Ng'ombe wapigwa risasi na maaskari mbuga ya Mikumi

chitalula

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,302
415
picha hizi zikionyesha ng'ombe wa wafugaji wakiwa wamepigwa risasi na maaskari wa wanyama pori katika mbuga ya mikumi
Baadhi ya ng'ombe walifariki baada ya muda kidogo kupita kutokana na majeraha hayo
08.JPG 10.JPG 012.JPG

My Take;

Sijapata sababu hasa ya kwa nini maaskari hao wamechukua hatua hiyo ila
hata kama wafugaji hawa walikosea kwa kuingiza mifugo sehemu ya hifadhi, kisheria naona sio sahihi kwa askari hao kufanya walivyofanya, kwani pia ni kinyume cha haki za wanyama.
Hata mambo yasiyohitaji fedha yanatushinda, mengine yanahitaji utashi tu wakisiasa, sitashangaa wakurugenzi wa mbuga hizi watakapowapongeza askari kwa watakao uita ushujaa waliofanya kwani hii nchi sasa inatetea ujinga mtupu.
Nategemea watu wanaohusika na haki za mifugo wachukue hatua dhidi ya kitendo hiki cha kinyama kabisa
 
si bora ya hao wanauwa wanyama askari hawa wengine wanatuua sisi raia
 
wakome...wanatusumbua sana hao...jangili wasumbue na wafugaji nao wasumbue...
haikubaliki....
juzi hapa faru wameuwawa mmekaa kupiga kelele kuwa hakuna ulinzi,...
askari wanauwawa na jangili mnakalisha midomo yenu chini..
na hao jangili wengine wanaingia kwa migongo ya kuchunga ng`ombe...kiutaratibu waliopiga hao ng`ombe wamefanya kitu kizuri....
 
Ng'ombe anakosa gani? Amechagua kuingia mbugani? Kwanini tunamhukumu ng'ombe kwa kosa asilolitenda? Hapana hawa Askari wamekosea, hata ng'ombe wana haki ya kuishi. Si kosa lao kuumbwa ng'ombe, lazma tuwajali na kuwatetea.
 
Ni jambo la kusikitisha lakini vile vile ni wakati muafaka sasa jamii ya wafugaji wakaachana na ufugaji wa kijima. Yaani wao ni kuswaga wanyama tu from north to south na baadae south to north looking for greener pastures.

Matokeo yake ni machafuko kila hawa watu wanapopita kwenye jamii za wakulima. Au kama hapa wanapokatisha kwenye mbuga au hifadhi za taifa. Wote tunajua majangili wengi wanaingia kwenye hifadhi zetu kwa disguise za kuswaga mifugo yao, hapo askari wa wanyamapori wanawekwa kwenye dilemma.

It's high time viongozi wa jamii za wafugaji wafundishwe ufugaji wa kisasa ili nawao wawafundishe wanajamii wao. Mambo ya overgrazing yatakua ni history.
 
wakome...wanatusumbua sana hao...jangili wasumbue na wafugaji nao wasumbue...
haikubaliki....
juzi hapa faru wameuwawa mmekaa kupiga kelele kuwa hakuna ulinzi,...
askari wanauwawa na jangili mnakalisha midomo yenu chini..
na hao jangili wengine wanaingia kwa migongo ya kuchunga ng`ombe...kiutaratibu waliopiga hao ng`ombe wamefanya kitu kizuri....
mkuu hapa ngombe kosa lake nini?tofautisha ngombe na mwenye ngombe.kama kweli walikua na hasira kwanini wasinge wakamata na kuwashtaki wenye ngombe?ok fine,baada ya kuwapiga risasi hao ngombe nini kilifuatia?
 
labda kwa taarifa tu ni kwamba hiyo kazi unavofikiria ni tofauti na hali halisi...,hao watu unakamata kesho wapo tena....ama wanaingiza wanatoka wanaenda kaa mbali...ukikamata ng`mbe...kijiji kizima kinakuja na kufanyia fujo askaripori,...na hapo hapo diwani mara mbunge ndo sehemu ya kuchukulia credit....
sasa kwakuwa kitu chochote ambacho hakitakiwi hifadhini ni illegal...then nafikiri hii ni njia nzuri kabisa ya kuziuia...na inawork i gurantee you...
hutaona kesho wameingiza....
na inatupunguzia usumbufu...
 
We unafanya TANAPA! Lazima tu. Sema ukweli bwana mkubwa!
 
Ukosefu wa akili na kufanya kazi kama maroboti, ukipewa amri hata kama ni ya kijinga we unakurupuka tu, sasa kama faru hapigwi risasi kwanini upige ng'ombe? Wachungaji wapo hao ndo wakukamata! Akili nyingine matope, hata wange-confiscate ng'ombe au wakawapa fine baada ya kukamata! Sisi ndio waafrika bwana! Nachukiaga sana kuzaliwa mwafrika!
 
Ni kweli mkubwa..kufanya kazi kama maroboti,..
na nyie mkiona mifugo hifadhini si ndo mnakimbilia kwa waziri kusema jamaa hawafanyi kazi kabisa..awachukulie hatua..
mfano juzi hapa mmeshabikia siasa za kusimamisha watumishi tanapa kwa faru wawili na mmesema mmepata waziri mchapa kazi na mkaandika kweli hapa....ila mngejua hao faru wenyewe wanakotoka S/africa tangu januari mpaka june 2012 wameuwawa 245 mngeacha ushabiki..
acheni hao tanapa wafanye kazi..,....
 
Baadhi yao ni wafugaji ma poachers, ardhi yote hii Tanzania ni lazima waingie kwenye hifadhi kulisha mifugo yao??
 
Tatizo la hao askari wengi wanafoji vyetii . hawajasoma shule. sasa unampiga huyo risasi kafanya nini? amekuwa simba huyo? kha!
 
Nawapa pole wadau wote mliotoka povu kwa tukio hili, pole yangu naitoa kwasababu mtoa mada ametoa taarifa juu juu bila kuelezea tukio lenyewe lilikuwaje na nyie bila hata kujiuliza mkaanza kuconclude na kubishana. Mngeonyesha busara kumuuliza mtoa mada tukio zima lilikuwaje hadi ikafikia kurusha risasi? Je kulikuwa na kukaidi amri au kutaka kujihami kwa wachungaji au vipi? Je hao ng'ombe walikuwa eneo gani la hifadhi? Ni katikati au huku mipakani? Wote tunafahamu sheria zipo na pia utashi huwa unatumika katika kutekeleza sheria hizo kwa hiyo ni mazingira ndo yangedetermine hao askari wawapige risasi au wawakamate na hatua zingine za kiutu zichukuliwe. Sasa nyie mmeshatoa lawama bila kufahamu mazingira ya tukio lenyewe.... Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom