Ngereja ni mwakilishi wa Rostam katika Baraza la Mawaziri?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Mara baada ya JK kutangaza Baraza lake la Mawaziri, kulikuwa na maoni kwamba kulikuwa na mafungu matatu ya mawaziri aliowachagua; Kwanza ni wale ambao ilibidi tu awachague kutokana na jamii ya Watanzania kuwajua kuwa ni wachapakazi (akina Magufuli, Mwandosya, Mwakyembe, Sita nk); pia kulikuwa na kundi la pili la "washikaji". Kundi la tatu ni la wale ambao majina yao yaliletwa na "wafadhiri" wa JK katika mbio za kuwania uraisi. Hapa ndipo watu kama kina Ngereja walitajwa, kwamba waliwekwa kwa maslahi ya watu wengine, na Ngereja kusemwa alikuwa mtu wa Rostam. Wengi hata wanasema ukiangalia utendaji wa Ngereja tangu ateuliwe kuwa Waziri utaona haujalenga kuinufaisha serikali, bali maslahi ya watu binafsi, licha ya kuwa kwa kweli hakuwa na vigezo vya kuwa na uwezo wa kuisimamia hiyo wizara, ikionyesha wazi "aliwekwa".Na sasa wengi wanaona huwa na makundi haya mawaili, "mawaziri wa washikaji" na "mawaziri wa wafadhiri" kuwa kumechangia sana hali iliyopo ya utendaji usio makini wa serikali. Basi nimejiuliza sana, kwamba ni mawaziri wangapi wa namna hii tunao katika Baraza la Mawaziri, ambao ni chanzo kikubwa cha serikali yetu kuwa mbofumbofu!
 
Yatasemwa mengi sana, na kwa jinsi anavyoboronga watu wataamini kila kitu. Kama ningepata nafasi ya kumshauri ningemshauri ajiuzulu tu kama RA abakie kula mabilioni aliyomake kwenye hii mikataba feki kwa vile hakuna sheria ya kumgusa katika nchi hii.
 
Halafu anamcheka Chifu Mangungo wa Usagara wakati na yeye ni wale wale.
 
Back
Top Bottom