News matokeo darasa la saba

Baba mtata

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
280
40
Habari wakuu
Katika taarifa ya habari ya clouds fm jioni hii saa 12 wamesema kuwa matokeo yametangazwa na asilimia za ufaulu zimepanda kwa asilimia 8.8 ukilinganisha na mwaka jana.Kawambwa amedai kuwa wasichana ndiyo waliofanya vizuri kuliko wavulana na kudai kuwa alama za juu ni 234 chini ya 250
My take mbona kuna thread zilikuja hapa na kudai matokeo ni mabaya sana sasa mbona Kawambwa anadai yameongezeka kwa asilimia 8.8?.
Nawasilisha
 
Hayo yamefanyiwa standardization! Ndiyo humo utakuta kuna waliofaulu wasiojua kusoma wala kuandika. Ndiyo matatizo ya kuchanganya siasa na taaluma.
 
kwa hiyo kama ufaulishwa umeongezeka kwa 8.8% tuna wasiojua kusoma na kuandika (8.8)/100 x5000 = 440 so wasiojua kusoma na kuandika ni approx 5440 kwa mwaka huu.(HAKI ELIMU)
 
Wanafunzi darasa la saba ni kweli kwamba wengi wao wamefeli. Kinachotangazwa ni wizi mtupu tena nadirikikusema kwamba ni ushenzi tena ushenzi wa viongozi wetu kwaa kushindwa kufanya kile ambacho wanatakiwa kukifanya.

Walimu kwa sasa hawana mori wa kufundisha hiyo ilikuwa ni kuficha aibu ya serikali. Wapo ambao mpaka sasa ajira zao ziko hatarini kwakuwa walikataa kuidhinisha matokeo hayo katika baraza la mitihani la tanzania. Ushuenzi mtuou huu. Asilimia ambazo zinaonyehwa ni za uongo. Wapo amabo wamechaguliwa kwa kupata asilimia chini ya hizo. Huu ni wehu na hasa wehu ya serikali ya ccm ambayo inaongozwa na watu ambao vichwa vyao havifanyi kazi sawasawa
 
hali halisi ndio hiyo ndugu yangu.siasa ndio inaharibu elimu ya tanzania.
 
Mwalimu wa shule ya msingi elimu yake duni, maisha yake magumu, kichwani kutwa anawaza ata survive vipi, halafu tunatarajia ataweza kufundisha vijana wetu vizuri, huu ni u-chizi. Hadi hapo serikali yetu itambue ni kwa nini elimu ya msingi iliitwa elimu ya msingi, hapo ndipo mambo yatakaponyooka.
 
Back
Top Bottom