Ngumi Jiwe!

Jamaa mmoja mrefu alikuwa akipigana na mshikaji mmoja mfupi sana mida ya saa 2 usiku. Watu walipoingilia kati kutaka kuwatenganisha, yule jamaa mrefu akasema, "hebu niacheni nimfundishe adabu huyu pimbi".

Baada ya kama dakika mbili,yule jamaa alipigwa kichwa na yule jamaa mfupi, akaanguka chini, akaanza kulia,' mamaa nakufaa, nichukulieni namba za gari iliyonigonga!.

[WATU]:Hakuna gari iliyopita hapa, ni yule pimbi kakupiga.
[JAMAA MREFU]:Basi naombeni nyundo aliyonipigia!.
[WATU]:Hakuwa na nyundo.
[JAMAA MUREFU]:Basi nipelekeni kivulini!.
[WATU]:Mida hii ni usiku, hakuna jua!

Ahahahahahahahahaha.
 
Back
Top Bottom