ney wa mitego

huyu dogo enzi hizo anaanza rap nilikuwa namfagilia sana. Anajua kwenda na biti. Mistari yake tata ila mizuri. Kila niliposikia wimbo wake niliacha ninachofanya na kusikiliza mashairi. Alijua kuyatunga na aliijua hiphop. Mara akaanza kubadilika na kuanza kubana pua. Mara akaja na hellow my love. Akabamba kinamna. Akanogewa akabana tena pua kwenye wimbo mwingine.
-akatoka tena na maunda- nakupenda we dada. Walichoimba sijakielewa hadi leo. Kelele tu.
- wakaja na kwaito. Kaimba humo alimradi tu.

Ney wa mitego soko la muziki linakupotosha. Kuimba waachie kina barnaba. Sauti yako si ya kuimba bali kurap. Mbona fid kadumu? We hardcore vipi? Unajifanya mtoto wa mama hupendezei. Go back to your roots, boy.
itafahamika rmx jamaa kasema "haiuzi hiphop wala bongo fleva,mziki wetu umegota"
 
kabla ya hii topic nilikuwa simjui ney wa mitego, nimeenda youtube na kusikiliza wimbo wa itafahamika, ni balaa, imetulia, nausikiliza kila dakika, acha nijaribu na hizo nyimbo zake nyengine nione amevurugaje.

kaharibu sana. Sio yule ney wa mitego tuliyemjua
 
itafahamika rmx jamaa kasema "haiuzi hiphop wala bongo fleva,mziki wetu umegota"

sijui nini kifanyike ili hiphop irudi. Mwana fa hajawahi kuimba ila bado yuko juu. Jo makini hajawahi kuimba ila anapata tuzo tu. Fid q sijawahi msikia akiimba. Cha msingi wanachotakiwa kufanya hawa wana hiphop ni kuwa na mistari iliyosimama kisha kuweka nakshi ya koras ya maana ambayo pia itabeba wimbo
 
Af kuna kipindi flani alisema ataenda kitu ka Germany kufanya porn movie, hy issue sijui ndo imeishia wapi...
 
Back
Top Bottom