Ngono yakithiri Makazini

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeeleza kuwa rushwa ya ngono sehemu za utumishi wa umma ni changamoto mpya, inayochangia kukwamisha juhudi za kupunguza maambukizi mapya ya Ukimwi nchini.

Mwenyekiti Mtendaji wa Tacaids, Dk Fatma Mrisho, alisema hayo mwanzoni mwa wiki hii kwenye warsha ya siku mbili iliyoshirikisha watendaji wakuu kutoka Idara za Utumishi wa Umma.

Kutokana na kukithiri kwa aina hiyo ya rushwa katika utumishi wa umma, alitaka waajiri na watu wengine wenye tabia hizo kuacha na wazingatie haki, sheria na vigezo wanapohitaji kuajiri watumishi wapya.

Dkt. Mrisho alibainisha, kwamba Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi ya UKIMWI tangu mwaka 2004 kutoka asilimia saba na kufikia asilimia 5.7. Akizungumzia mafanikio machache ya mkakati wa kupunguza maambukizi, alisema kuwa asilimia 94 ya Watanzania hawana maambukizi na hivyo ni vyema kila mmoja kuendelea kujikinga. Kutokana na mwelekeo huo, aliomba wananchi waendelee kuchukua hadhari za kujikinga ili wasiambukizwe.
 
flora, .... jaribu kutoa ushahidi ambao unaweza kutolea maelezo si kwa sababu tu hao ni Tacaids wanahusika na Ukimwi kwahiyo hata uhuru wa sifa / mambo yao yawekwe katika JF..

habari zao (wamezipata) zikiwa za kupambana na ukimwi nawapa sifa nzuri zikiwa za kuendeleza tabia za ngono nawapa sifa chafu na mbaya pia jamii haitowapendelea kuwa karibu nao.
 
hao wa makazini wanakubali kutoa mzigo bila ya kinga? ama kweli ni wapumbavu. ni kazi tu ndio inawasababisha wajitoe muanga, hawawazi kua wakiwa na afya njema ndipo watafaidi vizuri matunda ya hizo kazi zao?
 
Hapo tacaids kwenyewe ndo kitovu cha ngono kazini...watu wanaoigana mikato ya hatariiii

Kweli nimeamini, penzi kitovu cha uzembe!Ndo mana hata maambukizi yanazidi kuongezeka kwa sababu hao TACAIDS badala la kujitaidi kudhibiti maambukizi mapya yasiongezeke, wao ndo wanahamasisha maambukizi mapya, lol!
 
TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeeleza kuwa rushwa ya ngono sehemu za utumishi wa umma ni changamoto mpya, inayochangia kukwamisha juhudi za kupunguza maambukizi mapya ya Ukimwi nchini.

Mwenyekiti Mtendaji wa Tacaids, Dk Fatma Mrisho, alisema hayo mwanzoni mwa wiki hii kwenye warsha ya siku mbili iliyoshirikisha watendaji wakuu kutoka Idara za Utumishi wa Umma.

Kutokana na kukithiri kwa aina hiyo ya rushwa katika utumishi wa umma, alitaka waajiri na watu wengine wenye tabia hizo kuacha na wazingatie haki, sheria na vigezo wanapohitaji kuajiri watumishi wapya.

Dkt. Mrisho alibainisha, kwamba Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi ya UKIMWI tangu mwaka 2004 kutoka asilimia saba na kufikia asilimia 5.7. Akizungumzia mafanikio machache ya mkakati wa kupunguza maambukizi, alisema kuwa asilimia 94 ya Watanzania hawana maambukizi na hivyo ni vyema kila mmoja kuendelea kujikinga. Kutokana na mwelekeo huo, aliomba wananchi waendelee kuchukua hadhari za kujikinga ili wasiambukizwe.

Hii kitu ni kweli kabisa...sisi tukiendaga reatreat mpaka aibu..yaani mke wa mtu analala chumba kimoja na kajamaa tu na mme wa mtu anafanya vivyo hivyo. Ni balaa aisee
 
Hii ndio Tanzania kama niijuavyo; mkweree mwenyewe na mkewe wanahubiri mpango wa uzazi kwa mananchi, lakini wao wenyewe wana timu ya mpira nyumbani!!!
 
TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeeleza kuwa rushwa ya ngono sehemu za utumishi wa umma ni changamoto mpya, inayochangia kukwamisha juhudi za kupunguza maambukizi mapya ya Ukimwi nchini.

Mwenyekiti Mtendaji wa Tacaids, Dk Fatma Mrisho, alisema hayo mwanzoni mwa wiki hii kwenye warsha ya siku mbili iliyoshirikisha watendaji wakuu kutoka Idara za Utumishi wa Umma.

Kutokana na kukithiri kwa aina hiyo ya rushwa katika utumishi wa umma, alitaka waajiri na watu wengine wenye tabia hizo kuacha na wazingatie haki, sheria na vigezo wanapohitaji kuajiri watumishi wapya.

Dkt. Mrisho alibainisha, kwamba Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi ya UKIMWI tangu mwaka 2004 kutoka asilimia saba na kufikia asilimia 5.7. Akizungumzia mafanikio machache ya mkakati wa kupunguza maambukizi, alisema kuwa asilimia 94 ya Watanzania hawana maambukizi na hivyo ni vyema kila mmoja kuendelea kujikinga. Kutokana na mwelekeo huo, aliomba wananchi waendelee kuchukua hadhari za kujikinga ili wasiambukizwe.

Asilimia 1.3 for 8 year...

Wastani wa 0.16 kwa mwaka vs. resources wanazopata..

SIJUI ?!
 
Back
Top Bottom