Ngonjera za TFF, kupanga matokeo na bonanza la Azam Zambia

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linajing’ata na kujipuliza lenyewe. Na limeanza kwa kujihami kuhusu hofu ya kupanga matokeo kwenye ligi mbalimbali nchini.

Mwishoni mwa wiki shirikisho hilo lilitoa taarifa likiwaonya viongozi wa klabu, wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa michezo mbalimbali kutojihusisha na vitendo vya upangaji wa matokeo.

Likasema limejipanga vizuri kusimamia michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza, Daraja la Pili pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), mashindano ambayo yanaendelea.

Kwa ukali kabisa, TFF ikasema:"Yeyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo wa upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa.”
SOMA ZAIDI...vpl.jpg
 
Back
Top Bottom