News updates: UDSM kwawaka moto muda huu

Nchi gani wamefanikiwa kumpa mkopo kila mwanafunzi wa chuo kikuu.
 
hata hapa UK wanafunzi wanapewa mikopo unadhani wanatoa hela mfukoni? hata kama ada yao imepanda lakini bado mikopo wanapewa ambayo ni mlillion 20 za kibongo. wanachogomea ni kuwa kiasi hicho ni kikubwa sasa mtu kukirejecha ukilinganisha na kile cha mwanzo ambapo mwanafunzi alikuwa anarudisha 30% tu ya million 20.
 
Sweden, tena wanasoma bure co kwa mikopo

tena mpaka Phd ni bure isipokuwa tu kama unasoma PhD unakuwa kama umeajiriwa kwa kile kipindi unasoma hivyo stipend (ambayo kwao ni mshahara ) unakatwa PAYE
 
HAPA NDIPO HUWA NAMKUMBUKA Prof. Luhanga yeye alikuwa muwazi kwa serikali kuwa hawa wanawagomeeni ninyi (serikali) hivyo mnataka mimi nifanye nini, kwani nina hela? waache wagome ikifika siku ya tatu nafunga chuo. Nakumbuka siku moja waziri mkuu alimwambia tutafunga chuo yeye akamwambia uwezo huo hamna hata wewe waziri mkuu ukibandika tangazo hakuna atakaye ondoka ila mimi nikitoka notice ya masaa mawili tu huta muona mwanafunzi. Mukandara ni mnafiki alikuwa namcheka sana Luhanga enzi zake kuhusu migomo lakini kifupi kwa mukandara imekuwa mbaya zaidi.
 
ningependa kama watapata wazo waende bungeni, Tuligoma wakabadili viwango vya mikopo from 40% wakaleta utaratibu uliopo sasa, andamaneni na kushinikiza kuwa lazima kila mtanzania mwenye sifa za kwenda chuoni anapata Mkopo, do it for ur benefits and for the benefits of ur brother n sisters,tupo nanyi kiroho.
 
kumbukumbu zangu naamin ni sahii na ninakumbuka hlo kutokea Tanzania kuanzia wakati wa uhuru hadi late 1980's*

hilo liliwezekana kutokana na idadi ya wanafunzi waliokuwapo kwa kipindi hicho.

Idadi ya wanafunzi wanaosomeshwa na serikali kwa sasa inazidi ile ya miaka ya 80 kurudi nyuma.

Usijaribu kulinganisha maisha ya miaka ya 80 na haya ya sasa.
 
Polisi hawajawavamia ktk vyumba vyao na kuwakamata. Walikuwa wanafanya uhalifu.

Nyie tulieni msome, acheni kutumiwa na wanasiasa uchwara.[/QUOTE]

gamba utalijua tu.
 
unataka kuifananisha Sweden na Tanzania!. Hapa nazungumzia third world country.

Hyo ya 3rd world unaiongelea saiv kwenye comment yako hukusema hyo kitu. Nahc km wakurupuka tu
 
Acheni sheria ichukue mkondo wake. Acheni kuchanganya sheria na siasa.

Polisi wana kosa gani kuwakamata wahalifu. Wanaoandamana hovyo bila sababu ya msingi. Polisi wana wajibu wa kulinda usalama wa raia. Lazma iwashughulikie wote wanaojaribu kuhatarisha usalama wa watu wengine na nchi kwa ujumla.

Polisi hawajawavamia ktk vyumba vyao na kuwakamata. Walikuwa wanafanya uhalifu.

Nyie tulieni msome, acheni kutumiwa na wanasiasa uchwara.

kwa hiyoo mzee no loan unafikri itatokaje bila ya kugoma mkuu halafu unaendakusheherekea miaka 50 ya uhuni tanganyika kwanini usipeleke mshiko huo kwenye loan kwani hizo hela lazima zirudi na tena wameweka na interest..

pole sana mzee kwa kupenda kupost vitu bila ya kufikiria nini hasa mjadala una hitaji..
 
Nchi gani wamefanikiwa kumpa mkopo kila mwanafunzi wa chuo kikuu.

kama unaweza kutumia bil 2.3 kusomesha wafanyakazi 3 utashidwa kuwapa wengine mikopo midogo ya chuo,kumbuka awamu ya kwanza elimu ilikuwa bure mpaka univ
 
Bora tu wagome chuo kifungwe,imeniuma sn mdogo wangu hana wazazi hawajampa mkopo eti no priority.
 
Nchi gani wamefanikiwa kumpa mkopo kila mwanafunzi wa chuo kikuu.


Mkuu gadaf. istoshe sisi tunavyanzo vingi vya mapato sema viongozi wa nchi wameishiwa mawazo hawataki kushauliwa nchi yenye madini pande zote alidhi inayokubali mazao yote niayibu kuwa ombaomba
 
Nchi gani wamefanikiwa kumpa mkopo kila mwanafunzi wa chuo kikuu.


...Libya, walikuwa wanasoma bure kabisa hadi University level na wala sio mkopo! Sina uhakika na serikali mpya ya NTC labda wao wata-adopt sera za kinyama za kufaidisha watu wachache tu ndio wale keki ya taifa!!
 
unataka kuifananisha Sweden na Tanzania!. Hapa nazungumzia third world country.

blaza polepole. walisoma kabla hatujauza madini washindweje sasa? zinduka. tz si 3rd world ila ni ujinga wetu tu. na hata hao wanaosema hatuna maendeleo kama rwanda kwa kuwa nchi ni kubwa hawana haya. kwani uchina na tz wapi pakubwa?
 
Back
Top Bottom