Ngoyai Lowasa ni fundi wa kutafuta upenyo ktk siasa zilizompenya

Laptop01

JF-Expert Member
Nov 29, 2009
1,365
796
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu nyenendo za Ngoyai Lowasa ambae kufuatia sakata la Richmond Development Co.LLC alilazimika kupima na kubwaga manyanga UWAZIRI MKUU. Nimebaini kuwa ukiacha kilichoonekana kuwa ni kupenda kujilimbikizia kila kiitwacho mali, mtu huyu ni mtaalam wa kusoma nyakati zinazoweza azaliwe upya katika siasa za Tanzania.

Katika suala la mabomu alitoa kauli yake nzito
Katika suala la uchumi nimemsikia leo akitoa kauli kwamba paundwe tume ya kuchunguza namna bora ya kulishughulikia suala hili, target yake katika hili imekuwa ni kulilenga kundi la wafanya kazi.Kauli zake ni nzito na zenye maana kuliko zile za mkuu wa nchi katika kutatua matatizo ya kitaifa

Hitimisho langu likawa ni kwamba huyu mtu ni fundi wa kutumia matukio yanayojiri kitaifa ili kujiinua kisiasa. Lakini pia Ngoyai ni mchapa kazi na hutembea katika kauli zake. Nakumbuka suala la maji ya ziwa victoria na vikwazo vya wasudani na wamisri, suala la shule za sekondari za kata, suala la bandari kavu (despite the implementation failure)

Ushauri wangu kwake: kwakuwa giza linaendelea kuitafuna nchi na uchumi wake, Ngoyai toa kauli yako pia katika hili. Toa kauli yako Ngoyai katika malipo ya serikali ya taifa lako kwa DOWANS.
 
ni fisad kweli, ila ana afadhali sana kuliko huju kaka yao aliyekalia nchi
 
Anatafuta upenyo .......Leo amehamia habari ya mishahara midogo kwa wafanyakazi.
USHAURI: Agawe mali zake zote kwanza ndipo tuanze kukuelewa.
 
Na sioni ndani ya CCM anayeweza kumzuia sasa hivi kwa sababu kimahesabu na kimkakati kesha mwengua JK.
Wapinzani wanatakiwa kuweka darubini zao ktk tahadhari muda wote maana ninaona ktk ndoto CCM ikimsimamisha EL 2015.

Kuachia kwake ngazi 2008 kutahesabiwa kama kuwajibika kisiasa na si kwamba alifanya makosa.

Lowasa ni mahiri katika siasa za nchi hii hasa ukichukulia kwa sasa ndani ya CCM hakuna watu safi na wenye sauti. Kina Salim, Warioba, Butiku n.k wanaonekana ni wasafi lakini hawana nguvu (kama mwalimu) ndani ya chama.

Laiti EL akamrudia Mungu akaacha kupenda kujilimbikizia mali, akaacha ufisadi (kama huwa wanaacha), aka-renew mahaba yake kwa nchi he can make a very good leader as compared to our very own president ambaye naye jana alikuwa analalamika maisha magumu na kuwalaum Chadema kumpa siku tisa badala ya miaka 23 kama Mzee Nyerere (hamwiti baba wa taifa)
 
huyu lowasa na ra wote ni hatari wamesimika spika wao na mara ghafla kamati za bunge zimekuwa na nguvu kliko hata mawaziri kulikoni au sababu wenyeviti wengi wa kamati za bnge n vibaraka wao
 
huyu jamaa kiukweli ni fisadi lakin tuangalie upande wa pili wadau, kipindi akiwa waziri mkuu watu kwa kweli walikuwa wanawajibika vya kutosha haswa wakurugenzi wa halmashauri, lakin kwa sasa dah hali ni tete sana.. kwa ujumla huyu ni mtendaji mzuri ambaye kama angejiepusha na ufisad nadhani ndo mtu ambaye ndani ya CCM anathubutu hata kumwajibisha mtu, kaka yetu aliyeongoza nchi kwa kweli kapoteza mwelekeo kabsaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Hivi sio plan yao Kikwete aboronge ili EL ashine?.....Kikwete amekua mdhaifu sana kuliko awamu ya kwanza mpaka inanipa tabu kuwa ndo uwezo wake wa mwisho..
 
Back
Top Bottom