Nguvu ya CHADEMA yawatisha Polisi

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
• ASKARI WASHANGAZWA NA NGUVU ILIYOTUMIKA

na Mwandishi wetu

NGUVU ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika mikutano ya hadhara na maandamano inayofanya mara kwa mara hivi sasa yaelekea kutishia uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiasi cha kulazimika kuvitumia vyombo vya dola kuidhibiti, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.

Miongoni mwa mbinu hizo ni kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano yaliyopangwa kufanywa kwa siku 10 kuanzia jana katika Mkoa wa Morogoro kwa kulitumia Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi lilizuia mikutano hiyo na maandamano ya CHADEMA kwa madai kadhaa yakiwamo uchache wa askari, sherehe za Sikukuu ya wakulima (Nanenane), mgomo wa walimu uliozuiwa siku tatu zilizopita na maeneo husika kutumiwa na CCM katika mikutano ya hadhara.

Kinyume cha kauli ya Jeshi la Polisi mkoani humo kuwa lina uchache wa askari, jana idadi kubwa ilionekana ikijiandaa kukabiliana na maandamano na mikutano ya CHADEMA kama ingefanyika.

Baadhi ya askari waliowekwa tayari kukabiliana na CHADEMA, walieleza kushangazwa kwao na nguvu kubwa iliyotumika kuwazuia CHADEMA badala ya nguvu hiyo ingeelekezwa kuwalinda.

Polisi wapigwa jua

Taarifa kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa askari kutoka katika mikoa ya Iringa, Dar es Salaam na Dodoma waliokusanyika mkoani humo kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kukabiliana na mikutano ya CHADEMA kama ingefanyika hiyo jana, walijikuta wakishinda juani bila kazi.

Kushinda juani huko kwa askari hao kunatokana na uamuzi wa viongozi wa CHADEMA kuamua kusitisha maandamano na mikutano hiyo hadi Agosti 8, mwaka huu ambapo itaanzia katika eneo la Mikumi (Kilosa).

Baadhi ya askari waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa sharti la kuhifadhiwa majina yao walisema kwa namna ulinzi ulivyoimarishwa isingekuwa rahisi kwa maandamano na mikutano ya CHADEMA kufanyika.

"Logic (mantiki) iko wapi kama nguvu hii iliyoandaliwa kwa ajili ya kuyazuia maandamano ya CHADEMA ingetumika kuyalinda, si kila kitu kingekuwa sawa na yangeenda vizuri tu, sijui ni wapi tunaelekea katika hali hii," alisema mmoja wa askari.

Alisema kimsingi wao kama askari wa ngazi ya chini hawana tatizo na CHADEMA isipokuwa wanalazimika kupokea amri kwa kuwa ndiyo kazi waliyochagua kufanya na kusema kama watendaji wa serikali hawataacha siasa katika kazi kuna hatari ya kuipeleka nchi pabaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alipoulizwa kuhusu hali hiyo alikiri kuwapo kwa askari wengi mkoani Morogoro na kusema ni gharama zimetumika licha ya kukataa kutaja maeneo waliyotoka.

Kuhusu askari wa ngazi ya chini kulaani maandalizi makubwa ya kuzuia mikutano ya CHADEMA badala ya kulinda, Kamanda Shilogile alisema hakuna askari anayeweza kutamka kauli hiyo na kwamba hawatumiki kwa masilahi ya kisiasa.

"Unaniuliza askari wametoka wapi, hilo si swali la msingi, wewe jua gharama zimetumika kwa ajili ya suala hili na huku kusema askari wamesikitishwa na maandalizi ya kuzuia mikutano badala ya kuilinda mbona hawajaniuliza mimi? Hiyo ni wewe mwandishi umetengeneza stori," alisema Shilogile

CHADEMA yasogeza mbele Sangara

Uongozi wa CHADEMA jana ulitangaza kusogeza mbele mikutano yake na maandamano hayo (Operesheni Sangara) ili kuepuka maafa ambayo yangeweza kutokea baina ya wafuasi wake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro iliyozuia operesheni hiyo.

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, walisema zuio hilo la polisi limelenga kukisaidia chama tawala (CCM) ambayo hivi sasa ina hali mbaya kiutawala.

Mbowe alisema CCM imetishwa na matokeo ya ziara za CHADEMA zilizofanyika hivi karibuni katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mbowe alisema baada ya ziara ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa na mafanikio makubwa wabunge wa CCM walitishika kwa kiasi kikubwa hata kufikia baadhi yao kuomba mikutano hiyo ipigwe marufuku ili isiwaondolee uhalali wa kuitwa wabunge licha ya kuzembea katika majukumu yao.

