Elections 2010 Nguvu Zaidi, Ari Zaidi na Kasi zaidi - Nipeni Nafasi

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Miaka mitano ya awali nilikuwa najifunza na kupata uzoefu wa urais, Naombeni mnipe nafasi tena ya miaka mitano 2010-5 tuweze sukuma gurudumu la maendeleo. Wenyewe mnaona foleni zimeongezeka hapa mjini maana yake magari yamekuwa mengi. Hii yote ni dalili za maisha bora kwa kila Mtanzania.

Suala la Madini tumeongeza kodi ya Mrahaba, Muungano nimshughulikia na muafaka na CUF kule visiwani umefikiwa na tupo kwenye kuunda serikali ya pamoja.

Rais+Kikwete.jpg

Suala la ufisadi na nyie wenyewe mnajua kuna kesi kule mahakamani, sasa serikali haiwezi ingilia kuona kama zinacheleweshwa ama ni utaratibu.

Wafanyakazi mnajua nimeongozea mishahara yenu! Suala la Mbayuwayu na Kibong'ota ulikuwa ni utani kwangu na rafiki yangu bwana Mgaya. Wafanyakazi ninahitaji kura zetu ili tupate ushindi wa Sunami.

Upande wa pili

attachment.php

Hapa mgonjwa ndio anapata bed-rest !!!!!!!!!

Zahanati hii ipo ndani ya nchi yetu pendwa Tanzania yenye AMANI na utajiri mkubwa wa kila kitu. Mtanzania mwenzangu, Madhara ya kuchagua Rais na Mbunge baada ya kupewa t-shirt na chumvi, Ni makubwa zaidi, usichague sura wala mtu muongo! Kataa Kataaaa

Kura yangu hapati mkwere Mwenzangu!
·
 
Jibu ni moja tu mwambieni safari hii HATUDANGANYIKI Mgaya keshamaliza kazi.
 
kweli picha na hotuba vinaendana, tutafanya judgement 31/october
 
kufanana majina nako kubaya inawezekana watu walijua kila jeikei ni vilevile wakasahau kuwa kumbe hata fataki ni jina tu.
MJOMBA ANAPATA TABU HUKO ALIKO,HUKU KUFANANA MAJINA NAKO !
 
Nimeangalia hiyo picha ya Hospital na kitanda cha Mgonjwa nimetamani kulia! I m so touched huyo anaweza kuwa ni bibi yangu ama shangazi yangu kule Imaranguzu ama Igembesabo kijijini. Mtoto wa Mkulima waziri Mkuu akipata mafua anapanda ndege anaenda chekiwa UK.

Mungu saidia hili taifa, liwe na uongozi wenye kujali wananchi wake.

Mchungaji Masa
 
Rev,Masa usije shangaa kuwa watu wanaolala kwenye hivyo vitanda ndiyo hao wa kwanza kukatika na kukata viuno kushangilia CCM. Mimi nakubariana na mtu mmoja aliyesema inabidi tujichunguze kuna mdudu gani nchi hii. Mtu ambaye mlo mmoja kwake kazi, matibabu ovyo, hana maji ya bomba, Umeme ni ndoto na kifo kiko njiani muda wowote na ndiyo washabiki wa kwanza.
 
Ila watu kwa mbali wameanza kujua kweli hawadanganyiki! Kushindwa kwa Mzee Malecela kumeashiria mengi sana.......sema wizi wa hawa CCM kuna sehemu najua huwa hawashindi ila wanaiba tu!

Rev Masa in Texas
 
Inabidi CHADEMA wawe na clips za aina hii kwenye kampeni zinazoonyesha upande wa STAREHE za watawala na DHIKI za wananchi ili wapigakura waelewe jinsi nchi inavyoliwa wakati wananchi wanateseka! Pia magwanda ya kijani na T-shirts pamoja na caps tunazoziona ni mali ya wizi mtupuuuu!
 
Dah, hiyo hospitali si bora wangetandika chini wakalala jamani!!

Na huyu mtu wenu, hiyo miaka mitani alikuwa anajifunza nini?? Five good years ya kujifunza?? WTF...:mad2:
 
tumpeni jamani ajaribu tena kwani tunajifunza kutokana na makosa azu hamjuiwajameni????
maisha bora hayaji kwa miaka mitano tumpe nafasi atekeleze ahadi yake hiyo tukufu.
Miaka mitano ya awali nilikuwa najifunza na kupata uzoefu wa urais, Naombeni mnipe nafasi tena ya miaka mitano 2010-5 tuweze sukuma gurudumu la maendeleo. Wenyewe mnaona foleni zimeongezeka hapa mjini maana yake magari yamekuwa mengi. Hii yote ni dalili za maisha bora kwa kila Mtanzania.

Suala la Madini tumeongeza kodi ya Mrahaba, Muungano nimshughulikia na muafaka na CUF kule visiwani umefikiwa na tupo kwenye kuunda serikali ya pamoja.

Rais+Kikwete.jpg

Suala la ufisadi na nyie wenyewe mnajua kuna kesi kule mahakamani, sasa serikali haiwezi ingilia kuona kama zinacheleweshwa ama ni utaratibu.

Wafanyakazi mnajua nimeongozea mishahara yenu! Suala la Mbayuwayu na Kibong'ota ulikuwa ni utani kwangu na rafiki yangu bwana Mgaya. Wafanyakazi ninahitaji kura zetu ili tupate ushindi wa Sunami.

Upande wa pili

attachment.php

Hapa mgonjwa ndio anapata bed-rest !!!!!!!!!

Zahanati hii ipo ndani ya nchi yetu pendwa Tanzania yenye AMANI na utajiri mkubwa wa kila kitu. Mtanzania mwenzangu, Madhara ya kuchagua Rais na Mbunge baada ya kupewa t-shirt na chumvi, Ni makubwa zaidi, usichague sura wala mtu muongo! Kataa Kataaaa

Kura yangu hapati mkwere Mwenzangu!
·
 
DUH!!KAAAAAAZI KWELIKWELI>INGEKUWA MIMI NDO jk WALA SINGETHUBUTU KUGOMBEA TENA.
 
Miaka mitano ya mwanzo imekuwa disastrous. Unataka mitano mingine ili...? Hatutaki uendelee kufanya majaribio ya uongozi kwenye nchi yetu.
 
Dah, hiyo hospitali si bora wangetandika chini wakalala jamani!!

Na huyu mtu wenu, hiyo miaka mitani alikuwa anajifunza nini?? Five good years ya kujifunza?? WTF...:mad2:

It was a five years of training to have doctorate, si unaona mwenyewe kapata udocta. Wananchi wengi hawana elimu, hawawezi kupambanua mambo kwa upana. Time for change, the change we can believe in it.
 
Very sad, nimetoka sasa hivi kusoma orodha ya Nchi Maskini sana Duniani. Tanzania ni ya Tano, Uganda na Kenya zimetuacha mbali..Watanzania tufanye Badadiliko Mwaka huu ili na sisi tunufaike na 'BAADA YA DHIKI FARAJA' kwa kuwa sasa hivi kwa watanzania 'BAADA YA DHIKI NI DHIKI KUU'
 
:mad2:MSANII HAWEZI KULETA MAISHA BORA MURA,KASI NI VECTOR QUANTITY NA LAZIMA IWE NA DIRECTION HIVYO KASI MPYA YA KIKWETE ILIKUWA NI KURUDI NYUMA
 
Ile slogan ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" imepotelea wapi? Au wamegundua haiwezekani tena chini ya utawala wa thithiemu??????????
 
Back
Top Bottom