Ngasa kwenda west ham!!

Wakimkubali itabidi apelekwe on loan kwanza nchi nyingine halafu ndo aletwe kwenye EPL nadhani.
Namwombea success lakini hizi ni trials tu so tusifurahi sana.
 
Thanks Balantanda. Huu mwaka mbaya kwa mnyamaaa,sie yeboyebo tunapeta lakini mambo yetu si mazuri ligi ya mabigwa
 
Acha kauzibe kijana....umesema sheria eti sijui nini kuwa ukitaka kucheza EPL uwe katika fifa ranking za 70........tupe link au paste sheria hizo sio maneno ya vijiweni bar.....

Na wewe uache uvivu wa kutafuta data, pitia website ya home office, FA, au ask a friend, mipaka ya uwezo wako wa kufikiri isiishie hapa JF. Kuna mambo mengi nayasoma hapa JF ambayo ni mageni kwangu na most of the time siyachukulii kama yalivyoletwa hapa, I take my time to do my own little research, ntakusaidia kwa hili mdogo wangu, hizi sio story za kahawa.......

Bofya hapa
http://www.thefa.com/TheFA/NewsFromTheFA/Postings/2008/11/Work_Permits_Players_PBS.htm
 
Dogo ana future nzuri inatakiwa aandaliwe mapema,hili la rank hata kama unaenda kucheza league daraja la pili ni lazima au ni premier league tu

Sheria ina appy kwa yeyote anayetaka kuja kucheza kama professional footballer, regardless ya division.
 
kana ka mzungu....sheria zingine haziwi applied pale......kuna wengi hawajachezea nchi zao lkn wanakipiga huko.....na hata hio 70 ranking hawapo......mfano Lua lua lomano.......
 
kana ka mzungu....sheria zingine haziwi applied pale......kuna wengi hawajachezea nchi zao lkn wanakipiga huko.....na hata hio 70 ranking hawapo......mfano Lua lua lomano.......

Nimekuambia usiwe unakurupuka kuandika mambo hapa, do your research first. Huyo Lualua unayemsema aliingia UK akiwa mtoto mdogo kabisa wa miaka tisa, cha ajabu we ndo umemchagua kumtolea mfano.
Nitakupa mfano mdogo tu- Banitez mwanzoni kabisa alipojiunga na Liverpool alitaka kumsajili Mark Gonzalez, winga mkali kutoka Chile. Hii deal ilifia home office kwa kuwa ranking ya Chile ilikuwa ni 72, na hii issue ya ranking ndo yenye uzito kuliko hizo nyingine zote.

Soma hapa- http://www.workpermit.com/news/2005_08_30/uk/sports_stars.htm
 
Wadau hii ni tetesi tu nadhani. Sheria za uhamiaji zinaweka wazi kwamba kibali cha foreign professional footballer kitatolewa endapo mchezaji anatokea kwenye nchi ambayo ni ya at least 70 kwenye FIFA ranking, kwa maana hiyo kama wewe u mtanzania hata uwe unakipiga kama Pele- visa hupati. Most of PL clubs watakachofanya kama kuna mchezaji mzuri kwenye nchi ambayo hai qualify ni kumsajili mchezaji huyo na kum loan out kwenye ligi nyingine ndogo za Ulaya kama Belgium au Swiss then after 3 year ndani ya EU wanagain hiyo qualification na ndipo wanawachukua.

I was also thinking about that clause kwenye sheria zao za kutoa vibali vya kazi, nakumbuka hilo suala lilijitokeza kwa yule mchezaji wa Liverpool kutoka Chile, somebody Sanchez kama sijakosea! Ila ni dalili nzuri kama Ngassa ameweza kuwashawishi West Ham na kumuhitaji, ni hatua moja mbele.
 
Salama wadau. Vipi yeboyebo kashatawaza ubigwa au Toto wamegomaaaaa?

Mlinda mlango Kaseja afunga bao la mwaka

Paulina David, Mwanza


BAO la mwaka la kipa Juma Kaseja lilitosha kuweka historia mpya kwa kuipa Yanga ubingwa wa 22 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza huku Azam ikiichapa 6-2 Villa Squad jijini Dar es Salaam.


Yanga iliyokuwa ikihitaji pointi tatu ili kutangazwa mabingwa kwa msimu wa 2008/'09, iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 21 lililofungwa na Kaseja aliyetumia vizuri udhaifu wa mwenzake, Abdallah Msafiri wa Toto Africa na kuachia mkwaju ambao ulidunda na kutinga nyavuni.


Awali, Kaseja alidaka na kupiga mpira mrefu wa juu uliokwenda moja kwa moja wavuni, dakika tisa baadaye Hussein Sued aliisawazishia Toto Afrika kabla ya Mike Baraza kufunga bao la pili na ushindi kwa mabingwa hao.


Katika mchezo huo ulioshuhudia timu hizo zikikosa penalti kila moja, mshambuliaji Mkenya Mike Baraza wa Yanga alikosa penalti dakika ya 18 kipindi cha kwanza, naye Said Dilunga alipoteza nafasi ya pekee ya kuisawazishia Toto wakati mkwaju wake wa penalti ulipoishia mkononi mwa Kaseja, dakika ya 62.


Naye Sweetbert Lukonge anaripoti kutoka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuwa jahazi la Villa Squad limezidi kuzama baada ya kukubali kipigo cha mabao 6-2 kutoka kwa Azam FC.


Mshambuliaji Nsa Job ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa ngome ya Villa kwa kupachika mabao matano peke yake na kuzawadiwa mpira akimwachia mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Danny Wagaluka akihitimisha karamu hiyo ya mabao kwa bao la sita.


Katika mchezo huo uliokuwa na raha ya aina yake, ulishuhudia mabao manne yakifungwa ndani ya dakika nane za mchezo huo, Azam ilipata mabao kupitia kwa Nsa Job, dakika ya 16 na 25 wakati Villa walisawazisha kupitia kwa Juhudi Samwel (19) na Lewede Dayton (24),kipindi cha kwanza na kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mapumziko.


Kipindi cha pili kilikuwa kibaya zaidi kwa Villa baada ya Nsa Job kufunga bao la tatu, nne na sita katika dakika ya 51,74 na 88, huku Mganda Wagaluka akipachika bao la tano (85).


Katika kile kilichoonekana kama kuchanganyikiwa na kipigo, mchezaji wa Villa , Launt Bagia alikosa penalti mwisho mwa mchezo, dakika ya 90 iliyopanguliwa na kipa wa Azam, Vladimir Niyonkuru.


Kutoka Mbeya, Brandy Nelson anaripoti kuwa mvua kubwa iliyokuwa inanyesha mjini humo ilisababisha mwamuzi Dominick Nyamsana kutoka Dodoma kuusimamisha mchezo huo katika dakika ya 28.


Mchezo huo baina ya Prisons na Kagera Sugar ulikuwa ukichezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa huku zikiwa zimefungana bao 1-1.


Akizungumzia kuahirishwa kwa mechi hiyo mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mbeya, Festo Nkemwa alisema mvua kubwa iliyojaza maji uwanjani ndiyo sababu ya kuahirishwa kwake.


Nkemwa alisema mvua hiyo ilisababisha wachezaji wa timu hizo kuanguka na kuweza kuhatarisha afya zao.


Naye mwamuzi Nyamsana alisema hadi uamuzi huo ulifikiwa kutokana na hali ya uwanja kutofaa tena kwa mchezo huo.


Mabao hayo, Prisons yalifungwa na Shaban Mtupa dakika ya nne, Haruna Hassan wa Kagera akasawazisha, dakika ya 18.
Source: Gazeti la Mwananchi
__________________
 
Back
Top Bottom