Ni aibu kubwa kuwa ombaomba huku tukigawa mali kama njugu!!

KIKAO cha Bunge cha leo kinatarajiwa kupokea na kujadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Leo ni siku muhimu mno kwa wabunge kuhoji na kupata majibu ya kina kuhusu masuala mengi yanayoihusu wizara hiyo.

Kuna mifano mingi na hai katika dunia hii, inayothibitisha wazi kuwa kuna mataifa yanayostawishwa na utalii pekee.

Kwa mfano, nchi ya Misri yenye mto mmoja, na iliyozungukwa na jangwa la kutisha, pamoja na kuwa na mafuta, utalii unaiingizia mabilioni ya fedha kila mwaka.

Tanzania inaweza kuwavutia watalii wengi zaidi kuliko Misri. Ina hazina kubwa mno. Jana tu, imetolewa taarifa kuwa michoro ya watu katika mapango yaliyopo Kondoa, imetangazwa na UNESCO kuwa ni eneo la urithi wa dunia.

Maana yake ni kwamba, tukiwa makini kutangaza kivutio hicho na vingine visivyo idadi, tunaweza kupokea watalii wengi kupindukia.

Asilimia 20 ya ardhi ya Tanzania ni hifadhi ya wanyama na viumbe wengine. Hii imeipa sifa kubwa Tanzania.

Pamoja na sifa hiyo, Watanzania wameendelea kuwa makabwela. Utalii wa uwindaji umehodhiwa na kundi la wageni kutoka pande zote za dunia.

Watanzania wamebaki kuwa yatima, wakitaabika na kufa kwa maradhi yanayotibika, lakini hawana hata pesa za kununua dawa.

Wageni wanakusanya mabilioni ya shilingi kila siku, hakuna kodi zinazolipwa serikalini, na hata pale zilipolipwa, kiasi kilichotolewa ni kidogo mno. Ni aibu na fedheha.

Idara ya Wanyamapori inapaswa ifumuliwe ili iundwe upya. Kuna watu wamekaa kwenye idara hiyo kwa miaka 15. Hawa wamebweteka na kujiona kuwa wana haki ya kutapanya utajiri huu.

Wanashirikiana na wageni kuwanyima haki wazalendo ili waweze kushiriki shughuli hii muhimu.

Mtu mmoja na mwanawe wanamiliki eneo katika hifadhi ya Selous ambalo ukubwa wake ni sawa na nchi ya Djibouti! Mtu anapewa nchi! Tumlaumu nani? Umasikini wetu kwa nini tumtupie lawama Mungu?

Serikali ya Awamu ya Nne inapaswa ionyeshe nia ya kweli ya kuwakomboa Watanzania. Watanzania hawawezi kukombolewa na wageni wanaohodhi kila kazi, hata zile zinazoweza kufanywa na wenyewe kwa ubia na wageni.

Dhamana ya Watanzania iko mikononi mwa wabunge makini wanaohoji na kudadisi mambo.

Wabunge makini si waoga, si wabinafsi, na si wazembe katika kuitetea nchi na wananchi wao. Wabunge makini hudai majibu sahihi kwa maswali wanayouliza.

Nayo serikali huwasikiliza wawakilishi wa wananchi na kutoa majibu ya kuleta suluhu. Tunaamini kwa dhati kabisa kuwa, suluhu ya sasa ndani ya Wizara ya Malisili na Utalii, kama zilivyo wizara nyingine zenye mamangi meza, ni kuzifumua; na kuziunda upya.







**********************


Jamani wabunge amkeni nchi inzidishi kumalizwa! mbona hata hoja za muhimu na za maana tunasikia tu wabunge wa upinzani? ina maana wa CCM wao ni kuunga kila kitu kinachopelekwa humo na mawaziri? Mbona nilimskia JK akiwaambia msikubali kila kinachopelekwa bungeni na serkali? Au PM ndiye anayewabana kwa matakwa yake binafsi? Siku za baadaye tutarithi au tutawarithisha nini watanzania miaka 15-30 iajayo!

Tutajenga tram, reli na uchumia wa tanzania kwa malia asili gani wakati huo? au hao wazungu wataendelea kutupatia misaada! au tutazidisha kodi kubwa kutoka kwa wananchi by then!

au hapa napo mnadai ushahidi? Haya ushahidi ukitolewa Bunge litafanya nini? Akukweti vipi wewe?!!
 
Mkwawa
Ili bunge limejaa mawaziri 70, wakuu wa mikoa na wakuu wa idara mbali mbali. All of them protect their Interests kwa MP na Akwikweti whatever his name is.
 