"Tunapaswa kujua kuwa haya ni mapambano baina ya haki na batili, siku zote dhalimu hawezi akaruhusu kirahisi kuondolewa katika udhalimu wake…na atatumia njia mbali mbali ya kujihalalisha, kwa hiyo katika hili tunapaswa kuwa wavumilivu na wenye busara ya hali ya juu katika kukabiliana nao," alisema Mbowe.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kutambua kuwa kuminya haki za msingi za wananchi kwa manufaa ya wachache ni suala lisiloweza kukubalika mbele ya jamii na kwamba hali hiyo ya kuchagua watu wa kuwatumikia itasababisha watu kujenga usugu dhidi ya jeshi hilo.

Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu na Jeshi la Polisi walikubaliana kuahirisha uzinduzi wa ziara hiyo iliyokuwa ifanyike jana na badala yake itafanyika Agosti 8, katika Jimbo la Mikumi na kufuatiwa na ratiba nyingine ya mikutano katika Mkoa wa Morogoro.

"Jana (juzi) hatukulala tulikuwa katika mawasiliano na Jeshi la Polisi hata kufikia IGP kushindwa kupokea simu yangu, mwenyekiti alimtafuta na amempata leo asubuhi (jana), tumemfahamisha hoja zetu na mapendekezo yetu naye akatushauri turudi kwa RPC wa Morogoro kwa ajili ya mapendekezo hayo," alisema.

Alibainisha kuwa katika mapendekezo yao ni pamoja na kumueleza kuwa hoja ya CCM kufanya mikutano pamoja na CHADEMA haina nguvu, kwa kuwa CCM waliomba kwa ajili ya Agosti 4, mwaka huu tu, na maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro yanafikia kilele Agosti 8, mwaka huu na mgomo wa walimu umesitishwa na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.

Alisema Jeshi la Polisi linapaswa kufahamu dhana ya siasa ya vyama vingi ni kutoa uhuru wa wananchi kuchagua sehemu ya kwenda hivyo kuweka visingizio kuwa kuna mikutano miwili katika wilaya moja ni kuua demokrasia.

Aidha, Dk. Slaa aliongeza kuwa hata kitendo cha jeshi hilo kuchukua magari kutoka sehemu tofauti za nchi kwa ajili ya kuwadhibiti CHADEMA mkoani Morogoro ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma na badala yake gharama zilizotumiwa zingeweza kusaidia kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi wa jeshi hilo.

"Tunaionya serikali hii iwe mara ya mwisho na tumekubali hivi kwa sababu sisi si watu wa fujo, ila hatutaweza kuvumilia hasara ya namna hii, kwa kuwa hizi fedha tunazotumia ni za ruzuku zinazotolewa na serikali kwa vyama, sasa hasara hii iweje wabebeshwe wananchi kizembe zembe kwa ajili ya kuminya demokrasia?" alihoji.

Alisema Jeshi la Polisi linatumia sheria zilizowekwa na wakoloni katika kuendesha nchi huku likifahamu fika wakoloni walitumia fursa hiyo kwa ajili ya kuwaminya wapigania uhuru.

"Katika PGO ya Polisi ni mambo machache ndiyo yameboreshwa na zilizobaki ni zile za kikoloni, hivyo watambue sasa ni wakati wa siasa huru na si vita baina ya wenye nchi na wakoloni katika kudai uhuru," aliongeza Dk. Slaa.

Agosti mosi, mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Morogoro lilizuia mikutano na maandamano ya CHADEMA kufanyika mkoani humo na kutoa sababu mbalimbali ikiwamo kutokuwa na askari wa kutosha kuilinda mikutano hiyo.
 
Mbona wa Polisi wa kuzuia
mikutano na maandamano ya Chadema wapo? Kama siyo njama tu.
 
