Ngoma za siasa zisizojulikana...

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Watanzania!

1992 watu walitoka UT na kuanzisha vyama vya siasa ili kukidhi matakwa ya wafadhili. Na baadhi wakatoka TANU nope CCM kuanzisha ama kujiunga na vyama hivyo. Kikubwa hapa ni kwamba hayati Mwalimu ndiye alieshauri jambo hilo na likawa. Vyama KIINI MACHO vikaanzishwa na vimeendelea kuwepo bila malengo yake kufa ama kubadilishwa (VYAMA VIINI MACHO KWA WAFADHILI) na katika mfumo wa vyama hivyo ambavyo vipo kwa ajili ya... Watanzania walio wengi tumeendelea kuimbishwa na kuimba nyimbo ambazo hatuzifahamu na mwisho wa siku tunabaki kulalamika kuwa tumeonewa na wale wahusika tunaowatetea mda huo wako kimya wakila kuku. Tutaendelea kupata machungu na nyoyo kuuma kama tutaendelea kutaraji vyama hivi,

tutaendelea kusikia machungu na taarifa tusizozipenda ikiwa tutaendela kukumbatia vyama hivi...

mpaka siku tutakapojua kuwa tunachezeshwa kilua kwenye ngoma ya kimasai! muda utakuwa umekwenda na vizazi vitatuhukumu.

Ahsanteni sana.
 
Na katika kuthibitisha hilo: Mara zote chama kimojawapo kikianza kupata nguvu na kubadili uelekeo basi hapo songombingo na mashaka huanzishwa kwa makusudi maalumu ili chama kile kipate sura tofauti miongoni mwa watu, na miongoni mwa mapandikizi huhamia vyama vingine ama hurudi walikotoka wakipeleka maneno tofauti na matamshi yao ya awali. Wote mnajua nini kinatokea katika siasa za vyama vyetu vya upinzani iwe CDM, CUF, NCCR, TLP na hata vile ambavyo havina anuani!
 
Back
Top Bottom