Ngeleja aibomoa kambi ya CHADEMA, Wenyeviti, Makatibu watimkia CCM

Bwana mdogo Ngeleja hana hata nusu ya ubavu wa kubomoa CHADEMA. Hizi ni siasa tu.
Kama yeye mwamba mbona wenye vituo vya mafuta wanamtoa kamasi kila siku?
 
Wa ajabu kweli hawa vijana,yani wenzio wanaamka wao wanavuta shuka,wacha waende wakajifie huko
Wameona waende CCM ili wakalelewe huko na sio kuwa na wasiwasi wa kufukuzwa uanachama pale wanapotofautiana kifikra na m/kiti.
 
Wameona waende CCM ili wakalelewe huko na sio kuwa na wasiwasi wa kufukuzwa uanachama pale wanapotofautiana kifikra na m/kiti.

shida ni kwamba watapata lump sum na umaarufu kidogo wa muda, tu basi.. Hakitakuwa kipato cha kudumu.Utu ukishauuza,dah..
 
Hakuna shida. Muda baso sana. Binafsi nakubali kuwa ni pengo kwa sababu hata kura moja ni ya maana sana. Sidhani kama ni suala la kumuachia Dr. Slaa kwenda kufungua tawi jipya la CDM huku Sengerema, la kujiuliza kubwa ni hili "Ni nini chanzo cha umaskini wetu?" Kama tutapata jibu la swali hili, tunatakiwa kutafuta ni namna gani tutapambana na adui anayetuletea umaskini huu. Lakini kama hatufahamu kuwa adui mkkubwa kuliko UMASKINI, UJINGA NA MARADHI ni CCM kamwe hatuwezi kutoka hapa tulipo.
Njaa ni mbaya, wao wao walifikiri kupewa madaraka ya kuwa wenyeviti na makatibu wa wilaya watakuwa wamesolve matatizo yao, walisahau kuwa chama bado kinahitaji kujengwa kila ngazi ili kesho iwe ya neema kwa walio wengi na siyo mmoja mmoja. Kazi bado ni kubwa sana. Tunahitahi kuelewa ni namna gani tutapambana na adui CCM ili watoto wetu waje wafurahie matunda ya kazi zetu, vinginevyo, kizazi kijacho hakitakuwa na la kujifunza kutoka kwetu. Nawasilisha.
 
Hawa ni baadhi ya wanachama (viongozi) wasotakiwa kabisa awa ni njaa kali wamepewa viera vya wizi wakahama chadema, kwanza kura zao ni ngapi si ni sita tu, kwa taharifa yenu haijatokea chama cha upinzani chenye nguvu za ajabu kama chadema kwa sasa, na ata serikali inawaogopa sana, mkuu wa polisi katumiwa ati mikutano yao kaipiga marufuku, huu ni uoga, angalia balaa walofanya igunga, abraham shimbo pia alitutisha, haturudi nyuma. Sisi ni chadema na chadema ni sisi, peeeeeeepooooooooooz power,mungu ibariki chadema, mungu walaani sana CCM mafisadi, majizi, madhulumati na magamba yao...........
 
Njaa mbaya sana! Hao jamaa wameamua kurudi walikotoka kuliko na ufisadi na posho za wizi, kuwa mwanachama au kiongozi wa CDM unahitaji uzarendo wa dhati na si unafiki, kwa hii hali tete iliyopo Ccm leo, ni vigumu sana kusimama kidete kukitetea, na hata ikitokea mtu shujaa wa namna hiyo basi ujue ni njaa tu. CDM kiko ndani ya mioyo ya watanzania wa kweli wenye uzalendo usiyoteteleka
 
Huwezi kuwa na akili timamu asokuwa na utahahira ukaamua kuama chama cha haki chadema na kwenda kushrikiana na chama kinachoongozwa majizi, mafisadi (ccm mafisadi pia magamba) yanayojulikana dunia nzima kwa ufisadi, angalia sasa mafisadi ya ccm yanavyochakachua utaratibu wa kupata katiba mpya, kisa usalama wenu (ccm mafisadi pia magamba) na si kwa usalama pia wellbeing kwa watanzania, mjue kiama chenu (ccm mafisadi pia magamba) kinakaribia, ccm limekaa kama kasha tu na hao ndo viongozi ndani hamna kitu, majuzi mmejaribu kuvuana magamba mkashindwa kwa kuwa wote mmeoza leo mtu anahamia huko, uyo lazima ni tahahira. Na huo ndo mtaji wetu wa kuwamaliza
 
Ndio maana halisi ya demokrasia,mtu una ruhusa kujiunga na chama chochote cha siasa ili mradi hauvunji sheria,nawapa hongera hao waliohama na nawaambia tu kuwa uzuri wa walichokiona leo sio watakachokiona kesho
nakubaliana na wewe
 
Chama ni itikadi, wananachama, viongozi na vikao. CHADEMA kama chama cha siasa kupoteza wanachama na viongozi wake ni pigo kubwa sana.!! Nawapa pole kwa kupoteza mvuto miongoni mwa viongozi na wanachama wake hadi kuamua kurudisha kadi na kukihama chama chao. Nawapongeza wanachama hao kwa uamuzi wao wa busara kuhamia Chama Cha Mapinduzi. KARIBUNI CCM TUIJENGE TANZANIA YETU.!!

Mtaanza kuijenga sasa?
 
Kwan toka Dk slaa ambiwe analipwa mil 7 bila ya kodi hajajibu,wana cdm poleni du hii ingekuwa wamehama humu ingekaa wk na gazet letu la tanzaniadaima lingekuwa habar kuu
 
hivi ngeleja tofauti na huko kwao anaweza kupata ata ujumbe wa nyumba kumi? Sijui watu hao wa aina gani.
 
Da!amezibeba za wizara nin.mpaka kawakamata hao namin katumia pesa nying mno.hongera ngeleja.
 
Back
Top Bottom