Hawa viongozi wa cdm nao wanachosha kila siku wanalalamikia kukandamizwa na polisi na chama tawala. Maana ya uongozi ni pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto hizo. Sasa wao badala ya kutafuta soln wanalalamika. Wasemi basi kama uongozi umewashinda wawapishe wengine. Hivi niwaulize wataweza vipi kuiongoza nchi wakipewa utawala? maana kuongoza nchi si lelemama.Tumechoshwa na kulalamika kwenu kila siku mnaonewa, tafuteni ufumbuzi wa haya mnayo yalalamikia, sio kila siku kujificha kwenye kivuli cha kuwa sisi hatutaki vurugu. Kama polis ni wafuasi wa chama tawala na nyie cdm si mnawafuasi wenu? kama ccm wanatumia wafuasi wao na nyie si mtumie wafuasi wenu?
 
hujui ulinenalo usamehewe bure
 
hujui ulinenalo usamehewe bure

hebu niambie wewe unaiejua, kagame na wenzake wangeishia kulalamikia wale wahutu walio kuwa wanawatesa na kuaua watusi enzi zile tungeiona rwanda hii ya leo? narudi pale pale tumechoshwa na ulalamishi huu wakina slaa na wenzake. hawawezi ungozi wanyamaze au wapishe wanaoweza fullsimama. Mbona wakina mrema and the like wamenyamaza na maisha bado yana endelea.
 
Inaelekea ama huelewi kinachoendelea au HUNA MENTAL CAPACITY ya kuelewa kinachoendelea. Kwa taarifa yako tu ni kuwa CHADEMA wanatumia wafuasi wao ndio maana nyinyiem na kina kova wanahanja!

Worry not, utapata picha kamili 2015.
 
Hawa viongozi wa cdm nao wanachosha kila siku wanalalamikia kukandamizwa na polisi na chama tawala. Maana ya uongozi ni pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto hizo. Sasa wao badala ya kutafuta soln wanalalamika. Wasemi basi kama uongozi umewashinda wawapishe wengine. Hivi niwaulize wataweza vipi kuiongoza nchi wakipewa utawala? maana kuongoza nchi si lelemama.Tumechoshwa na kulalamika kwenu kila siku mnaonewa, tafuteni ufumbuzi wa haya mnayo yalalamikia, sio kila siku kujificha kwenye kivuli cha kuwa sisi hatutaki vurugu. Kama polis ni wafuasi wa chama tawala na nyie cdm si mnawafuasi wenu? kama ccm wanatumia wafuasi wao na nyie si mtumie wafuasi wenu?

Hatukushangai ndo hoja za mchumia tumbo, ni kuropoka bila kutumia hekima.hao polisi wanalipwa na kodi ya ccm?Polisi si wa chama chochote bali ni wawatanzania wote.serikali na dola kwa ujumla inatakiwa kutumikia watanzania wote bila kujali chama.Na wanalipwa kwa kodi ya watanzania wote bila kujali chama.Hivyo kuropoka cdm inawafuasi wake hivyo iwatumie, huoni kama unaongea wendawazimu.Kukandamiza cdm kwa kisingizio na kutumia mamlaka vibaya, ni kuvunja katiba ndugu yangu.Tumia hekima kuchambua hoja hata kama umetumwa
 
hivi polisi wanawezaje kuzuia fujo kwenye mkutano wa chadema kama kule kwa muheshimiwa mwigulu chadema walipokuwa wakifanya mkutano walivamiwa na wana-ccm na polisi wakawa wanaangalia tu na huku wakicheka, me nilikuwa nataka chama kituache tukapambane nao wenyewe wao wakae pembeni maana nisipokufa katika mapambano ya kutetea haki ni aibu kwani nitakufa mapema tu kwa hizi shida na mateso ya ccm katika huduma za kijamii
 
Ndugu Kupelwa Asante kwa kumpa elimu huyo (Dopodopo Kadopo). Amekosa uelewa kabisa.

Dopodopo hajui kama kila bidhaa anayonunua amelipa VAT? Je Hiyo kodi anayolipa anachangia yatima ama Anatoa sadaka? Hiyo kodi si inatakiwa itoe huduma za afya, ulinzi.nk.

Tatizo si kutumwa tu, hata uwezo wake wa kufikiri ni mdogo.

Polisi wanalipwa na kodi zetu sote watanzania. Na pia CCM hawana hatimiliki ya hii nchi. Watanzania tunapaswa kupata fikra mbadala za CDM, na wale zile fikra zilizotuletea umasikini watanzania kwa miaka 50.

Nchi kama Zambia, Kenya zinatuacha nyuma kimaendeleo watanzania wakati tunang'ang'ania C - C -Mabwepande.

Viva CDM, Hongera Mbowe na Dk. Slaa.

Hongera Makamanda wote wa CDM.

Polisi wamenywea baada ya kuiona Nguvu ya Umma.
 
