Natafuta Ng'ombe wa maziwa

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
156
Jamani, naombeni msaada wenu.
Natafuta ng'ombe wa maziwa wa kisasa, kama wale wanaopatikana Iringa (ASAS Dairy products).Nitawapata wapi huko Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha n.k.
Naomba contacts.
Nahitaji wanaotoa at least lita 20 kwa siku.
Nataka wenye mimba ya kuanzia miezi mitano hadi sita.

Nimetafuta sana bila mafanikio!

Wafugaji wengine wananiuzia ng'ombe waliochoka (ng'ombe anatoa lita 3-4 kwa siku?)
Na serikali nayo kimeo, nilishaweka oda ya ng'ombe (hybrid) huko Nanyumbu wanasema oda ya mtu inaeza kuchukua hata miaka miwili na pia unaweza kupata idadi chini ya ile uliyoomba. Nonsense!

Naomba msaada wenu.

Natanguliza shukrani.
 
pole sana kwa huo usumbufu. unaonaje ukienda hukohuko ASAS diaries ukwauliza? huenda wakawa na msaada zaidi.
hongera kwa kufikiria kufuga, ni plan nzuri sana.
 
huu ni mradi mzuri sana...... ukiwa na eneo la kutosha ukawa na ng'ombe wako wa maziwa atleast kumi wanaokamuliwa .... uknawatunza kwa ubora na lishe ya kitaalam .... hesabu yake ni nzuri sana .... wapo ng'ombe wanatoa mpaka 30-40 liters per day .... pale kilacha, Himo Moshi kuna shamba la mifugo la mission unaweza ulizia pale
 
huu ni mradi mzuri sana...... ukiwa na eneo la nkutosha uknawa na ngombe wakno wa maziwa atleast kumi wanaokamuliwa hesabu yake ni nzuri sana .... wapo ngombe wanatoa mpaka 30-40 liters per day .... pale kilacha, Himo Moshi kuna shamba la mifugo la mission unaweza ulizia pale

Thanks LAT.
Mi' nataka nichukue 20 cows.
Hata kama nitakuwa natumia 200,000 kwa matunzo kwa kila ng'ombe poa tu!
Unaweza kunipatia contacts? Hapo umeshanipatia mwanzo, nitafanya efforts za kuwapata.

Cheers!!!!!!!
 
Good idea! hivi unaweza ukafahamu bei ya kila ng'ombe kwa kulingana na umri wake? kwa kweli ni mradi mzuri kama ukiwa na eneo kubwa kama ulivyosema.
kama mkipata hao n'ombe naomba n mimi nipewe taarifa maana nina interest ya ufugaji hasa wa ngombe na kuku.
 
Thanks LAT.
Mi' nataka nichukue 20 cows.
Hata kama nitakuwa natumia 200,000 kwa matunzo kwa kila ng'ombe poa tu!
Unaweza kunipatia contacts? Hapo umeshanipatia mwanzo, nitafanya efforts za kuwapata.

Cheers!!!!!!!

CHE GUAVARA

by experience .... ukitaka u capitalize na kufurahia ufugaji wenye faida ni kuwa na utaratibu wa kuwa na stock ya vyakula vya mifugo ..... ukiweza kuwa na stock za from one month to three month hakika uta enjoy ufugaji na utaiona faida .... kwa ng'ombe wa maziwa fanya stock ya fodder (malisho ya mimea) , grains (pumba za mahindi, pollards, mashudu ya pamba n.k) , ng'ombe hawa wa kutoa maziwa hunywa mpaka lita 50 za maji kwa siku

i am very anxious to see you are succesful with this project
 
safi sana mkuu ata kitulo mbeya walikua wanatoa ao ng'ombe. mwenye mimba ilikua laki tano sa cjui kwa sasa
Duuh, ng'ombe mwenye mimba laki tano tu!! ilikuwa bei ya lini hiyo? it seems to be a reasonable and good price maana akifika tu unapata matunda yake hapohapo.
thanks for this contribution!!!!!
 
Duuh, ng'ombe mwenye mimba laki tano tu!! ilikuwa bei ya lini hiyo? it seems to be a reasonable and good price maana akifika tu unapata matunda yake hapohapo.
thanks for this contribution!!!!!

Lkn tatizo nasikia hawa ng'ombe hawawezi kuwa producive maeneo yenye joto kama Dar, Pwani, Mtwara n.k.
Nd'o maana maeneo wanakopatikana ni maeneo ya baridi (e.g: Kitulo-Iringa, Kilimanjaro, Arusha, mbeya e.t.c)

Lkn mimi nataka niwaweke Dar/Pwani.
Nataka kati ya 50-75% ya kamshahara kangu (4,000,000/= Tshs) kawe kanatumika kuwatunza wao.
 
Soko la Maziwa kwa Dar liko vp?

Hadi mwaka jana mwezi April lita moja ilikuwa si chini ya 1,000/= Tshs.
Kwa uzoefu wa nchi yangu ambayo pesa inashuka thamani kila kukicha, naamini bei HAITAKUWA chini ya 1,000/= Tshs kwa sasa.

