Ngo'mbe 20 kutua Tanzania leo

Delegate

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
331
201
Jana tumetangaziwa hapa Botswana kuwa Ng'ombe 20 mali ya rais wa Jamuhuri ya Tanzania zitaondoka leo kuelekea Tanzania,Rais Kikwete alinunua NG'Ombe 10 alipokuja hapa mwezi wa tatu kushiriki sherehe ya miaka 50 ya chama tawala,ng'ombe wengine 10 alipewa zawadi na Rais Khama wa Botswana,imebidi taarifa itolewe kwenye vyombo vya habari ili wananchi waweze kuelewa nini kinaendelea kwenye tukio zima,Rais Khama ametoa maelezo yake kuwa ng'ombe wake aliotoa zawadi ni mali yake aliyoachiwa urithi na wazazi wake,tunafurahi sana kuona viongozi wetu wa africa wakiweka wazi mambo yote yanayowahusu ili kuondoa matatizo ya kutiliwa shaka
 
Ng'ombe 20 na wote wana mimba, baada ya muda mfupi wanakuwa 40 huu ndio usafirishaji sahihi wa ng'ombe. Sijui Wataalam wetu waliufata?
 
acha upuuzi wewe,kwani hujui kama ni kodi zetu anatumia?
Na ww avga upuuzi zawadi mtu asipewe au asitumie mshara wake kwa sababu kodi yako?
Aje na perfume au chupi?
Mao tse-tung alimtuma Chuo en-lai amuulize Nyerere Tz ijengewe reli ya TZ - Zambia au tuwape (tuzae na wanawake wa TZ)mbegu za kichina hapo 1968 akachagua TAZARA bado alirudi na zawadi hazikutangazwa wa awamu ya pili Stella Attous wa aqamu ya tatu bonge la dhahabu zote kodi zenu?
 
wewe hujui unachokisema kabisaaa,poleeee.
 
Hata mimi ningependa sana kupata ng'ombe wa kisasa kutoka Botswana ila gharama za kuwasafirisha sitaziweza. Wenzetu wamekuwa ni wafugaji bora sana sana. Wameondoa kabisa breed ya ng'ombe wa kienyeji na kuwapandikiza kupata ng'mbe chotara aina ya Brahman. Hawa ng'ombe ni wakubwa sana ukilinganisha na aina ya ng'ombe tunaofuga Tanzania.

Kitu kingine tunachoweza kujifunza kutoka Botswana ni namna bora ya kufuga ng'ombe na siyo kuwa waswagaji tu. Hili lingeondoa kabisa tatizo tulilonalo sasa hivi ambapo nchi nzima inataka kuwa ni malisho ya ng'ombe kiru ambacho kinaleta migongano kati ya wakulima na wafugaji. Migongano kama hiyo haipo Botswana kwa vile wafugaji hawahami na mifugo yao na kila mfugaji anatakiwa kuwafugia kwenye eneo lake tu. Ni juu ya mfugaji kujua kuwa kuna wakati wa kiangazi na inabidi kuwa na kisima cha maji na akiba ya chakula cha mifugo (hay).
 
Jana tumetangaziwa hapa Botswana kuwa Ng'ombe 20 mali ya rais wa Jamuhuri ya Tanzania zitaondoka leo kuelekea Tanzania,Rais Kikwete alinunua NG'Ombe 10 alipokuja hapa mwezi wa tatu kushiriki sherehe ya miaka 50 ya chama tawala,ng'ombe wengine 10 alipewa zawadi na Rais Khama wa Botswana,imebidi taarifa itolewe kwenye vyombo vya habari ili wananchi waweze kuelewa nini kinaendelea kwenye tukio zima,Rais Khama ametoa maelezo yake kuwa ng'ombe wake aliotoa zawadi ni mali yake aliyoachiwa urithi na wazazi wake,tunafurahi sana kuona viongozi wetu wa africa wakiweka wazi mambo yote yanayowahusu ili kuondoa matatizo ya kutiliwa shaka
huo ni ufujaji wa pesa,mbona hapa bongo kuna ng'ombe kibaaaaao,tena zingine amezipiga chini kwenye baraza jipya!
 
Kama anaweza kutumia fedha zake kwa style hii............gharama ya kuwasafirisha hao ng'ombe ni gani? watalipa?
Je fedha zetu walipa kodi atazifanyeje?? kama sio kwenda kubembea!!!

this guy............ukulima na ufugaji hauji tu kwavile umestaafu au unakaribia kustaafu!!!
:crazy::crazy:
 
damn! Jamaa ana moyo kweli, kutoa mali ya urithi kama zawadi yataka moyo asee!...na mkuu wa Kaya yetu mbona kama katutosa wanakaya?! Hapa tuna ng'ombe, kwanini asingewanunua apa na kutubusti wanakaya? anyways thats how it goes
 
sasa kwanini Rais wetu asinunue hao ng'ombe hapa angalau awape biashara wananchi wake...kwanini apeleke hela nje?? hao wana madili yao mengine kumbukeni botswana ina almasi na madini mengineyo
 
hao n'gombe watasifirshwaje mpaka bongo??usikute ndege yetu ya rais ndio itafanya kazi hiyo
 
weye ndio wajii top thinker..???!! hivi rais pesa ya mshahara wake akitumia kwa matumizi yake binafsi mnasema ni kodi yenu ! khaa! mnataka mumpangie pia kula ale nini ..?
 
Hii issue inatatiza kidogo...ukiacha hao ng'ombe 10 alionunua JK...hao wengine 10 alipewa zawadi kama JK au kama rais wa Tanzania? Maana kama alipewa kwa kuwa ni rais wa Tanzania, ina maana ni ng'ombe wa waTanzania wote na JK alipokea kwa niaba. Awatoe kwa vituo vya yatima/wazee!
 
Jana tumetangaziwa hapa Botswana kuwa Ng'ombe 20 mali ya rais wa Jamuhuri ya Tanzania zitaondoka leo kuelekea Tanzania,Rais Kikwete alinunua NG'Ombe 10 alipokuja hapa mwezi wa tatu kushiriki sherehe ya miaka 50 ya chama tawala,ng'ombe wengine 10 alipewa zawadi na Rais Khama wa Botswana,imebidi taarifa itolewe kwenye vyombo vya habari ili wananchi waweze kuelewa nini kinaendelea kwenye tukio zima,Rais Khama ametoa maelezo yake kuwa ng'ombe wake aliotoa zawadi ni mali yake aliyoachiwa urithi na wazazi wake,tunafurahi sana kuona viongozi wetu wa africa wakiweka wazi mambo yote yanayowahusu ili kuondoa matatizo ya kutiliwa shaka

Mkuu tunashukuru kwa taharifa, labda nikutoe wasi wasi kwamba Jakaya ni Raisi muwazi na wala sitashangaa kama ng'ombe karibu wote atawapa vikundi vya raia, na yeye kwa kuwa ana shamba atabaki na ngombe wachache tu wa maziwa. Kusema kweli Botswana wana ujuzi mkubwa katika ufugaji wa ng'ombe wa kisasa ndio maana nyama yao inahuzika kwa wingi Ulaya.
 
Back
Top Bottom