Ney Wa Mitego Matatani Basata!!!

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,603
68,513
Ney wa mitego 2.JPG

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ney wa Mitego, yupo kwenye hatihati ya kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) baada ya kuachia remix ya wimbo wake wa Nasema Nao iliyojaa matusi na maneno makali dhidi ya wasanii wenzake na watu mbalimbali, King Kong III anakujuza

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Basata aliyeomba hifadhi ya jina lake kwani si msemaji rasmi, katika wimbo huo ulioanza kusikika mwishoni mwa wiki iliyopita, Ney wa Mitego ametumia lugha ya matusi na maneno yasiyo ya kistaarabu, huku akiwataja kwa majina watu aliowalenga, jambo ambalo ni kinyume na sheria za baraza hilo.

Baada ya kupata nyepesi hizo kutoka Basata, King Kong III alimtafuta Ney wa Mitego ambaye alisema kuwa wimbo huo wa Nasema Nao Remix umevujishwa na watu asiowatambua bila idhini yake lakini akaeleza kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka Basata juu ya kufungiwa

Baadhi ya Verses ya Wimbo huo ni:

Verse I
Tathmini inaonyesha ya kwamba heshima imeshuka
Game limechemsha mziki moshi unafuka
Ma Mcs wapo feki mashairi yao yananuka
Wanategemea kubebwa wakiachiwa wanaanguka
Leo ndio leo asemaye kesho muongo
Hapa nasema nao nawavunja mpaka migongo
Wasanii wa mikoani wote wameamia dar
Hawataki kurudi makwao nabaki kuwashangaa
rudini pande zenu tuachiane jiji letu
Mking'angania sana tutawageuza wake zetu
Ma mcs mmechakaa kama bibi nyakomba
Mnataka beat ya kapuka mkate viuno kama longomba
Hapa ni raha tu kama alivyosema AY
Kama ngumu kuingia mie naipaka KY
T kaa kati Ney kamata dimba
Mie niachieni hapa mbele niwatupie ndingaaaaa


Verse II
Naitawala dsm kama vile ghetto kwangu
Unamkuta demu wako na tatto ya sura yangu
I hate police,im the man of the people
Daudi Mwangosi kasimama mbele ya kristo
Lawama za qchief eti chid kamroga
suma mnazaleti na skendo ya ushoga
Mkari kwenye cypher daily natema lecture
Diamond kausika kumuua mganga wa nature
Star bongo wana search na yule jaji msagaji
Media ina wrong sight hii rap ndio mtaji
Malaya kama shilole anaua watoto wadogo
barnaba yound D Touch ,Ney wa mitego
Mistari yangu imenipa mpaka mke
Dunia ni yangu niacheni nikinukishe
Chid katoboa pua mie ndio basha wake
Ezekiel namjua umalaya ndio kazi yake


Kuupata Wimbo Click HAPA
 
asante king kong kwa habari hii,du! jamaa sijui anajiamin nini,mi pia sijapenda chid alivyotoboa pua,kumbe Nay ndio bahasha wake mh! kali ya mwaka
 
Huyu msanii sijui nini kinamfanya anajiamini kiasi hiki..nimemuona akihojiwa Star Tv kipindi cha Bongo Beat hata hana wasiwasi.
 
Huyu msanii sijui nini kinamfanya anajiamini kiasi hiki..nimemuona akihojiwa Star Tv kipindi cha Bongo Beat hata hana wasiwasi.

True Boy Mkong'oto jazz band na manzese army ndio tegemeo lake.
 
Huyu dogo anakaa manzese. anasema manzese haina rais madee anajiliwaza.
Hizi ndo nyimbo zake za siku zote. mi namkubali.
kuna sehemu anaimba "namuomba Mungu msichana anaye toa mimba nae afe hapo hapo". mia
 
jamaa yuko poa ila kusema wasanii wa mikoani waondke dar kachemka coz anajionesha km hajiamin tz m2 anaish popote.jiamini neema.haaaa!
 
Back
Top Bottom