Ngeleja ameshindwa kujibu swali

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Mh Zitto Ameuliza swali pesa zinazotumika kulipa mafuta mazito na wizara ya nishati na madini ili hali hizo pesa hazikuwa outlined kwenye bajeti ya 2010/2011. Je hii imekaaje, Amelijbu kisiasa kuwa wakutane na zito amupe maelekezo. Je hili bunge letu lipo kwa ajili yetu sisi wananchi au wanasiasa.

Hili ni TATIZO kwa Taifa letu
 
Labda wamezoeana kuitana pembeni na kutulizana kwa kitu kidogo,tumezoea ukisema pssssss,anaejua una muita ataitika ila kama haujui utaendelea na mambo yako!

Huyu kamuita zitto pembeni,tena mbele ya macho ya watanzania kabisa duh,...angekua sio wa pembeni angekataa aseme watanzania wanataka kujua hapo hapo
 
kwa hivi watanzania hatuna zaidi ya kujua ila zito. na kama ni Zito anayetakiwa kujua tu ya nini kuwa na public bunge!!?? ni vema kuwa na private bunge!!??
 
Majibu yanayohusu takwimu huweza kutolea majibu hapo kwa hapo bila ya kuwa na takwimu sahihi akifanya hivyo ataishia kuambiwa kuwa analidanganya Bunge
 
Majibu yanayohusu takwimu huweza kutolea majibu hapo kwa hapo bila ya kuwa na takwimu sahihi akifanya hivyo ataishia kuambiwa kuwa analidanganya Bunge

Kwani zimetakiwa takwimu au source ya hayo malipo?.........binafsi sielewi kwa nini tuNAwalipa hawa IPTL capacity charges,megawati wanazo supply TANESCO halafu tunawanunulia haya mafuta?.......ni kama kule TRL serikali iliuza hisa 51% halafu ikawa inalipa mishahara ya wafanyakazi,kukodi injini na mabehewa......hawa viongozi(vitongozi) vipi?
 
Zitto ni mnafiki anauliza maswali ya kujikosha.
Wote waweza kuwa ndani ya boti moja.
 
...fellow Tanzanians, the situation is becoming worse, kubali au kataa! Many of us know how Ngeleja 'won' the ministerial post and what is now doing, definitely no wonder!

My take:
Je badala ya kujihangaisha, kuna haja ya kufanye search/utafiti mpya kujua ni nani ameilaani nchi hii!!!??
 
Sasa wabunge wengine na spika nao wameona ni halali Zito kupewa majibu pembeni?

halafu ndio mnasema tuwaamini watutengenezee katiba hawa watu?:nono:
 
Naomba number za waheshimwa wabunge wengine kupitia CHADEMA ziwekwe wazi hapa,
kuna haja ya kuwa tunatoa maduku duku yetu direct.

Kama katika hili kuna haja ya kumdokeza Mbunge mwingine wa CHADEMA alirudie hilo swali
ili tuone kama na yeye ataitwa pembeni, na zaidi ili tujihakikishie kupata majibu juu ya hili swala.

Japo sihitaji very strategically kupata jibu, lakini sasa am concerned with the pembeniship going on
 
Maskini mpambanaji Zitto rushwa imeshamfanya mtu wa kutulizwa pembenni kama alivyo tulizwa kuwekwa katika kamati ya Raisi ya madini ambayo mpaka leo hatujui impact yake ni nini
 
Maskini mpambanaji Zitto rushwa imeshamfanya mtu wa kutulizwa pembenni kama alivyo tulizwa kuwekwa katika kamati ya Raisi ya madini ambayo mpaka leo hatujui impact yake ni nini

Hakika dogo zitto ni mzito hata wa kuelewa tumempoteza kala chambo ya kijani.
 
Maskini mpambanaji Zitto rushwa imeshamfanya mtu wa kutulizwa pembenni kama alivyo tulizwa kuwekwa katika kamati ya Raisi ya madini ambayo mpaka leo hatujui impact yake ni nini

Mnataka kulikuza na kumchafua mtu kwa jambo ambalo Zitto hana uwezo nalo kanuni hazimruhusu yeye kubishana na spika na hata kama angetaka kumkatalia ngereja maelezo yake angetakiwa anyoshe mkono na apewe nafasi jamani mbona mmunaendeleza chuki kwa huyu mbunge,waandishi wa habari wanafanya nini si wa mkomalie Zitto na Ngereja kwa vipi watapeana majibu nje ya kikao cha bunge
 
waandishi wa habari wanafanya nini si wa mkomalie Zitto na Ngereja kwa vipi watapeana majibu nje ya kikao cha bunge

Wakumkomalia Zitto na Mwenzake Ngeleja si waandishi wa habari tu bali ni watanzania wote wazalendo, wana wenye uchungu na nchi hii nikiwepo mimi na wewe..mbona mwenzetu unawaachia waandishi wa habari jukumu zito namna hii..? Mmmh hadi mwaka huu ukaishe sijui huyo Zitto atakuwa ktk position gani...sasa hivi anajionyesha dhahir ni mtu wa aina gani..
 
Mh Zitto Ameuliza swali pesa zinazotumika kulipa mafuta mazito na wizara ya nishati na madini ili hali hizo pesa hazikuwa outlined kwenye bajeti ya 2010/2011. Je hii imekaaje, Amelijbu kisiasa kuwa wakutane na zito amupe maelekezo. Je hili bunge letu lipo kwa ajili yetu sisi wananchi au wanasiasa.

Hili ni TATIZO kwa Taifa letu

Huyu jamaa hafai ama anajua udhaifu wa Zito wanataka wakachakachue majibu. kwa anataka wakutane nyuma ya pazia.
 
Mnataka kulikuza na kumchafua mtu kwa jambo ambalo Zitto hana uwezo nalo kanuni hazimruhusu yeye kubishana na spika na hata kama angetaka kumkatalia ngereja maelezo yake angetakiwa anyoshe mkono na apewe nafasi jamani mbona mmunaendeleza chuki kwa huyu mbunge,waandishi wa habari wanafanya nini si wa mkomalie Zitto na Ngereja kwa vipi watapeana majibu nje ya kikao cha bunge

Well said..! umekuwa mkweli. Ushabiki nao tukiuendekeza utatufikisha tusikokujua.
 
majibu yanayohusu takwimu huweza kutolea majibu hapo kwa hapo bila ya kuwa na takwimu sahihi akifanya hivyo ataishia kuambiwa kuwa analidanganya bunge
uzuri wake ndo huuu kuwa mawaziri kwa sasa wamekuwa makini zaidi si kulopoka kama makamba!
 
Haya mambo ndg hayakuanza leo, wakibanwa maswali walikuwa wanaema umetumwa, wakiambiwa watoe
huduma kwa wananchi wanatoa ahadi kesho, muda ukifika sababu kibao, je tunatafuta rangi ya paka au tunataka
paka anayejua kula panya????
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom