Ng'ombe bora wa maziwa

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
156
Hi, ladies and gents!
Habari zenu?
Naombeni mnisaidie - nitapata wapi ng'ombe bora wa maziwa (ng'ombe wa kisasa)?
Nilishawahi kusikia sikia kuwa kuna mahali naweza kupata ng'ombe ambaye/ ambao wana mimba ambao wanatarajia kuzaa ndani ya miezi miwili/ mitatu.
Sitaki kununua ng'ombe ambaye ametumika!
Sitaki kununua ng'ombe mdogo a.k.a ndama, ambaye atanichukulia muda wangu mwingi na gharama kubwa hadi kufikia kumfaidi!

Naomba msaada wenu wadau.
Mnipatie contacts na maelekezo yanayoweza kunisaidia.
Thank you in advance.
I remain.

Dr. Mbale (a.k.a Dr. Ernesto Che Guevara-II)
 
Morogoro ulizia SUA au kile chuo kipo jirani na SUA kinaitwa LITI. Pwani Kuna shirika la Elimu Kibaha. Arusha pia nadhani kuna taasis zinajishulisha na Mifugo. So Inategemea pia wewe uko wapi
Nahakika kwenye vyuo au taasisi zinazijishugulisha na mifigo utapata watu wenye information. Kwenye Tasisi kama hizi kuna watu wanaweza kuwa wanajua hata wahusika binafsi wenye wanao supply bidhaa unayohitaji.

NB
Sina utaaalamu wa mifugo lakini nahisi kwenye maeneo kama hayo unaweza kupata maelekezo mazuri
 
Duh! Kumbe JF members tuko faster kiasi hiki?
Nilidhani naweza kujibiwa baada ya mwezi hivi! Maana hii nd'o mara yangu ya kwanza kujitosa kwa ujumbe JF.
Asanteni sana. Thank you very much.
Nakaribisha majibu ya ombi langu la msingi, maoni, ushauri n.k......

Long live JF founder!!!!!!!!!!!!
 
Hope Malila is around, atakusaidia.

Lady umejuaje?

Ni kweli,naweza kutoa mchango kidogo. Kama uko Dsm/Pwani nenda Ruvu darajani kama unakwenda Chalinze,pale kuna shamba la serikali,watakwambia habari hizi vizuri tena bure na ng`ombe wenyewe utawaona kwa macho. Kama uko Mbeya/iringa nenda Kitulo dairy farm,utapata kilicho bora,kuna vituo vingi sana na watu binafsi wapo wenye ng`ombe. Nashauri kwenda ktk taasisi za serikali kwa sababu huko utapata mbegu ambayo ni sawa na unakopeleka au watakupa crossbreed sawa na location ya shamba lako.

Kwa watu binafsi iwe option ya mwisho, au uwe unamfahamu sana huyo mfugaji binafsi.
 
Duh! Kumbe JF members tuko faster kiasi hiki?
Nilidhani naweza kujibiwa baada ya mwezi hivi! Maana hii nd'o mara yangu ya kwanza kujitosa kwa ujumbe JF.
Asanteni sana. Thank you very much.
Nakaribisha majibu ya ombi langu la msingi, maoni, ushauri n.k......

Long live JF founder!!!!!!!!!!!!

Wasiliana na bodi ya maziwa au wasiliana na wafugaji wa ng'ombe kwa simu. Utawapata kwenye link nilizokupatia.

Ukifanikiwa tupe feed back
 
Hi, jamani, nashukuru kwa michango yenu mizuri sana.
Bado nahitaji michango yenu.
Contacts zilizopo hapo juu naendelea kuzitumia. lakini wengine nd'o hivyo tena wanahusika na kuuza maziwa tu na products zake. Lakini bado naendelea kuwatafuta wadau.

Thanx!
 
Hi, jamani, nashukuru kwa michango yenu mizuri sana.
Bado nahitaji michango yenu.
Contacts zilizopo hapo juu naendelea kuzitumia. lakini wengine nd'o hivyo tena wanahusika na kuuza maziwa tu na products zake. Lakini bado naendelea kuwatafuta wadau.

Thanx!

Che Guevara-II, Utakuwa ni muujiza mfugaji akuuzie ng'ombe wake anayemkamua maziwa, kama utampata basi ujue huyo ng'ombe ana matatizo ya afya. Ninakushauri utafute mfugaji mwenye mbegu bora ununue ndama kwake uanze wewe mwenyewe kumlisha hadi akuwe. Haiwezekani mfugaji akuuzie ng'ombe asubuhi na jioni uanze kumkamua maziwa.
 
Mwanza, Kwimba mabuki kuna ranchi... wanabreed ngo'mbe na nyati.. wana mbeguu nzuri.. tulinuna wetu huko!!
Dodoma Kongwa vilevile wanaweza kuwa nao!!
 
Back
Top Bottom