Hawa viongozi wa cdm nao wanachosha kila siku wanalalamikia kukandamizwa na polisi na chama tawala. Maana ya uongozi ni pamoja na kutafuta suluhisho la changamoto hizo. Sasa wao badala ya kutafuta soln wanalalamika. Wasemi basi kama uongozi umewashinda wawapishe wengine. Hivi niwaulize wataweza vipi kuiongoza nchi wakipewa utawala? maana kuongoza nchi si lelemama.Tumechoshwa na kulalamika kwenu kila siku mnaonewa, tafuteni ufumbuzi wa haya mnayo yalalamikia, sio kila siku kujificha kwenye kivuli cha kuwa sisi hatutaki vurugu. Kama polis ni wafuasi wa chama tawala na nyie cdm si mnawafuasi wenu? kama ccm wanatumia wafuasi wao na nyie si mtumie wafuasi wenu?
Masaburi type of thinking
 
hebu niambie wewe unaiejua, kagame na wenzake wangeishia kulalamikia wale wahutu walio kuwa wanawatesa na kuaua watusi enzi zile tungeiona rwanda hii ya leo? narudi pale pale tumechoshwa na ulalamishi huu wakina slaa na wenzake. hawawezi ungozi wanyamaze au wapishe wanaoweza fullsimama. Mbona wakina mrema and the like wamenyamaza na maisha bado yana endelea.

Highly cursed!Shame upon you!Have a nice bad dream of your beloved Tanzanian and God will defeat you with a great power because he is not and will not be on your side!
 
Hatukushangai ndo hoja za mchumia tumbo, ni kuropoka bila kutumia hekima.hao polisi wanalipwa na kodi ya ccm?Polisi si wa chama chochote bali ni wawatanzania wote.serikali na dola kwa ujumla inatakiwa kutumikia watanzania wote bila kujali chama.Na wanalipwa kwa kodi ya watanzania wote bila kujali chama.Hivyo kuropoka cdm inawafuasi wake hivyo iwatumie, huoni kama unaongea wendawazimu.Kukandamiza cdm kwa kisingizio na kutumia mamlaka vibaya, ni kuvunja katiba ndugu yangu.Tumia hekima kuchambua hoja hata kama umetumwa

nikuulize wale askari wa iliyokuwa libya ya khadaffi walikuwa wanalipwa kwa kutumia fedha za mafuta ya libya au fedha ya kodi ya wamarekani? Viongozi wa upinzani kule libya wange subiri na kulalama kuwa wanaonewa na kuwawa na khadaffi bila kuchukua hatua si wangekuwa wanalialia mpaka leo? kama hawa wa hapa kwetu.
 
• ASKARI WASHANGAZWA NA NGUVU ILIYOTUMIKA

na Mwandishi wetu

NGUVU ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika mikutano ya hadhara na maandamano inayofanya mara kwa mara hivi sasa yaelekea kutishia uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiasi cha kulazimika kuvitumia vyombo vya dola kuidhibiti, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.

Miongoni mwa mbinu hizo ni kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano yaliyopangwa kufanywa kwa siku 10 kuanzia jana katika Mkoa wa Morogoro kwa kulitumia Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi lilizuia mikutano hiyo na maandamano ya CHADEMA kwa madai kadhaa yakiwamo uchache wa askari, sherehe za Sikukuu ya wakulima (Nanenane), mgomo wa walimu uliozuiwa siku tatu zilizopita na maeneo husika kutumiwa na CCM katika mikutano ya hadhara.

Kinyume cha kauli ya Jeshi la Polisi mkoani humo kuwa lina uchache wa askari, jana idadi kubwa ilionekana ikijiandaa kukabiliana na maandamano na mikutano ya CHADEMA kama ingefanyika.

Baadhi ya askari waliowekwa tayari kukabiliana na CHADEMA, walieleza kushangazwa kwao na nguvu kubwa iliyotumika kuwazuia CHADEMA badala ya nguvu hiyo ingeelekezwa kuwalinda.

Polisi wapigwa jua

Taarifa kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa askari kutoka katika mikoa ya Iringa, Dar es Salaam na Dodoma waliokusanyika mkoani humo kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kukabiliana na mikutano ya CHADEMA kama ingefanyika hiyo jana, walijikuta wakishinda juani bila kazi.

Kushinda juani huko kwa askari hao kunatokana na uamuzi wa viongozi wa CHADEMA kuamua kusitisha maandamano na mikutano hiyo hadi Agosti 8, mwaka huu ambapo itaanzia katika eneo la Mikumi (Kilosa).

Baadhi ya askari waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa sharti la kuhifadhiwa majina yao walisema kwa namna ulinzi ulivyoimarishwa isingekuwa rahisi kwa maandamano na mikutano ya CHADEMA kufanyika.

"Logic (mantiki) iko wapi kama nguvu hii iliyoandaliwa kwa ajili ya kuyazuia maandamano ya CHADEMA ingetumika kuyalinda, si kila kitu kingekuwa sawa na yangeenda vizuri tu, sijui ni wapi tunaelekea katika hali hii," alisema mmoja wa askari.

Alisema kimsingi wao kama askari wa ngazi ya chini hawana tatizo na CHADEMA isipokuwa wanalazimika kupokea amri kwa kuwa ndiyo kazi waliyochagua kufanya na kusema kama watendaji wa serikali hawataacha siasa katika kazi kuna hatari ya kuipeleka nchi pabaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alipoulizwa kuhusu hali hiyo alikiri kuwapo kwa askari wengi mkoani Morogoro na kusema ni gharama zimetumika licha ya kukataa kutaja maeneo waliyotoka.

Kuhusu askari wa ngazi ya chini kulaani maandalizi makubwa ya kuzuia mikutano ya CHADEMA badala ya kulinda, Kamanda Shilogile alisema hakuna askari anayeweza kutamka kauli hiyo na kwamba hawatumiki kwa masilahi ya kisiasa.

"Unaniuliza askari wametoka wapi, hilo si swali la msingi, wewe jua gharama zimetumika kwa ajili ya suala hili na huku kusema askari wamesikitishwa na maandalizi ya kuzuia mikutano badala ya kuilinda mbona hawajaniuliza mimi? Hiyo ni wewe mwandishi umetengeneza stori," alisema Shilogile

CHADEMA yasogeza mbele Sangara

Uongozi wa CHADEMA jana ulitangaza kusogeza mbele mikutano yake na maandamano hayo (Operesheni Sangara) ili kuepuka maafa ambayo yangeweza kutokea baina ya wafuasi wake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro iliyozuia operesheni hiyo.

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, walisema zuio hilo la polisi limelenga kukisaidia chama tawala (CCM) ambayo hivi sasa ina hali mbaya kiutawala.

Mbowe alisema CCM imetishwa na matokeo ya ziara za CHADEMA zilizofanyika hivi karibuni katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mbowe alisema baada ya ziara ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa na mafanikio makubwa wabunge wa CCM walitishika kwa kiasi kikubwa hata kufikia baadhi yao kuomba mikutano hiyo ipigwe marufuku ili isiwaondolee uhalali wa kuitwa wabunge licha ya kuzembea katika majukumu yao.

"Tunapaswa kujua kuwa haya ni mapambano baina ya haki na batili, siku zote dhalimu hawezi akaruhusu kirahisi kuondolewa katika udhalimu wake…na atatumia njia mbali mbali ya kujihalalisha, kwa hiyo katika hili tunapaswa kuwa wavumilivu na wenye busara ya hali ya juu katika kukabiliana nao," alisema Mbowe.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kutambua kuwa kuminya haki za msingi za wananchi kwa manufaa ya wachache ni suala lisiloweza kukubalika mbele ya jamii na kwamba hali hiyo ya kuchagua watu wa kuwatumikia itasababisha watu kujenga usugu dhidi ya jeshi hilo.

Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu na Jeshi la Polisi walikubaliana kuahirisha uzinduzi wa ziara hiyo iliyokuwa ifanyike jana na badala yake itafanyika Agosti 8, katika Jimbo la Mikumi na kufuatiwa na ratiba nyingine ya mikutano katika Mkoa wa Morogoro.

"Jana (juzi) hatukulala tulikuwa katika mawasiliano na Jeshi la Polisi hata kufikia IGP kushindwa kupokea simu yangu, mwenyekiti alimtafuta na amempata leo asubuhi (jana), tumemfahamisha hoja zetu na mapendekezo yetu naye akatushauri turudi kwa RPC wa Morogoro kwa ajili ya mapendekezo hayo," alisema.

Alibainisha kuwa katika mapendekezo yao ni pamoja na kumueleza kuwa hoja ya CCM kufanya mikutano pamoja na CHADEMA haina nguvu, kwa kuwa CCM waliomba kwa ajili ya Agosti 4, mwaka huu tu, na maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro yanafikia kilele Agosti 8, mwaka huu na mgomo wa walimu umesitishwa na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.