Mgodi wa Buhemba tangu mwanoni tuliskia hata Mkatababa hawakuingia na makaburu bali walipawa tu kuanza kuchimba , Akina former PM Sumaye anahusika sana. Cha ajabu hata maji ya Bwawa la Kyarano nalo ni kama Makuru walipewa. Ni kwa nini makaburu wasianzishe mradi wa kuvuta maji tka ziwa victoria ambalo liko km 30 toka Buhemba!

Iko siku wezi wa nchi hii wataangamizwa tu!. Wao wajifunze ni jinsi gani wezi wanavyotendewa na wananchi through mob justice. Hamtaiba milele na wanachi hawatakaa kimya milele.
Maoni yangu bajeti hii ya wizara ya madini na Nishati ingekuwa ya kwanza KUKATALIWA NA WABUNGE HASA WA KANDA YA ZIWA!!!!!!!!!

WOTE IKATAENI MPAKA IWEKE MIKATABA YOTE WAZI!!

HATA WABUNGE WA KANDA NYINGINE MKIKAA KIMYA NI UPUUZI KWA MAANA INAYOATHRITHIRIKA NI NCHI NZIMA. LAKINI MUNGU NI MKUBWA NI MKUBWA WEZI WATASHINDWA TU IT IS A MATTER OF TIME I TELL YOU!

http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/07/17/habari1.php
 
Ndugu Mkwawa, hili ni tatizo kubwa la taifa zima anagalia Mgodi wa almasi mwadui, IPTL, mererani.

Kamati ilundwa na Lowassa alisema mambo yaote yatawekwa wazi kuhusiana na ugomvi ulipo kati ya wachimbai wadogo na kampuni ya akina Masha (Naibu waziri ).


Usitegemee jipya leo huko Bungeni chini ya kiranja wao current PM.


Kama Bunge halina uwezo au meno juu ya mikataba eti ni sirikali kati ya serkali na wawekezaji je ni kwa nini Bajeti ya hiyo wizara isiptishewa na wawekezaji na serikali?

Mimi Mandela niliwaambia wawekezaji toka SA waje kuwekeza kwa lengo la manufaa kwa pande mbili na hasa kwa wanachi na siyo kikundi cha viongozi wenu waliokuwa na tamaa na utajiri! wa kulaumiwa siyo wawekezaji bali walaumuni viongozi wenu ambao wameweka mbele maslahi yao binafsi.

hii ni apartheid nyingine juu ya maslahi ya taifa yanayotokana na mali asili zenu!

Wala hamhitaji akina mandela wengi bali mmoja tu atakayeamua kusema ukweli na kutakataa haya maoni hata kama atawekwa ndani kwa miaka 27 kama mimi.
Lakini hatimaye apartheid iliisha.
 
Mkapa Mkapa! Bingwa bingwa! Mjuaji mjuaji ! aliwaita watu wanaohoji 3% kuwa ni hawajui walisemalo! aliyetuliza naye anasema nini??! watalaaniwa hao watu.Hivi kuwa rais wa NCHI maana ni kuwa "bingwa" wa kila fani?! na kuwa wewe ni Msomi na uelewa wako ni wa kwanza kuliko watanzania wengine wote?. Hii mentality ni MBAYA SANA! VIONGOZI WETU WANAPASWA KUITOA VICHWANI MWAO. Waliosaini mikataba hiyo kwa sasa ni sawa na yule jamaa aliyestaafu wizi na kusema kuwa sasa hivi wezi na majambzi hawana raha hela wanazopata wanazitumia kukimbia kimbia ili kuwakwepa police.

Wabunge wetu wa upinzani ongezeni bidii msikatishe tamaa na ukimya wa wabunge wetu wa CCM amabo wengi wao ni opportunists! Hivi Bunge lingelikuwa na wabunge wote wa CCM hapo ndipo baadhi yao wangekuwa na sauti?

