo yako umeyabwaga hapo hapo kwa kuridhishwa tu na man dhari nzuri na upepo mwanana wa pwani hiyo ya Afrika!

Pia alitutaarifu (sisi wanafunzi wake) kuwa hata hao wazungu waliridhika na hilo jina, kwani hata wao walipapenda na kuanza kupajenga, na kwa kushindwa kutamka Bwagamoyo wakapaita Bagamoyo, na watu weusi tupendavyo kuiga ikawa nongwa, nasi tukaiga lafudhi yao na kupaita bagamoyo!

Ahsanteni, niliona ni bora nami nitoe machache niliyojulishwa na huyo mzee wetu ambaye kwa sasa ametangulia mbele ya haki.
 
mzizi mkavu ule mji unaitwa Bwagamoyo na sio Bagamoyo, ila kama ujuavyo watu huwa wanabadilisha lakini enzi hizo uliitwa Bwagamoyo ila kwa sasa inafahamika kama bagamoyo mkuu
 
ebwana hiyo ni nuri sana, wana lugha naona kuna uzamaji wa kweli kwenye hii bahari,lakini mie nina kajiswali kadogo sana, hivi wazungu hawa mbona wanakosea sana, na kuharibu majina yetu, mfano liringa-iringa, idodomya- Dodoma. na mengine mengi na pia je? hakuna majina ya sehemu wakaazo wazungu hao ambazo waswahili nasi tulikosea na baadaye yakaitwa kuendana na lafudhi zetu wabantu au waafrika, naombeni tusaidiane katika hayo akhsanteni........
 
Back
Top Bottom