Alisema Jeshi la Polisi linapaswa kufahamu dhana ya siasa ya vyama vingi ni kutoa uhuru wa wananchi kuchagua sehemu ya kwenda hivyo kuweka visingizio kuwa kuna mikutano miwili katika wilaya moja ni kuua demokrasia.

Aidha, Dk. Slaa aliongeza kuwa hata kitendo cha jeshi hilo kuchukua magari kutoka sehemu tofauti za nchi kwa ajili ya kuwadhibiti CHADEMA mkoani Morogoro ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma na badala yake gharama zilizotumiwa zingeweza kusaidia kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi wa jeshi hilo.

"Tunaionya serikali hii iwe mara ya mwisho na tumekubali hivi kwa sababu sisi si watu wa fujo, ila hatutaweza kuvumilia hasara ya namna hii, kwa kuwa hizi fedha tunazotumia ni za ruzuku zinazotolewa na serikali kwa vyama, sasa hasara hii iweje wabebeshwe wananchi kizembe zembe kwa ajili ya kuminya demokrasia?" alihoji.

Alisema Jeshi la Polisi linatumia sheria zilizowekwa na wakoloni katika kuendesha nchi huku likifahamu fika wakoloni walitumia fursa hiyo kwa ajili ya kuwaminya wapigania uhuru.

"Katika PGO ya Polisi ni mambo machache ndiyo yameboreshwa na zilizobaki ni zile za kikoloni, hivyo watambue sasa ni wakati wa siasa huru na si vita baina ya wenye nchi na wakoloni katika kudai uhuru," aliongeza Dk. Slaa.

Agosti mosi, mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Morogoro lilizuia mikutano na maandamano ya CHADEMA kufanyika mkoani humo na kutoa sababu mbalimbali ikiwamo kutokuwa na askari wa kutosha kuilinda mikutano hiyo.

chadema ongezeni nguvu Mupigwe na Polisi risasi ili wazanziabar wapumue
 
hebu niambie wewe unaiejua, kagame na wenzake wangeishia kulalamikia wale wahutu walio kuwa wanawatesa na kuaua watusi enzi zile tungeiona rwanda hii ya leo? narudi pale pale tumechoshwa na ulalamishi huu wakina slaa na wenzake. hawawezi ungozi wanyamaze au wapishe wanaoweza fullsimama. Mbona wakina mrema and the like wamenyamaza na maisha bado yana endelea.

Duh, mkuu unataka wawe na vichwa kama vya kagame?Si itakuwa balaa.Yaani wakiingiza watu mitaani sasa si itakuwa balaa.Hembu chukulia IRINGA,MBEYA, MWANZA,SHINYANGA,ARUSHA, MANYARA, IGUNGA, Makambako, Tunduma, etc waachie kitu kwa mara moja Si tutakuwa kama Libya?

Mi naona huu mwendo wa kulalamika na kuvumiliana angalau utatufikisha uchaguzi mkuu.Kama huju ni kwamba kwa uchache hiyo mikoa ikianzisha kwa pamoja, halafu polisi wajisahau piga virungu na mabomu watu wataanza taratibu hamia katika fujo, polisi watakimbizwa uraiani, vibaka watakuwa sehemu ya vurugu ili waweze iba, then taratibu watu wataanza hesabu siku tuu waanze jazwa sillaha kutoka nje.Kwanza wataanza tumia za jadi na baadaye habari itakuwa ikibadilika kama mgonjwa mautiuti.Then watu wa nje watachagua timu ndipo utasikia Ikulu ikishcnagnyikiwa na mambo ya defecting. Nadhani busar ya polisi iwe kuruhusu mikutano bila ruhusu mazingira ya kuonekana wameinyima haki nafasi.Hao polisi kama wamezuia mkutano basi waondoke mitaani.Wawepo kwa mpangilio wa amani.Ila hii tabia ya kutaka jaribu mabomu na kufurahia itakuja geuka vibaya .

Public psychology huwa hairuhusu sana patokee ugonvi at any point kwani huwa mambo yanweza evelove fasta sana, na baadaye chanzo cha ugomvi kisiwe kigezo tena,kwani kutakuwa na watu wanalipiza kisasi kwa kufiwa,kuumizwa,kuharibiwa mali zao etc.
 
Back
Top Bottom