NHIF uonevu umezidi

Aug 27, 2010
10
0
Tunaandika tukitambua kwa kufanya hivi tunahatarisha ajira zetu, lakini tunasukuma tukiamini kuwa ustawi wa taifa unatangulia mbele ya ajiri zetu. Sisi ni wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(National Health Insurance Fund-NHIF) tunachukua hatua hii baada ya kuwa tumepoteza imani na watendaji wakuu wa wizara ya Afya, Bodi inayosimamia Mfuko, Uongozi wa Juu Mfuko chini ya Mkurugenzi Bwana Emmanuel Dotto Bundala Humba ambao ndie kiini na mhimili wa ufisadi katika mfuko.

Baada ya kuwa tumejitahidi kuwasalisha hoja zetu kwa kufuata mikondo inayoeleweka pasipo hatua zozote kuchukuliwa tunalazimika leo kuwasilisha kwenu tukitambua juhudi zenu adhimu na za kizalendo katika kulisafisha taifa dhidi ya makucha yetu. Kwa msukumo huo tunawasilisha rasmi hoja zetu kwa viongozi wa CHADEMA kama taasisi pekee yenye dhamira sahihi katika kulisafisha taifa(hapa tunatambua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ndio mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kusimamia mahesabu ya Mashirika ya umma) pamoja na magezeti ya Mwanahalisi na Tanzania Daima ambayo kwa mtazamo wetu ndio magazeti pekee yenye ujasiri wa kutosha katika kuanika uozo katika jamii na taasisi za umma. Pia Tovoti ya Jambo Forum ambayo inaendelea kutoa mchango mkubwa kwa taifa katika vita dhidi ya ufisadi na ujenzi wa demokrasia nchini. Tunatanguliza shukran zetu kwa hatua mtakazo zichukua katika hili.

1. Mgongano wa Kimaslahi na “Hongo” kwa viongozi wa Bodi na Wizara ya Afya
Bwana Humba ni mjanja na mwepesi katika kuweka mitego kwa viongozi wanaopaswa kusimamia utendaji wake. Uongozi wa Bodi uliopita uliwahi kupokea malalamiko ya wafanyakazi juu ya “ukatili” na Minenendo mibaya ya bwana Humba. Bodi iliamua kuunda tume ya uchunguzi chini ya mwenyekiti wa bodi wakati huo Professa Msimbichaka na Makamu wake ndugu Rutazamba.

Kamati hii iliibua matumaini kwa wagfanyakazi wakijua hatimae kilio chao kitasikika. Ghafla bwana Humba aliamua kuambatana na Mwenyekiti wa Bodi kwenda china kuhudhuria mkutano. Waliporudi kamati ya uchunguzi ilikufa na Bwana Humba akanza kutoa vitisho kwa wafanyakazi kwamba alipokuwa China alielezwa na mwenyekiti wa Bodi(Professa Msimbichaka) kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi akiwaondoa “atafanikiwa” sana katika shughuli zake.

Pia aliendeleza tabia ya kutoa upendeleo kwa mwenyekiti wa bodi katka kuhakikisha yote anayopanga yanapitishwa na bodi. Kuna kipindi alilazimisha mfuko kulipa gharama za matibabu ya ndugu wa mwenyekiti wa bodi iliyomaliza mda wake(Professa Msimbichaka) aliekuwa ametibiwa katika hospitali ya St. Bernard iliyopo Kariakoo ihali tayari mkataba ulikuwa umevunjwa baina ya mfuko na hospitali hiyo. “Upendeleo” wa aina hii hudhoofisha sana uwezo wa kiutendaji wa bodi.

Bwana Humba amendeleza utamaduni mbaya wa “kununua” viongozi wa Bodi na tayari mwenyekiti mpya wa bodi amaenasa katika mtego kwani binti yake ameajiriwa katika mfuko huu jambo ambalo linadhibiti uwezo wake wa kusimamia utendaji wa mkurugenzi na wa shirika kwa maana anajaribu kulinda fadhila aliyopewa kwa mtoto wake kupewa ajira.

Kama vile haitoshi mtoto wa kaka yake na katibu wa wizara ya afya nae ameajiriwa katika mfuko huu. Itakumbukwa kuwa katibu mkuu wa afya kwa wadhifa wake alikuwa ni mjumbe mwenye ushwawishi mkubwa katika bodi ya mfuko wa bima ya afya. Kwa sasa mjumbe wa bodi toka wizara ya afya ni mkurugenzi wa mipnago wa wizara hiyo ambae kimlaka yupo chini ya katibu mkuu wa widhara na baadhi ya mikutano katibu huudhuria, hali hii inamuhakikishiwa “ulinzi” bwana Humba katika wizara ya afya.

