Ng'ombe 65 wauawa Sengerema

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Kuna habari ambazo hazijathibitishwa ambazo zinasema kwamba 'Mwekezaji wa Kimarekani" ameamuru ng'ombe wauawe na Land Cruiser huko Sengerema hatima yake ndiyo hao ng'ombe 65 kuuawawa. Kama kuna yeyote ambaye ana habari hizi azimwage hapa ukumbini.
 
Hao ngombe walikuwa wanaumwa au ? Imekuwaje kuwaje ? Kwanini ametumia gari asingeita afisa mifugo kwa ushauri zaidi
 
Kuna habari ambazo hazijathibitishwa ambazo zinasema kwamba 'Mwekezaji wa Kimarekani" ameamuru ng'ombe wauawe na Land Cruiser huko Sengerema hatima yake ndiyo hao ng'ombe 65 kuuawawa. Kama kuna yeyote ambaye ana habari hizi azimwage hapa ukumbini.


Nadhani ni Serengeti


Ng'ombe 65 kwa Land Cruiser, sio mzaha! Huenda zimetumika Land Cruiser 10



.
 
Hii land cruiser ni ng'ombe au kuku sioni Land cruiser ikiuwa ng'ombe 65
 
Hii nayo ni siasa?

Hapana ilistahili kuwekwa kwenye michezo. Wewe huoni habari ya mwekezaji aliyeingia nchini kwa mabadiliko yaliyofanywa na wanasiasa na si ajabu hana chochote cha kuwekeza bali amekuja na briefcase yake na akiondoka nchini ataondoka kama milionea au hata bilionea kuwa na kiburi cha kuamrisha dreva awagonge ng'ombe wa Watanzania kama ni siasa?

Habari hii imeandikwa katika gazeti la Mwananchi kama habari mpya, sijui kama ina ukweli kiasi gani, nilitegemea watakuwa wameshapata habari za kutosha kuhusu kilichojiri katika maujai hayo ya ng'ombe (kama ni kweli) lakini mpaka sasa hivi bado habari hiyo inaonyeshwa kama habari mpya na hakuna chochote kilichoongezwa zaidi ya "Mwekezaji Mmarekani aamuru ng'ombe wauwawe kwa Land Cruiser" sijui kama waliokufa ni hao 65, zaidi au pungufu. Kama unataka ihamishwe na kupelekwa kwenye michezo unaweza kuwaomba MODS wafanye hivyo.
 
Back
Top Bottom