Wenyeji watupatie majibu lkn naomba pia tusije tukabadili lengo la mada (Ng'ombe wa maziwa nitawapata wapi, contacts e.t.c)
 
huu ni mradi mzuri sana...... ukiwa na eneo la kutosha ukawa na ng'ombe wako wa maziwa atleast kumi wanaokamuliwa .... uknawatunza kwa ubora na lishe ya kitaalam .... hesabu yake ni nzuri sana .... wapo ng'ombe wanatoa mpaka 30-40 liters per day .... pale kilacha, Himo Moshi kuna shamba la mifugo la mission unaweza ulizia pale

Mkuu LAT

Kwa hii dunia ya leo, ufugaji mkubwa hauhitaji kabisa eneo kubwa. Tanzania tuna kila kitu ila Hii serekali ndio inaturudisha nyuma kabisa, Mfano kenya ufugaji ni biashara nzuri saana na inalipa, Kuna watu wanafuga, kuna watu wanaohususika na utengenezaji wa vyakula vya mifugo. Kwa hiyo mfugaji anakuwa na uhakika na vyakula kwa mwaka mzima. Pia kuna soko la maziwa la uhakika. Brookside wamefanya mapinduzi makubwa saana walikuja Tanzania ni hii hii serekali iliwafanya wakahamua kuondoka,

Kwa DSM soko la maziwa lipo na ni nzuri tena saana, Kupata ngombe jaribu pia kuwasiliana na Jamaa wa RUVU Ranch, pia tembelea kambi ya JKT pia ipo hapo ruvu unaweza kupata kwa bei nzuri. Kujifunza zaidi unaweza tembelea Ranch ya Fredrick Summay wanashamba kubwa saana na ngombe wengi anaweza akakuuzia pia,

Naomba uangalie hii video ya huyu dogo, Ukifungua hiyo link utapata na nyingine naamini utaelimika

Last edited by a moderator:
Soko la Maziwa kwa Dar liko vp?

mkuu .... pale mapinga bagamoyo kuna jamaa ana ng'ombe zaidi ya 60 ... tena anafuga kihuni huni tuu ... ng'ombe wanapelekwa nkulishwa machungani na ngombe hao wala sio wa kiwango kwa namna fulani , kwenye shamba lake heka mbili.... anatoka kila asubuhi na madumu ya 20 liters matano (20x5= 100 liters) ... yeye anauza maziwa katika milk shop yake tegeta .... anauza glasi moja ya maziwa sh 400 .... lita moja anatoa glasi tano ..... hivyo 400x5= tsh 2,000 .... Tsh 2,000 x 100 liters = 200,000 per day .... hata akitumia tsh 50,000 per day

hesabu nzuri sana hii

ila inahitaji security .... ng'mbe wanaibiwa sana na wanapelekwa unguja
 
Mkuu, siyo rahisi ukapata mkulima wa kukuuzia ng'ombe wa maziwa mwenye mimba. HAKUNA.

Ukitaka ng'ombe bora ni lazima ugharimike, tafuta mkulima mwenye mbegu bora za ng'ombe, kisha nunua ndama, tafuta bwana mifugo awe mshauri wako jinsi ya kuwakuza. Hakika baada ya muda utaingia kwenye kundi la wafugaji bora wa ng'ombe wa maziwa. Ng'ombe bora kwa sasa unaweza kukamuliwa maziwa lita zaidi 60 kwa siku.
 
Sasa mkuu si utujulishe hao ng'ombe wanapatikana wapi? Tupatie contacts if possible.
Tunaweza kulegeza masharti ya kusema "hadi ng'ombe awe na mimba"!

Niko tayari kununua ndama hata kwa laki tano (lkn kwa kumtumia mtaalamu wangu wa mifugo).

Kuna hasara gani ukitumia 600,000 kwa mwezi kwa matumizi kwa ng'ombe anayetoa lita 60 au hata 40 za maziwa kwa siku?

Hao ng'ombe wa lita 60 wanapatikana wapi ( au ni wa kwenye mtandao - Netherland, Switzerland, n.k).
Tunataka wanaopatikana hapa Tz!

Thanks
 
Mkuu, siyo rahisi ukapata mkulima wa kukuuzia ng'ombe wa maziwa mwenye mimba. HAKUNA.

Ukitaka ng'ombe bora ni lazima ugharimike, tafuta mkulima mwenye mbegu bora za ng'ombe, kisha nunua ndama, tafuta bwana mifugo awe mshauri wako jinsi ya kuwakuza. Hakika baada ya muda utaingia kwenye kundi la wafugaji bora wa ng'ombe wa maziwa. Ng'ombe bora kwa sasa unaweza kukamuliwa maziwa lita zaidi 60 kwa siku.

Mkuu Majimoto

Labda hujakutana nao WAPO WAKULIMA WANAUZA NGOMBE WENYE MIMBA, Moja wao alikuwa jamaa wa ASSAS-Iringa alitoa matangazo mpaka kwenye magazeti. Pia hata watu binafsi wanazo kunajamaa ntawasiliana nae ili anipe contact then ntaziweka hapa
 
Back
Top Bottom