Hao wachache akina Seleli et al. hongera sana!

http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/07/19/tahariri.php
 
Mkwawa said:
Mkapa Mkapa! Bingwa bingwa! Mjuaji mjuaji ! aliwaita watu.wanaohoji ..http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/07/19/tahariri.php
Nimefurahishwa na hii:
Freemedia said:
......Inasikitisha, na kwa kweli inakasirisha, kumsikia leo Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, akiunga mkono kupitiwa upya kwa mikataba ya madini!...
Swali langu kwake ni je nani aliipitisha na ilikuwa serikali ya nani??
Freemedia said:
......kwa mfano ya kuukodisha Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwa dola 1,000 kwa mwaka,!...
Sasa kuna huu ujinga mwingine hapa:
Majira.co.tz said:
......umeonesha kwamba IPTL, imekuwa inapewa ruzuku ya sh. bilioni 18 kila mwezi na fedha nyingine za mafuta sh. bilioni 3, na TANESCO imekuwa inakarabati mitambo ya kampuni hiyo, wakati si
kampuni ya Serikali...
http://majira.co.tz/kurasa.html?soma=tanzania&habariNamba=916
Freemedia said:
......Laana ya Tanzania ni nini? Je, si kweli kwamba laana ya Tanzania ni viongozi jeuri na wasioambilika? Kama kweli sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, basi sauti hii ya wabunge lazima iheshimiwe. Serikali ipeleke mikataba bungeni!...

What can i say?

Watu husema kuishi kwingi kuona mengi pia tembea uone na wajinga ndo waliwao!!
 
Haya!!! wanazichukua hela za madini kwa staili zote!!!

Mkapa jamani! hata wakaguzi ALIONA WATANZANIA HAWAWEZI!! NA ALAANIWE ZAIDI.

http://thisday.co.tz/News/583.html


US auditors take away 63.4% of total govt royalty earnings





SMALL-scale miners in Tanzania want the government’s ongoing review of exploitative contracts to include an international gold auditing firm hired to verify operations of large-scale miners.


The Federation of Miners Association of Tanzania (FEMATA), an organization with more than two million members, is questioning the government’s contract with Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation of the USA.

They question the rationale behind paying the auditing firm 1.9 per cent out of the 3 per cent royalty fees that the country earns from gold mining companies.

’’Under any circumstances, is there anywhere in the world where audit fees average 63.4 per cent of the value of the audited object or service as is the case with Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation and BoT?’’ they queried.

The government has paid Alex Stewart over $30 million (around 39bn/-) in just the past three years for its services ? having been contracted in 2003 to verify the cost of production, transportation of gold, and capital invested by large-scale miners.

Messrs Stewart Alex were contracted ostensibly following concerns that some of the major mining companies have been fiddling with figures to evade government taxes, but, small-scale miners are criticising the contract, saying it is just as exploitative as the mining contracts with the large-scale miners that Alex Stewart has been hired to audit.

In a recent letter to the Minister for Energy and Minerals, Dr Ibrahim Msabaha, FEMATA are also questioning the legality of the Bank of Tanzania (BoT) to enter directly into contract with the gold auditing firm on behalf of the government.

The federation argues that the firm should have entered into contract with the Tanzania Revenue Authority (TRA) which is charged with collecting government revenue, not the Central Bank.

The letter to the Minister for Energy and Minerals was also copied to the Prime Minister, the Attorney General, the Minister for Finance, the BoT Governor and the Minister of Planning, Economy and Empowerment.

FEMATA’s chairman, Mr Harry Lyimo, echoed sentiments of Members of Parliament who have been lamenting exploitative contracts in the mining sector, noting that despite its recent huge expansion, gold mining in Tanzania accounts for little more than 2% of GDP.

While commending President Jakaya Kikwete’s decision to evaluate mining contracts, the federation also wants the government to amend the 1998 Mining Act, which it claims inherently favours foreign corporations at the expense of local artisanal miners.

Mr Lyimo said apart from the need for better profit sharing arrangements and fuller accountability to the communities where mines are located, the firm contracted to audit the gold mines was an expensive burden to the country.

He also raised concern that the government intended to renew the contract of the gold auditing firm despite being a burden to the country.

However, the Deputy Minister for Energy and Minerals, Mr Lawrence Masha, dismissed suggestions that the government had extended the contract of the gold auditing firm. ’’These are just rumours ... the company’s contract runs until next year,’’ Mr Masha told THISDAY.

The assayers have been under contract with the Bank of Tanzania (BoT) since June 14, 2003, their mandate being to assess and determine actual investment and operational costs incurred by the big mining operators. These include costs of production and transfer of gold out of the country.

Tanzania is currently Africa’s largest gold producer after South Africa and Ghana. Gold mining operations grew by 27 per cent in 2004 against 17 per cent in 1999 -- only five short years before.
 
http://www.mwananchi.co.tz/mwananchisite/Mwananchi/Habari/Habari3.asp


Serikali yafunga mgodi wa dhahabu Musoma

Na Mathias Marwa, Musoma

SERIKALI imesitisha shughuli za uzalishaji wa dhahabu kwenye mgodi wa Buhemba Gold Mine (BGM) katika Kata ya Buhemba, Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara, kutokana na madini hayo kupungua katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya za Musoma Mjini na Vijijini, Saveli Maketa, aliwaeleza wafanyakazi 350 wa mgodi huo kuwa serikali imefikia uamuzi huo kutokana na sababu hiyo, lakini kuwahakikishia kuwa hakuna atakayefukuzwa kazi na wataendelea kulipwa mishahara yao kama kawaida.

