Ngorongoro heroes vipi?

kichenchele

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
539
176
Habari za asubuhi wana JF, naomba kama kuna mwanamichezo anayefahamu matokeo ya timu yetu ya vijana ''NGORONGORO HEROES'' na wale vijana wa Ivory coast, maana nimejaribu kuangalia ktk magazeti ya leo sioni kitu, au hii mechi imesogezwa mbele?
 
Gazeti la mwananchi wanaseme hadi wanakwenda mitamboni tulikuwa tumefungwa 1-0. TBC 1 jana waliripoti matokeo hayo huku mechi ikiwa inaendelea. Sijui matokeo ya mwisho yalikuwaje.
 
Ahsanteni sana wana JF, nadhani tayari sababu za kufungwa zimeshatolewa na kocha kwa kushirikiana na TFF au siyo? maana tumeshazoea kusikia, hali ya hewa ya kule ni tofauti na yetu, uchovu wa safari, maandalizi, majeruhi wengi n.k
 
Ahsanteni sana wana JF, nadhani tayari sababu za kufungwa zimeshatolewa na kocha kwa kushirikiana na TFF au siyo? maana tumeshazoea kusikia, hali ya hewa ya kule ni tofauti na yetu, uchovu wa safari, maandalizi, majeruhi wengi, refa hakuwa fair etc,
 
Sio kila siku ni Jumapili na sio kila siku pweza anatabiri ukweli..wamefungwa kwa kuzidiwa mchezo na vijana wa ivorycoast..natumai makosa wameyaona na watayarekebisha katika mechi ya marudiano..mcheza kwao hutunzwa.
 
bado napata moyo na hii timu ya vijana... naomba uzima nikawashangilie vijana mechi ya marudiano
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom