Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,268
- 33,041
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema msafara wake alipokuwa ziarani Geita kupita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) Ijumaa, haukuzuiwa na walinzi wa mgodi huo kwa nia ya kupekuliwa.
Akizungumza na NIPASHE jana kutokana na kuchapisha habari kuhusu kuzuiwa kwa muda kwa msafara wake kwenye lango la GGM, Ngeleja alisema habari hizo zimemshitua sana kwani hakukuwa na kitu kama hicho.
Jana gazeti hili lilichapisha habari katika ukurasa wake wa kwanza ikisema kuwa Waziri Ngeleja alionja machungu baada ya msafara wake kuzuiwa kwa muda na walinzi wa GGM ili kupekuliwa.
Katika habari hizo ambazo ziliandikwa na mwandishi aliyekuwa kwenye msafara wa Ngeleja, zilisema kuwa msafara huo ulikaa langoni hapo kwa takribani dakika 10 hadi uongozi wa juu wa mgodi ulipoingilia kati na kuokoa jahazi.
Naye Ofisa Uhusiano wa GGM, Joseph Mangilima, ambaye habari ya jana ilisema alipoulizwa juu ya kadhia hiyo alikataa kuzungumzia kwa maelezo kuwa kampuni inayolinda mgodi huo ya G4S inajitegemea na
hawezi kuzungumza kwa niaba yao, alitoa ufafanuzi zaidi wa kadhia hiyo.
Akizungumza jana kwa njia ya simu na NIPASHE iliyotaka kujua kwa kina chanzo cha kadhia hiyo, Mangilima alisema kimsingi msafara haukuzuiwa ili upekuliwe.
Walinzi walikuwa wanabadilishana zamu ndani ya kontena ndiyo maana wakachelewa kufungua geti mara moja. Hata dakika moja haikumalizika, alisema Mangilima.
Alifafanua kuwa msafara wa Waziri Ngeleja ulikuwa umetokea ziwani lakini mgodini kulikuwa hakuna taarifa kwamba ulikuwa unaelekea huko (mgodini), ndiyo maana walinzi hawakuwa tayari kufungua geti mara moja.
Mangilima alisema wamesikitishwa na habari hiyo kwa kuwa haikueleza ukweli wa suala lenyewe.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI