Elections 2010 Nguvu ya Dr.Slaa Mwanza kumpeleka Kikwete tena Mwanza?

slaa_mwanza.jpg

Mwafrika
 
habari za kuaminika nilizozipata hivi punde kutoka kwa mdau huko mwanza ni kuwa umati aliokusanya dr.slaa leo huko mwanza haujapata kutokea na imemlazimu jk kwenda mwanza tena kesho..

Naagiza vijana wanitumie picha niweke hapa

kikubwa ninachoweza kuwaasa ni kuwa kura za safari hii ni lazima watanzania tujitoe kuzilinda, kama tukiachia suala la kulinda kura kwa vijana ambao hawana uzoefu na bureaucracy ya kiserikali na vyombo vya dola. Vijana ambao hawana uwez wa kujibishana na makamanda wa polisi pindi watakapotaka kungiza kura za wizi, n.k tujue kuwa tumekwisha.

Dr slaa na chadema wamekamilisha wajibu wao kulingana na mazingira yaliyopo kikataba, kisheria n.k, kilichobaki ni sisi wananchi ni sisi wananchi kutimiza wajibu wetu wa kupiga kura na kuhakikisha kuwa hakuna mamabo yanayokiuka maadili yatakayotokea siku hiyo katika mchakatomzima wa kupiga, kuhesabu, kutangazwa kwa kura n.k

itakuwa upuuzi kusubiri hadi matokeo yatangazwe ndipo tujitokeze kupinga, hatua kama hizo ni sawa na kudhamiria kuharibu nchi yetu.

Mtanzania kamili mwenye nia njema ajitokeze sasa kuhakikisha kuwa hakuna ukiukwaji wa maadili ukalofanyika. Ikiwa serikali ijayo itatokana na ukiukwaji wa maadili ni lazima mafisadi wataneemeka na watanzania walio wengi kuumia kama ilivyo sasxa.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Habari za kuaminika nilizozipata hivi punde kutoka kwa mdau huko Mwanza ni kuwa umati aliokusanya Dr.Slaa leo huko Mwanza haujapata kutokea na imemlazimu JK kwenda Mwanza tena kesho..

Naagiza vijana wanitumie picha niweke hapa
JK anaenda kuwaongezea ahadi nyingine nini watu wa Mwanza, zile alizowapa kwanza hazikutosha. Nilicheka pale Kinana alipokuwa akihojiwa kuhusu utafiti wa Synovete naye akasema ni kutokana na ahadi nzuri anazotoa mgombea wao, akaitaja ile mikoa ambayo mgombea wao hajafika bado na kuwa akifika huko na kuwapa ahadi zao kura zitazidi kuongezeka. Unajua wakati mwingine nashawishika kuwaona hawa wenzetu wametufanya mazezeta, na kwamba wakitudanganya kwa ahadi basi tunaridhika. Sasa waone joto ya jiwe, na bado watachanganyikiwa wao safari hii. Wacha waongeze ahadi mpaka zifike mbinguni, safari hii Mwanza haitakuwa Amsterdam tena itakuwa Toronto.
 
Mkuu amini nakwambia. halitasalia jiwe juu ya jiwe. so as hatasalia fisadi juu ya fisadi.
Nimeipenda hii ya Mwanza kuwa Toronto. Hivi wasukuma wanaifahamu hiyo toronto wasije wakajenga picha ya talanta

yaaani mi najiandaaa kucheka kama kweli habari hizi na ataenda mwanza kesho ntacheka sana.maana najua Mwanza ndo alikoanzia kampeni baada ya kuanguka pale Jangwani..Aiseeeeee
ccm kwa ukabila ni noma. walishajipangia mikoa ya reserve ya kura na inapotokea mikoa hiyo ikatikiswa, inakuwa ngumu kweli kuiacha ipotee.
Jamani sijamwona kaimu Rais, PINDA akimpiga tafu bosi wake.
Mwaka huu vululu vululu
Mkuu ukicheka mie ntavunja mbavu zangu mbili tatu hivi
 
View attachment 15568
Naomba atakayeweza aikuze hiyo picha.