2.Kupindisha taratibu maksudi kwa maslahi Binafsi​

Mara nyingi bwana Humba amekuwa akikataa kuudhinisha malipo kwa wafanyakazi pale wanapokuwa wamepata matibabu katika vituo vya afya ua hopsitali ambazo hazijasaliwa na mfuko kwa maelezo kuwa ni nje ya utaratibu. Jambo la kushangaza ni kuwa mara mke wa wa Mkurugenzi alipopata matitizo ya mguu, alilazwa MOI(kitengo cha mifupa Muhimbili) wakati ambapo MOI hajaingia mkataba na Mfuko. Mfuko ulilipa kiasi kikubwa cha fedha kugharamia matibabu ya mke wa mkurugenzi.

Cha ajabu zaidi ni kuwa hivi majuzi mke wa mkurugenzi alipelekwa India kwa ajili ya matibabu na kugharamiwa na Mfuko. Safari hii iligharimu Mfuko kiasi cha shilingi 25,764,000. Itakumbukwa kuwa Mfuko haujaanza kugharamia matibabu nje ya nchi, mkurugenzi kwa kujitetea alisema kwamba ampewa kibali na wizara ya afya!

Cha kujiuliza ni wanachama wangapi wa mfuko wanapata fadhila hizi? Ikubukwe kuwa sehemu kubwa ya wanachama wa mfuko na wanchangiaji wakubwa ni walimu je wao wanaweza kupelekwa nje kwa matibabu? Cha kusikitisha ni kuwa haya yanatokea wakati ambapo raisi wa chama cha walimu ni mjumbe wa bodi.

Pia katika maonyesho ya sabasaba jumla ya shilingi 23,033,000 zilitoweka, yani haizkutolea maelezo yoyote katika ripoti. “Uwizi” huu ulifanyika chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Sabasaba Bwana Raphael Mwamoto. Rafiki mkubwa wa Mkurugenzi. Uwizi huu ulibainishwa na mkaguzi wa ndani lakini habari zilipofikishwa kwa mkurugenzi hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Utendaji wa bwana Mwamoto ni wa kutilia shaka tangu alipoajiriwa katika mazingira ya kutatanisha. Hakuweza kufaulu katika kipindi cha majaribio(Propabation) lakini katika hali ya kustaabisha mkurugenzi aliaamua kumbadilisha idara. Bwana Mwamoto alikuwa mwalimu katika chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM) kabla ya kuletwa na mkurugenzi katika mfuko wa bima ya afya, inasemekana hajaacha rekodi nzuri IFM. Mara nyingi wafanyakazi wanapojaribu kumchunguza na kumuwajibishwa hutishiwa kwa maelezo kuwa yeye ni afisa wa usalama wa taifa!

3.Ufujaji wa fedha​

Kiasi kikubwa cha fedha huwa kinapotea katika miradi mbalimbali ya shirika. Uwizi mkubwa upo katika kununua mfumo wa PREMIA ambao ulipaswa kubuniwa katika kusaidia uharakishaji wa malipo ya madai. Mfumo huu ulinunuliwa India. katika mkataba ulionekana utagharimu dola za kimerekani laki nne(400,000), hii ilikuwa mwaka 2005. Lakini cha kushangaza zimetumika zaidi ya shilingi milioni 700 katika manunuzi na mpaka leo mfumo huu(sytem) bado haujaanza kufanya kazi mpaka sasa. Ukipita katika ofisi za kanda utakuta wanatumia mfumo wa kawaida kulipa mahospitali.

Gharama za jumla za kuleta mfumo huu hewa zinazidi Bilioni moja ukujumlisha gharama za maandalizi, kuzunguka mikoani kutoa elimu kwa watoa huduma, matangazo katika vyombo vya habari na uzinduzi uliofanywa kwa kishindo kwa kuwakaribisha viongozi kutoka wizara ya Afya.

Cha kujiulizwa ni kwanini bodi inashindwa kuwawajibisha viongozi wa shirika kwa hasara kubwa kama hii? Uwizi huu unatokea ihali kuna malamiko makubwa toka kwa wanachama juu ya huduma mbaya za Mfuko. Hii ni sehemu ndogo tu ya ufisadi katika Mfuko wa bima ya Afya. Uchunguzi toka taasisi huru unaeweza kuibua mengi sana katika maeneo ya fedha, ukiukwaji wa taratibu na ajira holela zizizofuata taratibu za ajira.

