Ni aibu kubwa mwanasiasa kujidhalilisha kiasi hiki...

Hiiii nchi ina watu wa ajabu sana,sijapata kuona yaaani mtu yupo upinzani(UPDP) baada ya kuikemea serikali yeye anakemea upinzani,yaaani ni vitu vya ajabu sana,huyu Dovutwa si yule aliye jitoa siku za mwisho kwenye kampeni(uchaguzi) na kusema kwamba kula zake apewe jk?Kwa maana hiyo yeye ndio mtu wa kupimwa akili.Jinsi alivyo anaonekana tu kuwa kichwa chake kibovu,na anatumika na serikali ya magamba kuwapinga na kuwakosoa wapinzani,kwa sababu yeye sio mpinzani.
 
Watu kama hawa ni kuwaacha walopoke, ili mradi tu hawaendi nje ya maadili na ukiukwaji wa Katiba. WaTanzania watachambua na kuamua lipi jema na baya, pumba na mchele. Yeye kaongea leo, kesho watashuka Chadema na timu yao, baadae wananchi watachambua nani GARASA na MKWELI.
 
-Hivi huyu bwana ni Press Secretary wa Magamba? au ni wa Serikali?

-Siasa za sampuli hii ya "Upinzani" ziko Tanzania tu!

-Mwenye picha za waliohudhuria mkutano huo atuwekee tuone idadi ya "wapuuzi" wenzake.

Picha watoe wapi? Who is Dovutwa by the way? Acheni kujadili ujinga wa huyu kibaraka, anatafuta namna ya kutoka.
 
Ndugu Dovutwa, katiba ya nchi yetu haikuzuii kurejea chama tawala kama utaona inafaa, nibora ukarudi huko kuliko kuwa sehemu ambayo huifai, kuwa na roho ya kibinadamu waachie wenye mlengo wa kuwakomboa watanzania waendelee na harakati za ukombozi
 
Ni kweli imetokea ingawa ni kama utani.Juzi vyombo mbalimbali vya habari vilitangaza kwa mbwembwe kwamba chama cha UPDP kitafanya mkutano wake wa hadhara jana katika viwanja vya bakhresa manzese.Lengo likasemwa ni kuwashukuru wapiga kura na kuimarisha chama.Ilipofika jana viwanja vilipambwa kwa maandalizi ya nguvu.Sisi wengine tukajiuliza nguvu hii ya maandalizi makubwa kwa UPDP imetoka wapi? Muda ulipowadia mkutano ukaanza na mwenyekiti wa UPDP Fahm Dovutwa akapanda jukwaani.Badala ya kutangaza sera kama walivyodai,akaanza kuporomosha matusi dhidi ya chama cha Chadema na viongozi wake.Aliongea mpaka mishipa ikamtoka huku akiomba msajili wa vyama John Tendwa akawapime akili viongozi na wanachama wa chadema.Alisema atapambana na chadema mpaka mwisho ili kulinda amani ya watanzania.Nikadhani kwa upupu ule alioongea hakuna chombo cha habari ambacho kingeripoti habari ile.Lakini asubuhi magazeti pendwa ya UHURU na JAMBA LEO yameongoza na kupamba ukurasa wa mbele kwa upupu wa Dovutwa kana kwamba hakuna habari yoyote muhimu iliyotokea jana.
Mimi nadhani ifike mahali wanasiasa uchwara wanaotukana wenzao badala ya kutangaza sera za vyama vyao wazomehe kila wanapohutubia mpaka watakapoachana na tabia zao mbaya kwa vyama vingine...

Kwanza inatakiwa yeye ndo aimwe akili kabla ya kudhani kwamba wenzake ndo wanastahili kupimwa.

Pili inatakiwa huyu jamaa aanze kuonjeshwa joto ya jiwe kwa huu upuu anaotapika, wananchi wanatakiwa wawe wanamzomea anapoanza kutapika, bahati yake anakwenda kuhutubia manzese siku akipotea njia akaja kumwaga upupu mtaani kwetu atapata fundisho!!

Tatu magazeti ya uhuru na jamba leo yasikupe shida, we endelea kuyasoma kupitia redio na television, hakuna mtu mwenye akili timamu anayanunua, zaidi ya wenye magamba.
 
Kama vyama vya upinzani vipo kwa ajili ya kushika dola siku moja, hiki naona kimepotea njia kwani kupambana na CHADEMA hakutawasaida. CHADEMA hawashikilii hiyo dola ambayo wao wanaitaka.
 
Ukweli ni kwamba hata wafanye vipi mwisho wa siku kilakitu kitakuwa wazi, itajulikana kuwa nani yuko nyuma ccm na nani ni mpinzani wa kweli. Mwenye nia njema na mapenzi mema na tz.
 
