Ngumi yamuua dereva wa daladala

Kwanza niwape pole wafiwa kwa msiba wa ghafla mno. Nawaasa madereva wote barabara si uwanja wa ngumi wala ubabe kumbukeni kuwa gari ni mali yako but katu barabara sio mali binafsi so kila mtu anahaki ya kutumia bora tu anafuata sheria na kanuni za usalama. Juzi kati tumempoteza sweti leo suka wa daladala nini hatima ya haya yote na yanaashiria nini tuendako.nawaombeni kuweni na subra na msamaha pale dereva mwenzio anapokosea ikibidi mwelekeze na kama mbishi mwache epusha shari.
 
RIP Suka
Jamani tujifunze kuzidhibiti hasira zetu hili ni fundisho kwetu sote. Maana kuna watu wanashindwa kabisa kuzizuia hasira zao, huwezijua mwenzako ana magonjwa gani au pengine siku yake ishafika unakunja tu jigumi-matokeo yake ndo hayo unanunua kesi ya mauaji.

Tuwe tunafikiri kabla ya kutenda.

Poleni wafiwa.
 
Naomba niwatoe kwenye mada kidogo.... juzijuzi kuna wajeshi waliua!!! tuliacha mada na kushambulia jeshi, leo suka kaua, naona tunapeana nasaha za maana zaidi

Ushauri wangu ni kwamba tuwaangalie watu kama watu na si kama wawakilishi wa watu wengine

HASIRA HASARA REGARDLESS WEWE NI NANI KATIKA JAMII... POLE WAFIWA NA TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA, SI KILA ATEMBEAYE NI MZIMA
 
kaka hapa kweli umenena..
haswa sisi wabongo hatuna kabisa utamaduni wa kupima afya zetu, hivyo basi hatujijui tunaumwa nini.
 
Wacha afe manaake wao wakiwa wanaendesha daladala huwa wanatutesa sana madereva wa magari mengine madogo, wacha rife

Eeee jamani maneno gani haya,hivi ingekua ni ndugu yake yamemkuta hayo ungeongea hayo maneno? kabla ya kuandika kitu hebu jaribu kufikiri ingekua ni kaka,dada,shemeji yako ungeongea?
 
Naona huko home watu kupigana kama kuku wanaona ndiyo dili sana au ndiyo kuonyesha ubabe, mara askari wamepiga wameua, ooh mwalimu kapiga mtoto shuleni kaua, mara mama wa kambo kamchoma mtoto makalioni na sehe mu za siri, mara dereva wa daladala.

Jamani unaruhusiwa kupigana pale tu unapokuwa unatetea uhai wako na siyo hasira zako. Hata wezi wakikuvamia kama wanachotaka ni mali wachukue waende zao lakini kama wanataka uhai huo usiwape kirahisi lazima zipigwe.

Sasa barabarani ukiwa na hasira za hivyo utaendeshea gari kwenye bedroom yako? Maana hayo matukio ni mengi kama mchanga wa bahari barabarani. Inabidi ukubali kuyazaoea na kuvumiliana nayo.

Wewe Godliving Severini uliyeua mwenzako hivi ungeshuka unipige ngumi mimi ingekuaje? Hizo hasira zenu za kijinga kuna siku mtakuja kuzifanya kwa Ninja halafu muone matokeo yake.

'' A true man is identified not by showing his temper but by his control of it". Mtu yeyote asiyeweza kudhibiti hasira zake hajakamilika kiumeni.
 
duh! njaa hasa inatutuma vibaya.
mungu wangu tuondoshee njaa hii na uwajaalie subira wafiwa. ...amen
 
Naona huko home watu kupigana kama kuku wanaona ndiyo dili sana au ndiyo kuonyesha ubabe, mara askari wamepiga wameua, ooh mwalimu kapiga mtoto shuleni kaua, mara mama wa kambo kamchoma mtoto makalioni na sehe mu za siri, mara dereva wa daladala.

Jamani unaruhusiwa kupigana pale tu unapokuwa unatetea uhai wako na siyo hasira zako. Hata wezi wakikuvamia kama wanachotaka ni mali wachukue waende zao lakini kama wanataka uhai huo usiwape kirahisi lazima zipigwe.

Sasa barabarani ukiwa na hasira za hivyo utaendeshea gari kwenye bedroom yako? Maana hayo matukio ni mengi kama mchanga wa bahari barabarani. Inabidi ukubali kuyazaoea na kuvumiliana nayo.

Wewe Godliving Severini uliyeua mwenzako hivi ungeshuka unipige ngumi mimi ingekuaje? Hizo hasira zenu za kijinga kuna siku mtakuja kuzifanya kwa Ninja halafu muone matokeo yake.

'' A true man is identified not by showing his temper but by his control of it". Mtu yeyote asiyeweza kudhibiti hasira zake hajakamilika kiumeni.

Aksante Ninja kwa kutukumbusha hili. Bado wale wanaowabonda wake/ waume zao majumbani!!
 
Hasira ni hasara,na biblia pia ikasema Hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu,juzi alikuja rafiki yangu amefura hasira eti katoka huko alikotoka anaenda kugombana na mtu,ilibidi nimwulize kwanza sababu aliponieleza sababu kwanza nilicheka,nilipocheka hasira yake ndo ikapanda zaidi,ikabidi nimweleze sbbu za mimi kucheka,alipoelewa nikaanza kumpa darasa nikamwambia mtu akikukorofisha nenda kaongee nae kirafiki kabisa atakuelewa kuliko kwenda kishari,nashukuru alinielewa na akaufanyia kazi ushauri.

My point is pale tunapohisi hatukutendewa haki ni vizuri kutulia kwanza na kutafakari cha kufanya mambo ya kukurupuka si mazuri,huwa nawambia rafiki zangu siku hizi watu wanatembea wamekufa anasubiri sababu tu,unaweza ukagombana na mtu pressure ikapanda akaanguka utaambiwa umeua,kwa hiyo ni vizuri tujifunze kudhibiti hasira zetu.
 
Duh!! Bonge la point mwana, nimepunguza hasira zangu ghafla baada ya kusoma hii post yako
 
Back
Top Bottom