Jamani si mlisema uwanja waliopewa ulikuwa ni mdogo sana. Ina maana hapa sasa wamefanyia kwenye uwanja gani? Walikubaliwa kufanyia mkutano uwanja wa Furahisha au imekuwaje? Maana sasa huo umati, nafikiri hata ingekuwa kirumba bado isingetosha. Hii ni hatari kubwa bandugu. Mungu akutangulie Slaa katika mapambano haya.
 
Duh, hapa hata ungekuwa uwanja mpya wa taifa wa Dar es salaam yumkini usingetosha. Halafu hao ndo wamepigwa mabomu ya machozi, hawajapewa khanga wala tshirt na wala hawakuletwa na malori. Nawatamani watanzania wa kizazi hiki.
 
Tbc hawajajua mpaka sasa bosi wao mpya ni nani, naona wanacheza cheza tu. Nguvu ya umma, itatoa maamuzi muda si mrefu
 
Ule Umati wa Mwanza sio mchezo.. lazma jamaa achanganyikiwe, pamoja na kuwapiga mabomu lakin watu wakajaa mbaya
 
Duh, hapa hata ungekuwa uwanja mpya wa taifa wa Dar es salaam yumkini usingetosha. Halafu hao ndo wamepigwa mabomu ya machozi, hawajapewa khanga wala tshirt na wala hawakuletwa na malori. Nawatamani watanzania wa kizazi hiki.

Ndugu zangu Watanzania wana kiu ya mabadiliko na wamekwisha amua kufanya hivyo. Sasa kazi iliyopo ni kuwahamasisha kulinda kura ili kuhakikisha kuwa kura za Dr. Slaa hazitangazwi kuwa ndizo za Kikwete. Hii inatokana na imani yao kuwa mtu wa maana katika uchaguzi si mpiga kura au mhesabu kura bali mtangaza matokeo kama Kivuitu. Hapo ndio lazima kuhakikisha kuwa Makame na Kiraivu hawageuzi matokeo imani yetu ni ndogo sana kwao na kwa kweli haipo.
 
Umati wa kawaida kabisa huu, mbaya zaidi wengi wao sio wapiga kura!
Kibs usije ukawa kama yule msemaji wa Serikali ya Sadam Hussein, Al Sahaf (??). Majeshi ya marekani yanaingia na kutwaa Baghdad yeye anasema majeshi yetu ya Iraq yako imara kulinda mji mkuu!! Kaa benchi!
 
Kama wapiga kura au sio hilo sio jukumu lako.. maana we sio tume ya uchaguzi'
Tusubir tarehe 31 muone km hatutapiga kura this time around.. Hapa mpaka kieleweke'
 
Umati wa kawaida kabisa huu, mbaya zaidi wengi wao sio wapiga kura!

Unasema ni wa kawaida kwani mko tayari kuuiba kura bila kuheshimu matakwa ya Watanzania. Kama mlivyomuibia Mrema mwaka 1995 ndio sasa mnataka kutuzuga kuwa hao si wapiga kura. Nakwambia hao ni wapiga kura sema kuwa CCM, NEC, UWT na wezi wa kura wa Teknohama wanataka kuiba hizo kura na kutuambia hao wote walimpigia Kikwete badala ya Dr. Slaa kama alivyofanya Kivuitu huko Kenya. Mwaka huu mmeshindwa. Kama Dr. Slaa alivyosema mpeni Kikwete habari sahihi asije akaanguka chini kwa shinikizo pale atakapoambiwa ameshindwa.
 
Kibs usije ukawa kama yule msemaji wa Serikali ya Sadam Hussein, Al Sahaf (??). Majeshi ya marekani yanaingia na kutwaa Baghdad yeye anasema majeshi yetu ya Iraq yako imara kulinda mji mkuu!! Kaa benchi!

Sikujua hata hapa JF wanachakachua picha, kila ninayofungua haifunguki, inakuwaje? loh
 
Nimeipenda hii ya Mwanza kuwa Toronto. Dar je? Nadhani hii itakuwa Los Angeles. All in 5 years. And all if we choose Kikwete. Kishasahau ahadi za 2005.
 
Back
Top Bottom