Hili sio kwa Mwenyekiti wa UPDP tu, bali ni tatizo kubwa la vyama vya Upinzani Tanzania kuanza kupingana wenyewe kwa wenyewe ina maana hawafahamu wanacho kitafuta. Tangu mfumo wa vyama vingi uanze hakuna chama ambacho hakijawahi kukisema cha kingine vibaya, halafu wanalalamika kuwa CCM inashinda kila mwaka, kwa nini CCM isishinde ilihali wapinzani hawaaminiki? Hata kama Sera zao ni tofauti, kuna sababu gani ya kusemana majukwaani? Kusema majukwaani ina lengo kuchafuana na kubomoana. Kwa nini wasikae pamoja waakaelezana mapungufu ili kujenga upinzania wenye nguvu na wakweli? Tatitizo ni kwamba kila mmoja anataka kuwa Rais ilihali nafasi ya Rais ni moja tu. Je, ipo siku hawa wataungana dhidi ya chama chochote Tawala?
 
Hii ni Useless Thread hapa JF. huwezi kuijadili maiti tuna mambo ya msingi ya kujadili ya Nchi yetu.
 
Anatafuta umaarufu kupitia Cdm! CDM inawakuna vilivyo. Hawalali bila kuiota CDM. Pongezi kwa CDM.
 
Nadhani Dovutwa kwa kauli yako hiyo hata mtoto mdogo atakucheka. Unajitungia maneno ya kipropaganda na kuyabubujika.
 
Ni kweli imetokea ingawa ni kama utani.Juzi vyombo mbalimbali vya habari vilitangaza kwa mbwembwe kwamba chama cha UPDP kitafanya mkutano wake wa hadhara jana katika viwanja vya bakhresa manzese.Lengo likasemwa ni kuwashukuru wapiga kura na kuimarisha chama.Ilipofika jana viwanja vilipambwa kwa maandalizi ya nguvu.Sisi wengine tukajiuliza nguvu hii ya maandalizi makubwa kwa UPDP imetoka wapi? Muda ulipowadia mkutano ukaanza na mwenyekiti wa UPDP Fahm Dovutwa akapanda jukwaani.Badala ya kutangaza sera kama walivyodai,akaanza kuporomosha matusi dhidi ya chama cha Chadema na viongozi wake.Aliongea mpaka mishipa ikamtoka huku akiomba msajili wa vyama John Tendwa akawapime akili viongozi na wanachama wa chadema.Alisema atapambana na chadema mpaka mwisho ili kulinda amani ya watanzania.Nikadhani kwa upupu ule alioongea hakuna chombo cha habari ambacho kingeripoti habari ile.Lakini asubuhi magazeti pendwa ya UHURU na JAMBA LEO yameongoza na kupamba ukurasa wa mbele kwa upupu wa Dovutwa kana kwamba hakuna habari yoyote muhimu iliyotokea jana.
Mimi nadhani ifike mahali wanasiasa uchwara wanaotukana wenzao badala ya kutangaza sera za vyama vyao wazomehe kila wanapohutubia mpaka watakapoachana na tabia zao mbaya kwa vyama vingine...
Its funny!!..huyu jamaa anajiita mpinzani wakati at first alsema kura zake ziende kwa kikwete....may be hakufafanua ni mpinzani wa upinzani,hope that was the meaning,ni mchumia tumbo huyo atafanyaje na yeye anatafuta mkate wa kila siku,nashangaa sana nawadays vyama vyote vinaishambulia CHADEMA whats wrong...ndio maana mpinzani wa kweli hii nchi ni chadema tu hao wengine wote ni vibaraka..
 
''Mkinipa kura zenu nitajenga kiwanda Cha Silaha Tanzania'' - Fahmi Devutwa, Presidential Candidate in 2010 Tanzania Elections.

Nafikiri jamaa yuko right kwa swala la Wanawania Urais Kupimwa akili.
 
Ukijipendekeza sana hata kwa hao unaojipendekeza kwao watakudharau..
 
Kagamba kadogo hako na kenyewe kamepata uwanja wa kuongea pumba basi naye anajifanya Kenge kwenye msafara wa Mamba
 
''Mkinipa kura zenu nitajenga kiwanda Cha Silaha Tanzania'' - Fahmi Devutwa, Presidential Candidate in 2010 Tanzania Elections.

Nafikiri jamaa yuko right kwa swala la Wanawania Urais Kupimwa akili.
Huyu jamaa sijui hata alitokea wapi
 
Back
Top Bottom