ney wa mitego

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
huyu dogo enzi hizo anaanza rap nilikuwa namfagilia sana. Anajua kwenda na biti. Mistari yake tata ila mizuri. Kila niliposikia wimbo wake niliacha ninachofanya na kusikiliza mashairi. Alijua kuyatunga na aliijua hiphop. Mara akaanza kubadilika na kuanza kubana pua. Mara akaja na hellow my love. Akabamba kinamna. Akanogewa akabana tena pua kwenye wimbo mwingine.
-akatoka tena na maunda- nakupenda we dada. Walichoimba sijakielewa hadi leo. Kelele tu.
- wakaja na kwaito. Kaimba humo alimradi tu.

Ney wa mitego soko la muziki linakupotosha. Kuimba waachie kina barnaba. Sauti yako si ya kuimba bali kurap. Mbona fid kadumu? We hardcore vipi? Unajifanya mtoto wa mama hupendezei. Go back to your roots, boy.
 
nadhani dogo ameshikwa masikio kweli kweli. Na waliomghilibu wanaonekana kushinda
 
Aliimba kuwa itafahamika. Nadhani naye muda si mrefu anawekwa kapuni.
 
Ndo mambo ya virusi hayo HIPHOP haiuzi kaona abane pua hawa mapromota uchwara wanalazimisha wasanii kuimba wasichokitaka na wasikilizaji kusikiliza tusichokitaka ila kwa jinsi kinavyopigwa promo tunakizoea
 
Usifikili kazi rahis sana ya kutunga na kuimba,na wala usifikili rahisi sana kuingia studio,mwanamuziki anapoingia studio lengo kuwa na hadhira ukiona ww hakufurahishi kuna mwingine anafurahishwa kazi ngumu sana mwanamuziki kumlizisha kila msikilizaji wake hata Rip michael jackson kuna watu aliwauzi kwa tungo zake,so give him suport cos hata kuingia studio kunaitaji pesa na sio kitu rahis,kumponda hakutamsaidia huyu ney wako
 
jamaa nilimchanikia kama pimbi pale alivyoanza kuwadiss top guns wa game ya bongo!
 
Its true,jamaa ana sauti ya ku rap sio ya kuimba yoo

Great thinker habari yako yoo?

Hua tu wanifurahisha post zako hasa nikifananisha na jina lako... Sisemi kua sio GT ila tu si waelewa man kua akina "yooo" hua they don't brag about their great thinking....:eyebrows:
 
Nadhani Raia Fulani umesahau maneno ya Fid Q

"Watoto wanapenda kurap ila maboss wanapenda waimbe"
 
Nadhani Raia Fulani umesahau maneno ya Fid Q

"Watoto wanapenda kurap ila maboss wanapenda waimbe"

ndio maana nikamwambia hapo juu kuwa soko la muziki linawapotosha. Na hao mabosi waangalie kina nani wanajua kuimba, la sivyo hata mi nitaimba
 
kabla ya hii topic nilikuwa simjui ney wa mitego, nimeenda youtube na kusikiliza wimbo wa itafahamika, ni balaa, imetulia, nausikiliza kila dakika, acha nijaribu na hizo nyimbo zake nyengine nione amevurugaje.
 
Great thinker habari yako yoo?

Hua tu wanifurahisha post zako hasa nikifananisha na jina lako... Sisemi kua sio GT ila tu si waelewa man kua akina "yooo" hua they don't brag about their great thinking....:eyebrows:

Hiyo ID haimfai bora aendelee ku2mia ile nyingine.
 
huyu dogo enzi hizo anaanza rap nilikuwa namfagilia sana. Anajua kwenda na biti. Mistari yake tata ila mizuri. Kila niliposikia wimbo wake niliacha ninachofanya na kusikiliza mashairi. Alijua kuyatunga na aliijua hiphop. Mara akaanza kubadilika na kuanza kubana pua. Mara akaja na hellow my love. Akabamba kinamna. Akanogewa akabana tena pua kwenye wimbo mwingine.
-akatoka tena na maunda- nakupenda we dada. Walichoimba sijakielewa hadi leo. Kelele tu.
- wakaja na kwaito. Kaimba humo alimradi tu.

Ney wa mitego soko la muziki linakupotosha. Kuimba waachie kina barnaba. Sauti yako si ya kuimba bali kurap. Mbona fid kadumu? We hardcore vipi? Unajifanya mtoto wa mama hupendezei. Go back to your roots, boy.
tuu tuu twee,kijamaica zaidi.
 
Back
Top Bottom