4. Huduma Mbovu za Mfuko​

Uongozi wa sasa wa Mfuko umeshindwa kabisa kubuni mikakati ya kuimarisha huduma kwa wateja wake. Mfano sehemu kubwa ya wanachama wa mfuko huu ni walimu, wanapokwenda katika mahospitali au vituo vya afya katika maeneo yao na kukosa dawa, hulazimika kutumia fedha zao kununua dawa na Mfuko hukataa kuwafidia ghrama za mananuzi ya dawa ihali kila mwezi hukatwa katika mishahara yao kwa ajili ya mfuko. Haya yanatokea wakati Mfuko umekuwa mwepesi katika kutoa michango mikubwa katika shughulizi za hisani kama michezo!

Pia Kuna usumbufu mkubwa sana katika kutengeneza vitambulisho vya wanachama. Uongozi wa Humba hujitetea kuwa wao bado ni wachanga, yaani ni miaka saba ya uchanga! Itachukua miaka mingapi kwa Mfuko huu kukua chini ya uongozi wa Mfuko huu?

Katika hali ya kukosa mwelekeo ya kiongozi Mkurugenzi amaahaidi kujenga Hospitali Dodoma na Dar es salaam kwa kile anachokiita “centre of execelence”. Pia Mfuko umetoa shilingi milioni 225 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya amana na mwananyamala! Hizi “centre of execelence” wanamjengea nani wakati wanachama wa Mfuko wako vijijini? Haya yanatokea wakati Raisi wa chama cha Walimu(CWT) bwana Mukoba na mwakilishi wa wafanyakazi wa serekali (TUGHE) bwana kiwenge ni wakumbe wa bodi! Ni kwanini wanashindwa kutetea maslahi ya wale wanaowawakilisha? Wanapumbambazwa na nini?

Kuna hitaji la lazima kuchukua hatua za haraka katika kuunusuru mfuku muhimu katika ustwi wa wafanyakazi. Tutaendelea kuwataarifu zaidi juu ya ufisadi unaoendelea katika taasisi hii muhimu katika ustawi wa wananchi hasa wenye kioato kidigo.

5.Dharau na Mienendo isiyokubalika katika jamii​

Mkurugenzi mkuu wa bima ya Afya moja ya Taasisi nyeti sana nchini ni mtu mwenye tabia ya majigambo, vitisho na dharahau. Mwenendo wake huu amewahi kuudhihirisha nje ya ofisi na kuupa fursa umma kutambua tabia halisi ya kiongozi mkuu wa shirika muhimu katika taifa. Itakumbukwa amewahi kumtukana na kumnyanyapaa nesi mmoja wa hospitali ya Hindu mandal(sasa marehemu) aliekuwa muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI. Alifanya hivyo baada ya kuwa amekataliwa kupewa huduma kupitia mfuko wa bima ya afya kwa kuwa hakwenda na kitambulisho chake. Huu ni utaratibu wa kawaida katika uendeshaji wa mfuko.

Marehemu kwa kutambua muongozo na taratibu za mfuko alimkatalia mkurugenzi kwa kuwa alikuwa amekiuka utaratibu, mkurugenzi alijaribu kumtisha kwa kutumia wadhifa wake na kwamba atahakikisha anafukuzwa kazi, baada ya marehemu kuwa na msimamo pamoja na vitisho vya mkurugezi ndipo bwana Humba alipoanza kutukana matusi na kumskashifu marehemu kutokana na hali yale ya kiafya hali iliyopelekea marehemu kupata shinikizo liliochukua maisha yake masaa machache badae. Habari hii iliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari lakini ghafla ikapotea katika namna ya kushangaza. Upo uwezekano alihonga ndungu wa marehemu na baadhi ya vyombo vya habari ili kudhibiti taarifa zaidi kutoka na pengine kuchukuliwa hatua za kisheria. Kadhia kama hizi sehemu ya kazi kwa wafanyakazi wa NHIF. Hatuamini kama hizi ni tabia stahili kwa mtu mwenye dhamana ya kuongoza shirika la bima ya Afya nchini.
 
Rushwa kivipi? Hapo umeongea kiudaku, ongea kiproo twende sawa. Hata mimi nachukia rushwa kinoma kwa sababu sijawahi kupewa
 
ni kati ya wale wanaolipwa mamilion kutokana na michango yetu? yafaa atumbuliwe akaoneshe majigambo kwa mkewe!
 
Hi nchi si yawatu fulan mbona wanajisahau sana pale kila mtu mwenye sifa anatakiwa kuhudumia sasa wao wanafikili ni shilika la familia ama koo fulan.
 
Naomba leo niulize tena, baada ya aliyekuwa mkurugenzi wa NHIF Emmanuel Humba kutumbuliwa ni nani aliyepewa dhamana ya kuliendesha hili shirika letu? Nani mkurugenzi mkuu wa mfuko kwa sasa?
 
Back
Top Bottom