"Serikali imetenga eneo lingine la kuchimba dhahabu baada ya dhahabu ya hapo kupungua, lakini hakuna mfanyakazi atakayefukuzwa na wote mtalipwa mishahara yenu kwa kipindi chote ambacho mtakuwa hamfanyi kazi," alisema.

Maketa aliwaeleza wafanyakazi hao kuwa mgodi huo wa Buhemba ni mali ya serikali pamoja na mali nyingine, ikiwamo mitambo yake na kwamba hata mishahara wanayolipwa ni ya serikali kupitia kwa mwekezaji kutoka Afrika Kusini.

"Mgodi, samani zote za ofisi, mali zote za hapa mgodini na mishahara yenu ni mali ya serikali ya Tanzania, hivyo ni mali zenu. Hao mnaowaita makaburu hawana chochote hapa bali wao ni mawakala tu wa serikali," alisema Maketa.

Alifafanua kuwa serikali haiwezi kumudu kukaa na wafanyakazi hao wote 350 wakati hakuna uzalishaji, hivyo utaratibu umepangwa wa kuwarejesha baadhi yao kwao ingawa wataendelea kulipwa mishahara yao na wengine watabaki katika eneo hilo kufukia mashimo, kusawazisha eneo hilo na kupanda miti ili kuhifadhi mazingira.

Alisema, wafanyakazi hao hawatapata malipo ya muda wa ziada kwa kuwa hakuna uzalishaji kwa sasa, ila baada ya uzalishaji mpya kuanza kwenye eneo jipya ambalo tayari limeishapangwa.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema pia kwamba serikali ina akiba maalum benki inayotokana na mapato ya mgodi huo ambayo iko chini ya Bodi ya Wadhamini wakiongozwa na Gavana wa Benki Kuu (BoT) na kwamba akiba hiyo ndiyo itakayotumika kuwalipa mishahara.

Akijibu maswali ya wafanyakazi hao, Maketa aliwaeleza kuwa serikali itatoa fedha kwa ajili ya eneo lingine jipya la mgodi huo katika eneo hilo la Buhemba, lakini itachukua takriban miezi saba kuanzia sasa.

Kwa mujibu wa DC, mgodi huo umewekeza kiasi cha Sh18 bilioni, ikiwamo mishahara ya wafanyakazi, mitambo na samani zote za ofisi.

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Ujenzi, Nishati na kazi nyinginezo (Tamico) kanda ya ziwa, Stephen Mageta, alisema pamoja na ujumbe mzuri wa DC kwa wafanyakazi hao, lakini wanataka serikali iwahakikishie kwa maandishi kuwa hawatawafukuza kazi na kwamba watalipwa mishahara yao wakati huo wa mpito.

"Wafanyakazi tulikuwa hatuamini kwamba mgodi huu ni mali yetu, sisi tunajua ni mali makaburu kutokana na unyanyasaji, vipigo tunavyopigwa, mishahara midogo na matusi juu," alisema Mwenyekiti wa Tamico tawi la Buhemba, Edward Ng'wenge.

Meneja wa mgodi huo, Jian Duvenage alikataa kuzungumza lolote na waandishi wa habari mgodini hapo na badala yake alimuomba DC aongee naye faragha.

Gazeti hili toleo la Novemba mosi, mwaka huu lilichapisha habari zikimkariri Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, akiutaka mgodi huo, pamoja na mambo mengine waonyeshe ankara zao na takwimu za mrahaba wanaolipa tangu waanze kuchimba dhahabu.

"Endapo BGM itapuuza, agizo hilo litaliwasilisha bungeni na nikishindwa nitakwenda kuwatetea wananchi mahakamani," alisema Mkono ambaye pia ni wakili.
 
Mijadala yenye tija kama hii siku hizi ni aghalabu sana kuzipata.... Toka mwaka 2006 mpaka leo halmashauri bado hawajaongezewa zaidi ya dola laki mbili...Regardless Barrick et al wanatengeneza faida ya kiasi gani....Stupidity ktk level iliyotukuka...
 
Back
Top Bottom